Hukumu Rufaa ya Godbless Lema yaiva

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
RUFAA ya kupinga kuvuliwa ubunge ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), imepangwa kusikilizwa Septemba 20, mwaka huu, mbele ya majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa; Natalia Kimaro, Mbarouk Salim Mbarouk na Salum Massati.

Kwa mujibu taarifa za kikao cha Mahakama ya Rufaa cha Arusha, rufaa hiyo iliyofunguliwa na Lema akipinga uamuzi uliotengua ubunge wake kufuatia shauri lililofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, inatarajiwa kusikilizwa kwa siku moja ambapo baada ya hapo itapangwa tarehe kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Awali, Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.

Kwenye baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.

Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Katika madai mengine, Lema anamlalamikia, Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa, alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Lema anadai kuwa, Jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.

Kesi hiyo iliyotengua ubunge wa Lema, ilifunguliwa na wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM); Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, wakidai kuwa wakati wa kampeni mbunge huyo alimdhalilisha mgombea mwezake, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.


Source: Tanzania Daima
 
We expect good newz from court of appeal abt our hero'z destiny..apewe u MP wake.salum massati'z smart
 
Nataka haki itendeke, Naona kuna vuguvugu la kuhama kutoka utawala wa kisheria na kidemokrasia, tunaelekea kwa uhitaji la wachache, mahakama iko mfukoni mwa wenye uwezo, hazitendi haki ipasavyo.

Mwisho wa siku,ukweli hujipambanua wenyewe, kesi ya Lema ni bifu za kisiasa na mahakama kutothamini umuhimu wa haki.
 
Subirini atakavyoumbuliwa na rufaa yake angeenda zake tu Kaloleni kuuza mbege
 
RUFAA ya kupinga kuvuliwa ubunge ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), imepangwa kusikilizwa Septemba 20, mwaka huu, mbele ya majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa; Natalia Kimaro, Mbarouk Salim Mbarouk na Salum Massati.
Hapo kwenye red kuna walakini hebu soma hapa chini ushahidi wa Mh. Tundu Lissu (MB) kama ulivyonukuliwa kwenye utetezi wake kwenye kamati haki, maadili na madaraka ya Bunge.

JAJI WA RUFAA MBAROUK SALIM MBAROUK

Mbarouk Salim Mbarouk aliteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania mwaka 2008. Kabla ya uteuzi huo Jaji Mbarouk alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Sifa za mtu kuteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa zimeainishwa katika ibara ya 118(3) ya Katiba:


"Majaji ... wa Rufani watateuliwa na Rais, kwa kushauriana na Jaji Mkuu, kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ... zilizoainishwa katika Ibara ya 109 ya Katiba au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zinazotumika Zanzibar na wamekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano."


Kwa mujibu wa Ibara ya 94(3) ya Katiba ya Zanzibar, 1984,
"Mtu hatoweza kuteuliwa kuwa Jaji au Kaimu Jaji wa Mahkama Kuu mpaka awe na shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu kinachotambuliwa au Chuo cha aina hiyo; au awe au amewahi kuwa Jaji wa Mahkama zilizofanana na hii kwa kesi zote za jinai na madai katika Tanzania au sehemu yoyote ya Jumuiya ya Madola au Mahkama ya Rufaa kutoka Mahkama hizo; au awe Mwanasheria wa Zanzibar au Tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka saba; au awe na uzoefu wa Jaji au mwanasheria kwa pamoja usiopungua miaka saba."

Jaji Mbarouk hajatimiza hata moja ya masharti hayo ya Katiba ya Zanzibar. Jaji huyu hana shahada yoyote ya sheria inayotambuliwa na mamlaka ya ithibati ya Tanzania kama inavyotakiwa na Ibara ya 109(7) ya Katiba.

Jaji huyu ana stashahada ya juu ya sheria (Post Graduate Diploma in Law) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shahada ya Uzamili ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha nchini Uingereza.

Uteuzi wa Jaji Mbarouk kuwa Jaji wa Rufaa ulileta minong'ono mingi katika taaluma ya sheria kiasi kwamba marehemu Wakili Leopold Kalunga anasemekana kufungua shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania kutaka uteuzi huo utenguliwe. Hata hivyo, Wakili Kalunga alifariki kabla ya shauri lake kusikilizwa na kwa hiyo liliondolewa mahakamani.

Aidha, monong'ono hiyo ilimfanya Jaji wa Rufaa Mbarouk kujiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambako bado ni mwanafunzi hadi ninapoandika Addendum hii.
 
Hao majaji wawili watasomeshwa na ta scholar kulinda maslahi kama alivyosomeshwa yule jaji kwenye kesi ya Mpendazoe.
 
Imekaa vizuri Lema atarudi bungeni namuamini sana jaji Salum Massati 99.9% pia na Natalia Kimaro 80% lakini huyu walakini Mbarouk Salim Mbarouk 50%
 
Molemo
hapa hamna kitu Lema atulie tu aendeleee na kazi yake ya ujangiri kama zamani na kukwiba magari ya watu Arusha kama alivyotuhumiwa na Zombe kwakuwa wanajuana vizuri..

Ubunge asahau kwa sasa
 
Last edited by a moderator:
Yule Jaji wa Mahakama ya Rufaa asiye na sifa sitahiki,mwenye dipoloma ya sheria tu ,naye ni mmoja wa majaji kwenye jopo hili.

Nadhani msajili wa mahakama alilipanga hili kabla ya Nondo za Tundu Lissu kuvuja.
 
We expect good newz from court of appeal abt our hero'z destiny..apewe u MP wake.salum massati'z smart..........

Masati anaweza kuwa smart, what about Mbarouk Salim? Si ndiye jaji tuliyeambiwa na Lissu kuwa ndio kwanza anasomea shahada ya kwanza ya sheria chuo kikuu huria?

Nina wasiwasi hata yule wakili Kalunga aliyefungua shauri kupinga uteuzi wa jaji huyu alipigwa kipande.

Usiweke matumaini ya kupata haki kwenye mahakama za majaji wa aina hii.
 
Imekaa vizuri Lema atarudi bungeni namuamini sana jaji Salum Massati 99.9% pia na Natalia Kimaro 80% lakini huyu walakini Mbarouk Salim Mbarouk 50%
Unatumia kigezo gani kumpa 50% mtu ambaye hana hata sifa ya kuwa hakimu mkazi?
 
hapa hamna kitu lema atulie tu aendeleee na kazi yake ya ujangiri kama zamani na kukwiba magari ya watu arusha kama alivyotuhumiwa na zombeee kwakuwa wanajuana vizuri..ubunge asahau kwa sasa
kweli wewe mfuasi wa MABWEPANDE una shida!! Bado unamshabikia jambazi lenzako la MABWEPANDE of all the persons of this world!! ZOMBE!! oh my GOD you are not serious.
 
Hivi Lema akishinda rufaa baadaye CCM wakaipinga kwa kigezo cha jopo la majaji ku- include mtu ambaye si jaji itakuwaje? Technically huyu mzanzibar si jaji.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom