Naomba ushauri, nimepewa hukumu ya kugawana mali na aliyekuwa mke wangu

Naomba ushauri, nimepewa hukumu ya kugawana mali na aliyekuwa mke wangu

kama mwenye kiwanja alipanga baada ya miaka 10 apauze kwa Tsh 80,000,000/= leo pana thamani pamoja na nyumba vyote 30,000,000/= unategemea mahakama kumpoka haki yake kwa kulazimisha auze hivyo hivyo?
Umeshawahi kufanyiwa land valuation yoyote au kuhudhuria?? Huwa inadili na vitu gani??? Nyumba siyo sehemu ya land valuation???
 
Pia NecZec ukithibitisha pia kuwa Wakili ni ndugu yake, kata rufaa kuwa Wakili ana maslah binafsi na mteja wake.

Kithibitisho unaonyesha Mahakama kuwa wana undugu wa karibu na wakili.
Conflict of interest
Mkuu wakili hata mwanao anaweza kuwa wakili wako nadhani,, Hakimu au jaji ndio changamoto kama akiwa na ukaribu na mmoja walalamikiwa au mlalamikaji .
 
Sheria za wapi hizo
Jamaa ameingizwa mjini tu hapo
Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971 (Law of Marriage Act, 1971), kifungu cha 160(1), ikiwa mwanaume na mwanamke wameishi pamoja kwa miaka miwili au zaidi, na katika mazingira ambayo jamii inawatambua kama mume na mke, basi kuna dhana ya ndoa inayoweza kutolewa na mahakama.

📜 Kifungu cha 160(1) cha Sheria ya Ndoa, 1971:
“Pale inapothibitishwa kwamba mwanaume na mwanamke wameishi pamoja kwa miaka miwili au zaidi, katika mazingira ambayo wamepata sifa ya kutambulika kama mume na mke, basi kutakuwa na dhana inayoweza kupingwa kwamba walikuwa wameoana kihalali.”

✅ Vigezo vya kutambuliwa kwa dhana ya ndoa:
  • Kuishi pamoja kwa miaka miwili au zaidi.
  • Jamii inayowazunguka kuwatambua kama mume na mke.
  • Kuishi kama wanandoa, ikiwa ni pamoja na kushirikiana majukumu ya kifamilia.

⚠️ Mambo ya kuzingatia:
  • Dhana hii si ndoa halali moja kwa moja, bali ni dhana inayoweza kupingwa mahakamani.
  • Inatumika hasa katika mazingira ya migogoro ya kifamilia, mirathi, au madai ya matunzo.
  • Ikiwa dhana hii itathibitishwa, mmoja hawezi kuoa au kuolewa tena bila kupata hati ya kuvunja ndoa kutoka mahakamani [1] .

📚 Rejea:
  • Sheria ya Ndoa ya Tanzania, 1971, kifungu cha 160(1).
  • Kesi ya Kimba v. Kimba, ambapo mahakama ilitambua dhana ya ndoa baada ya wanandoa kuishi pamoja kwa muda mrefu [2] .

Ikiwa unahitaji msaada zaidi kuhusu haki zako au hatua za kuchukua katika hali kama hii, ni vyema kushauriana na wakili au kituo cha msaada wa kisheria kilicho karibu nawe.
 
Mapenzi/mahusiano huwa yana expire

Ova
 
Mimi na mpenzi wangu tuliyeishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili tuliachana baada ya mwanamke huyo kuanza visa na akaenda nyumbani kwao. Badae akaibukia mahakamani akiomba talaka na mgawanyo wa mali akiongozwa na wakili mmoja hivi ambae ni ndugu yake.

Moja ya mali ni nyumba ambayo mahakama imeona tumechuma pamoja lakini mahakama hiyohiyo amejiridhisha kuwa kiwanja ni mali yangu peke yangu. Sasa mahakama imeagiza nyumba iuzwe tugawane kwa asilimia ambazo mahakama imeziona. Mimi sitaki kuuza kiwanja changu ambacho mahakama pia imedhibitisha kuwa ni mali yangu pekee yangu ila nyumba ambayo imejengwa ndio imeonekana tumechangia kujenga na huyo mwanamke. Je hii hukumu itatekelezeka vipi kisheria maana ndio tunasubili uthamini?
Ibomoe mgawane matofali halafu ujenge kwenye kiwanja chako. Usikubali iuzwe maana na kiwanja chako kitauzwa.
 
Dah pole sana bro NecZec .

Mm Sio mwanasheria

1. Tathimini ikitoka means mgawanjo ww utapata 2/3 (una Kiwanja na nusu ya thaman ya nyumba)

2. Subiri tathmini alaf ukae mezan na huyo mtalaka wako ili ww umlipe kias chake 1/3 kama hela , ila nyumba usiuze.

Sometimes sio kila vita inabidi upigane, nyingne unaona kabisa ukipigana utashindwa na unapotezana kabisa .
Kuwa mpole , cheza na akili, bidada akubali ili ww umlipe hela bila kuuza nyumba.
Yawezekana Jamaa kwa sasa uchumi umeyumba na hataweza kumlioa
Mara nyigi hawa hugeuka baada ya sisis uchumi kuyumba
 
Dah ndoa za kikristo zinachosha sanaa

Yani nyumba iuzwe kisa kaachika? Na huko si ndo mnaposema mpk kifo kikutenganisheni? Mmmmhhh sheria za kibinadamu ni kandamizi zaidi
 
Kama hujamuoa huyo mwanamke uza hiyo property halafu jikaushe .
Akikupeleka mahakamani mzungushe wee baade mfanye tathimini ya mchango wake aliotoa kwenye ujenzi wa hiyo nyumba zen mlipe.
Ila wanaume wengine hivi unaanzajeanzaje kujenga nyumba kwa kushirikiana na mwanamke? Ila watu wengine mna moyo.
Mimi kuna mwanamke huko mwanza tuna mtoto yeye alikuwa anafanya kazi benki.
Mimi kutokana na kazi yangu nilikuwa na connection na watu wa halmashauri akina tukae na marehemu kabwe kila wakitangaza wanauza viwanja lazima niloby nipate nikawa na viwanja 3 .
Sasa yule bi dada hakuwahi kupata kiwanja hivyo vya halmashauri sasa akaniambia eti nibadili umiliki wa kiwanja kimoja kisome jina lake ili apeleke hiyo hati ofisini kwao (benki) apewe mkopo ajenge kwenye hicho kiwanja halafu eti baada ya hapo atakuja kuongeza jina langu kwenye hiyo hati mimi wakati huo tayari nina nyumba yangu hapo mwanza.
Kusema kweli nilimkatalia nikamshauri anunue jamaa wa halmashauri walikuwa wanajimilikisha viwanja hakafu baadae wanauza bei ndogo tu yeye akawa anang'ang'ania cha kwangu akibadilishe akakope ndipo atapata hela.
Kusema kweli alishindwa kunishawishi yaani ikabidi tuachane mazima manake alikuwa analalamika simuhamini wakati tuna mtoto
Mbona hiyo sababu ndogo sana ya ninyi kuachana?, wote hapo mna kosa, ww humuamini, na yeye huenda alikuwa na ajenda zake za siri, ndo maana alikuacha evangelical
 
Dah ndoa za kikristo zinachosha sanaa

Yani nyumba iuzwe kisa kaachika? Na huko si ndo mnaposema mpk kifo kikutenganisheni? Mmmmhhh sheria za kibinadamu ni kandamizi zaidi
Mkuu siyo ndoa ya Kikristo wala ya Kimila ni Mwanamke alimfata Mwanaume wakaanza kuishi pamoja kama mke na mume, yani ata wewe kama ni Muislam ungefanya hivyo yangekukuta tu yalivyo mkuta huyu Mwenzetu.
 
Dah ndoa za kikristo zinachosha sanaa

Yani nyumba iuzwe kisa kaachika? Na huko si ndo mnaposema mpk kifo kikutenganisheni? Mmmmhhh sheria za kibinadamu ni kandamizi zaidi
Umesikia wapi kwamba huyo jamaa alikuwa na ndoa ya Kikristo?
 
Kaeni mtumie tu ubinadamu hapo lazima huyo binti aumie,mgawie kilicho chake maisha yaendelee,hata kama ni asilimia thelathini
 
Dah ndoa za kikristo zinachosha sanaa

Yani nyumba iuzwe kisa kaachika? Na huko si ndo mnaposema mpk kifo kikutenganisheni? Mmmmhhh sheria za kibinadamu ni kandamizi zaidi
Wewe una hasira tu dhidi ya ukristo.
Umesoma vizuri maelezo ya mleta mada?
Amesema hawajafunga ndoa bali walikuwa wanaishi tu kama mume na mke kwa miaka kadhaa wakajenga nyumba wote ktk kiwanja cha mwanaume.
 
Back
Top Bottom