Hukumu kesi ya MV Bukoba na mafunzo kwetu

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,562
HUKUMU KESI YA MV. BUKOBA NA MAFUNZO KWETU.

Na Bashir Yakub.
+255 784 482 959.

( A ).NAMBA YA KESI.

Kesi ya Jinai Na. 22/1998, Mahakama kuu Mwanza , Mbele ya Jaji Mlay.

( B ) WASHITAKIWA.

  1. Kapteni Jumanne Rume Mweiru. Huyu ndiye alikuwa Kapteni siku ya tukio, akiendesha toka Bukoba VIA kemondo Bay hadi Mwanza.
  2. Gilbert Mokiwa. Huyu alikuwa mkaguzi wa meli, na ndiye alikuwa na wajibu wa kuikagua MV Bukoba.
  3. Alphonce Sambo. Huyu alikuwa afisa bandari Bukoba, na wakati meli inaanza safari yeye na wenzake waliratibu safari.
  4. Prosper Rugumila.Huyu alikuwa afisa bandari kemondo ambapo MV Bukoba ilipitia ikitokea bandari ya Bukoba na kuongeza abiria na mizigo.
( C ) KOSA WALILOSHITAKIWA NALO.

Kuua bila kukusudia kinyume na kifungu cha 195 cha Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania.

( D ) MAELEZO YA KOSA.

Kuwa, tarehe 21 / 5 / 1996 majira ya saa 7 :30 asubuhi, eneo la ziwa Victoria Mwanza washitakiwa kwa uzembe walisababisha meli ya MV BUKOBA iliyokuwa ikitokea Bukoba kuelekea Mwanza kupinduka na kuzama ,na hivyo kusababisha vifo vya watu 159.

( E ) MASHAHIDI UPANDE WA MASHTAKA.

Upande wa mashitaka ulileta mashahidi 32 wakiwemo ;

  1. Kapteni Cleophas Magoge . Huyu saa 8 : 15 asubuhi,aliitoa MV VICTORIA bandarini Mwanza ilipokuwa inaendelea na matengenezo na kulazimika kuiendesha kuelekea kwenye eneo la ajali baada ya kuambiwa kuwa MV BUKOBA imezama.
Anasema alipofika eneo la tukio aliiona MV Bukoba ikiwa kichwa chini miguu juu, huku mizigo hasa ndizi,watu, na miili mingi ikielea majini. Na aliposogea karibu alimuona Kapteni wa MV Bukoba mshitakiwa wa kwanza akiwa ananing’inia juu ya meli iliyozama.

  1. Shahidi mwingine ni Kapteni Mannase Ephraim Kombo. Huyu anasema siku ya tukio alikuwa akiendesha MV BUTIAMA kutoka Port Bell Uganda kuelekea Mwanza. Anasema saa 6 :00 za asubuhi aliingia kwenye radio na kuwasiliana na bandari ya Mwanza kuwa atafika saa 9 : 00 asubuhi.
Anasema wakati akiwasiliana alisikia Kapteni wa MV Bukoba naye akiwasiliana kuwa atafika mwanza saa 8 :00 asubuhi. Anasema alifika bandari ya Mwanza saa 9:00am akashusha mizigo lakini MV Bukoba iliyosema kufika saa 8:00am haikuwa imefika.

Anasema, baadae alimsikia MPANGALA aliyekuwa muongoza meli siku hiyo akiiita MV Bukoba kwenye radio bila majibu. Anasema MPANGALA aliita sana mpaka akaamua kutoka nje kutizama, na kwa mbali saana aliona kitu ambacho hakukielewa. Alirudi ndani na kuchukua hadubini(binocular) kutizama tena, na hapohapo alimsikia akiongea kwa mshtuko kuwa MV Bukoba inazama.

Anasema maramoja aliamua kuiendesha MV BUTIAMA kuelekea eneo la tukio ambapo alikuta mitumbwi kadhaa ya wavuvi ikiokoa watu, na aliona maiti nyingi, watu hai, na mizigo vikielea.

  1. Shahidi mwingine ni meneja wa yard ya meli Mwanza. Anasema siku 29 kabla ya kuzama yaani april MV Bukoba ilikuwa na matatizo ya kuyumba ambayo pia yalithibitishwa na mashahidi wengine. Anasema, mtaalam kutoka Ubelgiji ambao ndio waliotengeneza meli hiyo aliletwa kuchunguza tatizo hilo na aliifanyia majaribio katika eneo liitwalo Karumo.
Mtaalam aligundua matatizo ya kuyumba na akasema watatoa ripoti mwezi wa 7 /1996, lakini meli ikazama mwezi 5/ 1996 miezi miwili kabla ripoti kutolewa.Anasema lakini baada ya majaribio hayo kuanzia tarehe 12 / 5 / 1996 meli ilifanya safari tatu, mbili Mwanza – Port bell Uganda , na moja Mwanza – Kisumu Kenya, na ya nne ndio ilikuwa ya mwisho ya Mwanza- Bukoba.

Anasema siku hiyo MV BUKOBA ilienda Bukoba lakini haikuwa imepangiwa kwenda huko, na badala yake MV VICTORIA ndiyo iliyokuwa imepangiwa kwenda Bukoba. Anasema MV Victoria ina uwezo wa kubeba abiria 1200, na tani za mizigo 250 wakati MV BUKOBA ina uwezo wa kubeba abiria 400, tani za mizigo 85.

Anasema kwahiyo tiketi za abiria na mizigo zilizoandaliwa huko Bukoba zilikuwa ni za MV Victoria kwasababu ndiyo ilitakiwa kwenda. Kutokana na hitilafu za injini ikashindwa kwenda na ikabidi ibadilishwe na MV BUKOBA na hivyo MV Bukoba ikafanya kazi ya MV Victoria.

  1. Munaf Hussein Ibrahim Punja ni abiria aliyenusurika katika hiyo ajali. Anatoa ushahidi kuwa alipanda meli saa 9:00 pm bandari ya Bukoba na watu walikuwa wengi pamoja na mizigo. Anasema meli ilikuwa inakwenda upande. Anasema walipofika Kemondo saa 10 ;00 usiku alishangaa kuwaona David pamoja na Mutayoba ambao aliwaacha bandari ya Bukoba na hawakuwa wamepanda meli.
Anasema aliwauliza kulikoni, wakamwambia kuwa kule Bukoba bandarini walizuiwa kuingia kwenye meli kwasababu ilijaa kwahiyo wakaamua kuchukua Taxi kuja kuisubiria Kemondo Bay. Anasema hapo Kemondo walipanda na wakasafiri wote.

  1. Zabron Kasindirano naye ni abiria aliyenuurika. Anasema meli ilipofika Kemondo Bay alimuona shemeji yake Francis Justusi Kaganji na kushangaa kwasababu walimuacha Bukoba. Anasema alimuuliza amefikaje Kemondo akamwambiwa alipanda taxi baada ya kuzuiwa kupanda bandari ya Bukoba.
Anasema saa 7 :00 asubuhi wakati wamekaribia kufika meli ilianza kuyumba sana. Anasema alikuwa amekaa na wanawake akawaambia wapande juu kuchukua “life Jacket” lakini wakamcheka kuwa ni mwanaume muoga na hivyo kwa hofu ya kutoonekana muoga naye hakuchukua tena Jacket.Anasema haikupita dakika 10 tokea aambiwe muoga meli ikapinduka, akatupwa kwenye maji karibia na mkungu wa ndizi ambao aliushikilia mpaka akaokolewa, na kuwa wale wanawake hakuwaona tena.

Mashahidi walikuwa wengi ila kwa kutaja ni wachache.

( F ) ILI WATUHUMIWA WAPATIKANE NA HATIA YALITAKIWA KUTHIBITISHWA MAMBO YAFUATAYO.

  1. Kwamba meli ilikuwa na matatizo ya kiufundi(ya kuyumba) na wao hawakuyashughulikia/kuyajali au kuzingatia matatizo hayo.
  2. Pili, waliijaza meli watu kuzidi uwezo wake.
  3. Tatu, waliijaza meli mizigo kuzidi uwezo wake.
MATATIZO YA KIUFUNDI.

Hii ilishindwa kuthibitika kwasababu kwanza hakukuwa na rekodi yoyote ya mafundi na wataalum akiwemo yule Mbelgiji, iliyozuia meli kuendelea kufanya kazi. Hakukuwa na shaka kuwa meli ilikuwa na matatizo ya kuyumba ila haikuzuiwa kufanya kazi.

Pili, hakukuwa na ushahidi wa kisayansi ulioonesha kuwa matatizo ya kuyumba ndiyo yaliyopelekea meli kuzama.

KUJAZA WATU KULIKO UWEZO.

Hii nayo ilishindwa kuthibitika kwasababu hakukuwa na rekodi sahihi ya watu waliongia kwenye meli. Baadhi ya vitabu vinaonesha 400, vingine 700, vingine 759 nk.

Pia idadi ya watu ilioneshwa kwa kuangalia tiketi zilizouzwa. Hakukuwa na ushahidi wa kuonesha waliongia ndani ya meli yaani waliosafiri walikuwa wangapi. Mashahidi nao wanathibitisha kuwa kununua tiketi sio kusafiri, unaweza kununua tiketi halafu usisafiri. Kwahiyo ni vigumu kupata idadi ya waliosafiri kwa kuhesabu tiketi zilizouzwa.

Kitabu cha uhakiki wa wasafiri ambacho hutumiwa na wakaguzi ndani meli inapokuwa safarini ndicho kinaweza kuthibitisha waliosafiri yaani waliokuwa ndani ya meli, na hivyo kujua kama ilizidisha au hapana. Hata hivyo kitabu hicho nacho kilizama, na hivyo kukosa ushahidi wa kujua mpaka meli inazama ilibeba abiria wangapi, na hivyo kuweza kutambua kama walikuwa wamezidi ama hapana.Hii nayo ikafia hapo.

KUJAZA MIZIGO KUPITA UWEZO.

Hii nayo haikuweza kuthibitishwa. Hakuna rekodi Bukoba bandari kuwa zilipakiwa tani ngapi ,na hakuna rekodi Kemondo Bay ziliongezwa tani ngapi. Unawezaje kusema ilizidisha mizigo kwa ushahidi wa macho tu bila rekodi sahihi ya mizigo.Hii nayo ikafa.

( G ) HUKUMU.

Kama hakuna ushahidi kuwa ubovu wa meli ndio uliosababisha izame, kama hakuna ushahidi kuwa meli ilipakia abiria wengi kuliko uwezo wake, kama hakuna ushahidi kuwa meli ilipakia mizigo kuliko uwezo wake, nini kilichobakia zaidi ya kuwaachilia huru washitakiwa wote wanne.

Mahakama ikaona washitakiwa wote wanne hawana hatia , ikaamuru waachiliwe huru mara moja.

( H ) TUNAJIFUNZA NINI.

Ajali zote za majini, kuanzia hii ya MV Bukoba, Spice Islanders Zanzibar, mpaka sasa Mv nyerere, nk, hadithi ni moja tu, kuzidisha abiria na mizigo. Pamoja na hayo katika ajali zote hizi, hakuna mtu unayeweza kumsimamisha akwambie idadi halisi kabisa,ile yenyewe ya watu waliokuwemo na akakwambia. Huu ni ukweli. Hayupo, na narudia hayupo. Si mkata tiketi, si mkaguzi anayesafiri na meli, si kapteni, si ofisa wa bandari, hakuna. Ndio maana utaona inatajwa idadi ya waliokufa leo, kesho wanasema mwili mwingine umegunduliwa na hivyo waliokufa idadi imeongezeka na kufikia kadhaa.

Hakuna mtu wa kukwambia waliosafiri ni 100, walionusurika ni 50, tuna maiti 30, na hivyo sasa hivi tunafuta maiti 20 TU tufunge zoezi. Hakuna wa kutoa takwimu kama hii. Ajali zikitokea tunakaa mwaroni tunasuburi chochote ambacho kitatemwa na ziwa ndicho tunachobeba na kuongeza kwenye idadi. Ziwa lisipotema tunasema basi wameisha. Hatuwezi kusema kwenye idadi yetu anakosa maiti mmoja na ndiye tunamtafuta kwasasa, katu hatuwezi. Kweli dunia hii ya karne ya 21 hatuwezi hata kujihesabu hata kwa kutumia vidole na vijiti ?, Kweli. ?.

Mbona huku kwenye usafiri wa anga idadi iko wazi na inajulikana. Utaambiwa abiria waliosafiri,na sio waliokata tiketi, bali waliosafiri ni 257, watumishi wa ndege(crew) ni 10, na hivyo waliokuwemo jumla ni 267. Na inakuwa hivyohivyo kweli hakuna kubabaisha. Kwanini haiwi hivyo kwenye meli/vivuko. Leo ni miaka 22 tangu MV Bukoba izame, nakuhakikishia hakuna wa kukwambia idadi halisi ya waliofariki katika ajali hiyo, hayupo. Leo ni miaka 7 tangu MV Spice Islanders izame, nakuhakikishia hakuna wa kukwambia idadi halisi ya waliofariki katika ajali hiyo, hayupo. Na leo nasema hakuna wa kukwambia idadi halisi kabisa ya waliofariki kwenye kivuko cha MV Nerere, hayupo. Na huu ndio ukweli. Kadhalika katika meli zote hizo hakuna wa kukupa idadi ya tani halisi ya mizigo iliyokuwemo bila kubabaisha, hakuna.

Sasa unaweza kujiuliza tunakabiliwa na tatizo gani hasa, hatujui hesabu hizihizi za kuhesabu 1-10 na.....,ni wazembe, ni wasiojali,ni wapuuzi, ni watu ambao bado tunaishi maisha ya ujima,ni watu wa aina gani hasa. Watu ambao ulaya, America na uchina wameanza kugawana maeneo mwezini ili wachimbe madini ya PLAGIOCLASE sisi hatuwezi hata kuhesabiana kwa hesabu ya darasa la kwanza.Tuseme nini hiki kama sio janga. Na hakuna shaka kushindwa kuhesabiana ndiyo sababu ya ajali za majini . Hatuna ajali ya majini ambayo idadi ya watu ilikuwa sawa(capacity). Zote idadi ilizidi.

Tizama pale feli kigamboni. Vinafanya kazi vivuko vitatu kwa kupishana na wote tiketi mnachukua sehemu moja. Kama kinazama kivuko kimoja pale(mungu aepushie mbali) nani anaweza kusema idadi ya waliokuwemo. Kwasababu hata tukisema tuhesabu tiketi bado hutopata jibu kwakuwa tiketi za kupanda kivuko chochote kati ya vitatu zinakatwa sehemu mmoja, hivyo huwezi kujua aliyekata tiketi amepanda kivuko kipi kati ya vitatu.

Lakini tizama watu wanavyoingia kwenye kivuko. Geti likifunguliwa mpaka mtu mwenyewe aseme kimejaa sana siingii, vinginevyo watu wote mlioko kwenye banda la kusubiria mtaingia. Kivuko hiki kinabeba watu wangapi kwani. Kikija kidogo wanaingia haohao, kikija kikubwa wanaingia haohao, Looh.Mwanzoni nilifikiri kwakuwa safari ya feli - kigamboni ni ya karibu sana basi sio rahisi kutokea janga, lakini MV Nyerere imenifunza mengi.

Hoja ni kwamba, kama huwezi kujua na ukawa na idadi halisi ya waliosafiri maana yake huwezi kudhibiti upakiaji unaozidi uwezo wa chombo. Kwanini, kwasababu unajua chombo kinahitaji kupakia wangapi, lakini hujui wanaoingia huwa ni wangapi.Na hapa ndipo yalipo majanga.

Sasa tubadilike, yatoshe tuliyofunzwa na ulimwengu. Tunahitaji mifumo mizuri ya kuratibu upakiaji wa abiria na mizigo katika vyombo vya majini. Uratibu unaanza na nani anawajibika na nini, vifaa vya kutambua watu wanaoingia kusafiri, na sio mashine za kukatia tiketi tu, usimamizi wa kiwango cha juu kwenye vituo vya meli na vivuko, kuondoa rushwa meneo hayo,mfumo wa uongozi katika bandari na meli unaoanisha kwa uwazi wajibu wa kila mfanyakazi. Isiwe kama ya MV Bukoba kapteni anasema, ni chief officer, chief officer anasema ni 1st officer, 1st officer anasema ni marine surveyor, marine surveyor anasema port officer, yaani unakosa hata awajibike nani katika nini mpaka mwisho watu wote wanaachiwa huru. Mfumo mzuri wa nani anawajibikia nini.

Watu wa marine wachukue semina ya usimamizi wa abiria na mizigo kwenye viwanja vya ndege. Hakuna dhambi umakini uleule unaotumika kwa abiria na mizigo kwenye viwanja vya ndege ukatumika maeneo ya bandarini kwasababu pote zinabebwa roho za watu. Kwanini huku ionekana tahadhari kubwa ya abiria na mizigo wakati huku hakuna, na wanaobebwa wote ni watu. Tusipofanya hivyo tukaendelea na uenyeji enyeji wetu huu, tujiwekee guarantee ya kupokea misiba ya majini kila baada ya kipindi fulani.

Narudia tena tatizo lipo kwenye upakiaji, soma ripoti zote za ajali za meli ni abiria na mizigo kuzidi. Hapa ndipo tunatakiwa kushughulika napo. Yanitoshe haya kwa leo.
 
Wajifunze wamelogwa, watanzania? Wafu ?
A very renowned Judge , Mlay! Hukumu safi in all fours of law!
 
Attachments

  • MV BUKOBA CASE MLAY JUDGE.docx
    94 KB · Views: 193
Asante sana Bashiru kwa uchambuzi huu,tatizo tumekuwa watu wa kutafuta suluhu baada ya majanga,inauma n.a. kusikitisha.
 
Kweli sheria na matamko ni sawa na maji na mafuta!! Ila hili la mv bukoba, halikuendeshwa kwa mizuka ya siasa kama hili jingine!! Viongozi waliacha sheria ifuate mkondo wake, na hata watuhumiwa walipoachiwa huru hukusikia wanasiasa wana lalamika!! Ila hili la zamu hii ngoja tusubilie!! Kwani sheria haiendi unavyotaka wewe!! Ila wao watalazimisha iwe wanavyotaka wao!! Hata ukijaribu kuangalia toka mwanzo ukamataji wa wahusika uliongozwa na mzuka!! Mala ohh captain hakuwepo lazima akamatwe huko aliko!!!
 
hii ajali ya MV Nyerere wamekufa watu wengi sana kuliko hata Mv Bukoba ila imepotezewa kama hakuna kilichotokea.
 
Ni bahati mbaya, tena sana na hili la Mv Nyerere tutalisahau kama yalivyopita mengine. Kwa wenzetu majanga ni mafunzo sisi tunadhani 'kuna mkono wa mtu' sijui 'kafara', poor reasoning, stupid thinking!

Itoshe tu kusema, Mungu azilaze pahala pema roho za marehemu!
 
Tumeshindwa kusimamia wenyewe basi tufuate mifumo inayotumiwa na nchi nyingine... Hapa naona rushwa sana na tamaa ya kupata hela nyingi hasa kwa abiria na mizigo na huko majini wakaguzi ni wale wale wanajuana tofauti na barabarani ambako kuna polisi na wengine wanaoweza kuzuia upakiaji wa mizigo na abiria kuzidi. Tatizo ni lile lile miaka na mika na hatujifunzi
 
Mv liemba ndio meli kongwe duniani na bado inafanya kazi ndani ya ziwa Tanganyika.
 
Mi mwenywe nmeshangaa hiyo idadi haifikii hata robo ya watu waliokufa kwenye MV BUKOBA
Mkuu ukisoma ile hukuma hakukuwa na manifesto inayoonesha watu wangapii walipanda meli ile esp katika madaraja ya walala hoi la pili na la tatu, manifesto ya daraja la kwanza lile la walalahai inaonesha kulikuwa na watu 196 na kati yao 32 na crew 4 ndo waliopatikana wakiwa hai na crew wengine 6 kupoteza maisha....

Hivyo iyo idadi ni daraja la Kwanza wale wa daraja la pili na tatu hawajulikani pengi hawakuwemo kwenye meli....haaa

Lakini ukienda ule mnara wa MV BUKOBA Bwiru mwanza kuna abilia 808 waliopotza maisha na miili yao kupatkana 116 ambao miili yao ilipatikana na 114 ambao walinusurikaa sasa jiulizee shida ilikuwa nini.....kama sio kuzidishaa uzitooo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HUKUMU KESI YA MV. BUKOBA NA MAFUNZO KWETU.

Na Bashir Yakub.
+255 784 482 959.

( A ).NAMBA YA KESI.

Kesi ya Jinai Na. 22/1998, Mahakama kuu Mwanza , Mbele ya Jaji Mlay.

( B ) WASHITAKIWA.

  1. Kapteni Jumanne Rume Mweiru. Huyu ndiye alikuwa Kapteni siku ya tukio, akiendesha toka Bukoba VIA kemondo Bay hadi Mwanza.
  2. Gilbert Mokiwa. Huyu alikuwa mkaguzi wa meli, na ndiye alikuwa na wajibu wa kuikagua MV Bukoba.
  3. Alphonce Sambo. Huyu alikuwa afisa bandari Bukoba, na wakati meli inaanza safari yeye na wenzake waliratibu safari.
  4. Prosper Rugumila.Huyu alikuwa afisa bandari kemondo ambapo MV Bukoba ilipitia ikitokea bandari ya Bukoba na kuongeza abiria na mizigo.
( C ) KOSA WALILOSHITAKIWA NALO.

Kuua bila kukusudia kinyume na kifungu cha 195 cha Kanuni za Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania.

( D ) MAELEZO YA KOSA.

Kuwa, tarehe 21 / 5 / 1996 majira ya saa 7 :30 asubuhi, eneo la ziwa Victoria Mwanza washitakiwa kwa uzembe walisababisha meli ya MV BUKOBA iliyokuwa ikitokea Bukoba kuelekea Mwanza kupinduka na kuzama ,na hivyo kusababisha vifo vya watu 159.

( E ) MASHAHIDI UPANDE WA MASHTAKA.

Upande wa mashitaka ulileta mashahidi 32 wakiwemo ;

  1. Kapteni Cleophas Magoge . Huyu saa 8 : 15 asubuhi,aliitoa MV VICTORIA bandarini Mwanza ilipokuwa inaendelea na matengenezo na kulazimika kuiendesha kuelekea kwenye eneo la ajali baada ya kuambiwa kuwa MV BUKOBA imezama.
Anasema alipofika eneo la tukio aliiona MV Bukoba ikiwa kichwa chini miguu juu, huku mizigo hasa ndizi,watu, na miili mingi ikielea majini. Na aliposogea karibu alimuona Kapteni wa MV Bukoba mshitakiwa wa kwanza akiwa ananing’inia juu ya meli iliyozama.

  1. Shahidi mwingine ni Kapteni Mannase Ephraim Kombo. Huyu anasema siku ya tukio alikuwa akiendesha MV BUTIAMA kutoka Port Bell Uganda kuelekea Mwanza. Anasema saa 6 :00 za asubuhi aliingia kwenye radio na kuwasiliana na bandari ya Mwanza kuwa atafika saa 9 : 00 asubuhi.
Anasema wakati akiwasiliana alisikia Kapteni wa MV Bukoba naye akiwasiliana kuwa atafika mwanza saa 8 :00 asubuhi. Anasema alifika bandari ya Mwanza saa 9:00am akashusha mizigo lakini MV Bukoba iliyosema kufika saa 8:00am haikuwa imefika.

Anasema, baadae alimsikia MPANGALA aliyekuwa muongoza meli siku hiyo akiiita MV Bukoba kwenye radio bila majibu. Anasema MPANGALA aliita sana mpaka akaamua kutoka nje kutizama, na kwa mbali saana aliona kitu ambacho hakukielewa. Alirudi ndani na kuchukua hadubini(binocular) kutizama tena, na hapohapo alimsikia akiongea kwa mshtuko kuwa MV Bukoba inazama.

Anasema maramoja aliamua kuiendesha MV BUTIAMA kuelekea eneo la tukio ambapo alikuta mitumbwi kadhaa ya wavuvi ikiokoa watu, na aliona maiti nyingi, watu hai, na mizigo vikielea.

  1. Shahidi mwingine ni meneja wa yard ya meli Mwanza. Anasema siku 29 kabla ya kuzama yaani april MV Bukoba ilikuwa na matatizo ya kuyumba ambayo pia yalithibitishwa na mashahidi wengine. Anasema, mtaalam kutoka Ubelgiji ambao ndio waliotengeneza meli hiyo aliletwa kuchunguza tatizo hilo na aliifanyia majaribio katika eneo liitwalo Karumo.
Mtaalam aligundua matatizo ya kuyumba na akasema watatoa ripoti mwezi wa 7 /1996, lakini meli ikazama mwezi 5/ 1996 miezi miwili kabla ripoti kutolewa.Anasema lakini baada ya majaribio hayo kuanzia tarehe 12 / 5 / 1996 meli ilifanya safari tatu, mbili Mwanza – Port bell Uganda , na moja Mwanza – Kisumu Kenya, na ya nne ndio ilikuwa ya mwisho ya Mwanza- Bukoba.

Anasema siku hiyo MV BUKOBA ilienda Bukoba lakini haikuwa imepangiwa kwenda huko, na badala yake MV VICTORIA ndiyo iliyokuwa imepangiwa kwenda Bukoba. Anasema MV Victoria ina uwezo wa kubeba abiria 1200, na tani za mizigo 250 wakati MV BUKOBA ina uwezo wa kubeba abiria 400, tani za mizigo 85.

Anasema kwahiyo tiketi za abiria na mizigo zilizoandaliwa huko Bukoba zilikuwa ni za MV Victoria kwasababu ndiyo ilitakiwa kwenda. Kutokana na hitilafu za injini ikashindwa kwenda na ikabidi ibadilishwe na MV BUKOBA na hivyo MV Bukoba ikafanya kazi ya MV Victoria.

  1. Munaf Hussein Ibrahim Punja ni abiria aliyenusurika katika hiyo ajali. Anatoa ushahidi kuwa alipanda meli saa 9:00 pm bandari ya Bukoba na watu walikuwa wengi pamoja na mizigo. Anasema meli ilikuwa inakwenda upande. Anasema walipofika Kemondo saa 10 ;00 usiku alishangaa kuwaona David pamoja na Mutayoba ambao aliwaacha bandari ya Bukoba na hawakuwa wamepanda meli.
Anasema aliwauliza kulikoni, wakamwambia kuwa kule Bukoba bandarini walizuiwa kuingia kwenye meli kwasababu ilijaa kwahiyo wakaamua kuchukua Taxi kuja kuisubiria Kemondo Bay. Anasema hapo Kemondo walipanda na wakasafiri wote.

  1. Zabron Kasindirano naye ni abiria aliyenuurika. Anasema meli ilipofika Kemondo Bay alimuona shemeji yake Francis Justusi Kaganji na kushangaa kwasababu walimuacha Bukoba. Anasema alimuuliza amefikaje Kemondo akamwambiwa alipanda taxi baada ya kuzuiwa kupanda bandari ya Bukoba.
Anasema saa 7 :00 asubuhi wakati wamekaribia kufika meli ilianza kuyumba sana. Anasema alikuwa amekaa na wanawake akawaambia wapande juu kuchukua “life Jacket” lakini wakamcheka kuwa ni mwanaume muoga na hivyo kwa hofu ya kutoonekana muoga naye hakuchukua tena Jacket.Anasema haikupita dakika 10 tokea aambiwe muoga meli ikapinduka, akatupwa kwenye maji karibia na mkungu wa ndizi ambao aliushikilia mpaka akaokolewa, na kuwa wale wanawake hakuwaona tena.

Mashahidi walikuwa wengi ila kwa kutaja ni wachache.

( F ) ILI WATUHUMIWA WAPATIKANE NA HATIA YALITAKIWA KUTHIBITISHWA MAMBO YAFUATAYO.

  1. Kwamba meli ilikuwa na matatizo ya kiufundi(ya kuyumba) na wao hawakuyashughulikia/kuyajali au kuzingatia matatizo hayo.
  2. Pili, waliijaza meli watu kuzidi uwezo wake.
  3. Tatu, waliijaza meli mizigo kuzidi uwezo wake.
MATATIZO YA KIUFUNDI.

Hii ilishindwa kuthibitika kwasababu kwanza hakukuwa na rekodi yoyote ya mafundi na wataalum akiwemo yule Mbelgiji, iliyozuia meli kuendelea kufanya kazi. Hakukuwa na shaka kuwa meli ilikuwa na matatizo ya kuyumba ila haikuzuiwa kufanya kazi.

Pili, hakukuwa na ushahidi wa kisayansi ulioonesha kuwa matatizo ya kuyumba ndiyo yaliyopelekea meli kuzama.

KUJAZA WATU KULIKO UWEZO.

Hii nayo ilishindwa kuthibitika kwasababu hakukuwa na rekodi sahihi ya watu waliongia kwenye meli. Baadhi ya vitabu vinaonesha 400, vingine 700, vingine 759 nk.

Pia idadi ya watu ilioneshwa kwa kuangalia tiketi zilizouzwa. Hakukuwa na ushahidi wa kuonesha waliongia ndani ya meli yaani waliosafiri walikuwa wangapi. Mashahidi nao wanathibitisha kuwa kununua tiketi sio kusafiri, unaweza kununua tiketi halafu usisafiri. Kwahiyo ni vigumu kupata idadi ya waliosafiri kwa kuhesabu tiketi zilizouzwa.

Kitabu cha uhakiki wa wasafiri ambacho hutumiwa na wakaguzi ndani meli inapokuwa safarini ndicho kinaweza kuthibitisha waliosafiri yaani waliokuwa ndani ya meli, na hivyo kujua kama ilizidisha au hapana. Hata hivyo kitabu hicho nacho kilizama, na hivyo kukosa ushahidi wa kujua mpaka meli inazama ilibeba abiria wangapi, na hivyo kuweza kutambua kama walikuwa wamezidi ama hapana.Hii nayo ikafia hapo.

KUJAZA MIZIGO KUPITA UWEZO.

Hii nayo haikuweza kuthibitishwa. Hakuna rekodi Bukoba bandari kuwa zilipakiwa tani ngapi ,na hakuna rekodi Kemondo Bay ziliongezwa tani ngapi. Unawezaje kusema ilizidisha mizigo kwa ushahidi wa macho tu bila rekodi sahihi ya mizigo.Hii nayo ikafa.

( G ) HUKUMU.

Kama hakuna ushahidi kuwa ubovu wa meli ndio uliosababisha izame, kama hakuna ushahidi kuwa meli ilipakia abiria wengi kuliko uwezo wake, kama hakuna ushahidi kuwa meli ilipakia mizigo kuliko uwezo wake, nini kilichobakia zaidi ya kuwaachilia huru washitakiwa wote wanne.

Mahakama ikaona washitakiwa wote wanne hawana hatia , ikaamuru waachiliwe huru mara moja.

( H ) TUNAJIFUNZA NINI.

Ajali zote za majini, kuanzia hii ya MV Bukoba, Spice Islanders Zanzibar, mpaka sasa Mv nyerere, nk, hadithi ni moja tu, kuzidisha abiria na mizigo. Pamoja na hayo katika ajali zote hizi, hakuna mtu unayeweza kumsimamisha akwambie idadi halisi kabisa,ile yenyewe ya watu waliokuwemo na akakwambia. Huu ni ukweli. Hayupo, na narudia hayupo. Si mkata tiketi, si mkaguzi anayesafiri na meli, si kapteni, si ofisa wa bandari, hakuna. Ndio maana utaona inatajwa idadi ya waliokufa leo, kesho wanasema mwili mwingine umegunduliwa na hivyo waliokufa idadi imeongezeka na kufikia kadhaa.

Hakuna mtu wa kukwambia waliosafiri ni 100, walionusurika ni 50, tuna maiti 30, na hivyo sasa hivi tunafuta maiti 20 TU tufunge zoezi. Hakuna wa kutoa takwimu kama hii. Ajali zikitokea tunakaa mwaroni tunasuburi chochote ambacho kitatemwa na ziwa ndicho tunachobeba na kuongeza kwenye idadi. Ziwa lisipotema tunasema basi wameisha. Hatuwezi kusema kwenye idadi yetu anakosa maiti mmoja na ndiye tunamtafuta kwasasa, katu hatuwezi. Kweli dunia hii ya karne ya 21 hatuwezi hata kujihesabu hata kwa kutumia vidole na vijiti ?, Kweli. ?.

Mbona huku kwenye usafiri wa anga idadi iko wazi na inajulikana. Utaambiwa abiria waliosafiri,na sio waliokata tiketi, bali waliosafiri ni 257, watumishi wa ndege(crew) ni 10, na hivyo waliokuwemo jumla ni 267. Na inakuwa hivyohivyo kweli hakuna kubabaisha. Kwanini haiwi hivyo kwenye meli/vivuko. Leo ni miaka 22 tangu MV Bukoba izame, nakuhakikishia hakuna wa kukwambia idadi halisi ya waliofariki katika ajali hiyo, hayupo. Leo ni miaka 7 tangu MV Spice Islanders izame, nakuhakikishia hakuna wa kukwambia idadi halisi ya waliofariki katika ajali hiyo, hayupo. Na leo nasema hakuna wa kukwambia idadi halisi kabisa ya waliofariki kwenye kivuko cha MV Nerere, hayupo. Na huu ndio ukweli. Kadhalika katika meli zote hizo hakuna wa kukupa idadi ya tani halisi ya mizigo iliyokuwemo bila kubabaisha, hakuna.

Sasa unaweza kujiuliza tunakabiliwa na tatizo gani hasa, hatujui hesabu hizihizi za kuhesabu 1-10 na.....,ni wazembe, ni wasiojali,ni wapuuzi, ni watu ambao bado tunaishi maisha ya ujima,ni watu wa aina gani hasa. Watu ambao ulaya, America na uchina wameanza kugawana maeneo mwezini ili wachimbe madini ya PLAGIOCLASE sisi hatuwezi hata kuhesabiana kwa hesabu ya darasa la kwanza.Tuseme nini hiki kama sio janga. Na hakuna shaka kushindwa kuhesabiana ndiyo sababu ya ajali za majini . Hatuna ajali ya majini ambayo idadi ya watu ilikuwa sawa(capacity). Zote idadi ilizidi.

Tizama pale feli kigamboni. Vinafanya kazi vivuko vitatu kwa kupishana na wote tiketi mnachukua sehemu moja. Kama kinazama kivuko kimoja pale(mungu aepushie mbali) nani anaweza kusema idadi ya waliokuwemo. Kwasababu hata tukisema tuhesabu tiketi bado hutopata jibu kwakuwa tiketi za kupanda kivuko chochote kati ya vitatu zinakatwa sehemu mmoja, hivyo huwezi kujua aliyekata tiketi amepanda kivuko kipi kati ya vitatu.

Lakini tizama watu wanavyoingia kwenye kivuko. Geti likifunguliwa mpaka mtu mwenyewe aseme kimejaa sana siingii, vinginevyo watu wote mlioko kwenye banda la kusubiria mtaingia. Kivuko hiki kinabeba watu wangapi kwani. Kikija kidogo wanaingia haohao, kikija kikubwa wanaingia haohao, Looh.Mwanzoni nilifikiri kwakuwa safari ya feli - kigamboni ni ya karibu sana basi sio rahisi kutokea janga, lakini MV Nyerere imenifunza mengi.

Hoja ni kwamba, kama huwezi kujua na ukawa na idadi halisi ya waliosafiri maana yake huwezi kudhibiti upakiaji unaozidi uwezo wa chombo. Kwanini, kwasababu unajua chombo kinahitaji kupakia wangapi, lakini hujui wanaoingia huwa ni wangapi.Na hapa ndipo yalipo majanga.

Sasa tubadilike, yatoshe tuliyofunzwa na ulimwengu. Tunahitaji mifumo mizuri ya kuratibu upakiaji wa abiria na mizigo katika vyombo vya majini. Uratibu unaanza na nani anawajibika na nini, vifaa vya kutambua watu wanaoingia kusafiri, na sio mashine za kukatia tiketi tu, usimamizi wa kiwango cha juu kwenye vituo vya meli na vivuko, kuondoa rushwa meneo hayo,mfumo wa uongozi katika bandari na meli unaoanisha kwa uwazi wajibu wa kila mfanyakazi. Isiwe kama ya MV Bukoba kapteni anasema, ni chief officer, chief officer anasema ni 1st officer, 1st officer anasema ni marine surveyor, marine surveyor anasema port officer, yaani unakosa hata awajibike nani katika nini mpaka mwisho watu wote wanaachiwa huru. Mfumo mzuri wa nani anawajibikia nini.

Watu wa marine wachukue semina ya usimamizi wa abiria na mizigo kwenye viwanja vya ndege. Hakuna dhambi umakini uleule unaotumika kwa abiria na mizigo kwenye viwanja vya ndege ukatumika maeneo ya bandarini kwasababu pote zinabebwa roho za watu. Kwanini huku ionekana tahadhari kubwa ya abiria na mizigo wakati huku hakuna, na wanaobebwa wote ni watu. Tusipofanya hivyo tukaendelea na uenyeji enyeji wetu huu, tujiwekee guarantee ya kupokea misiba ya majini kila baada ya kipindi fulani.

Narudia tena tatizo lipo kwenye upakiaji, soma ripoti zote za ajali za meli ni abiria na mizigo kuzidi. Hapa ndipo tunatakiwa kushughulika napo. Yanitoshe haya kwa leo.
Critical analysis
 
( G ) HUKUMU.

Kama hakuna ushahidi kuwa ubovu wa meli ndio uliosababisha izame, kama hakuna ushahidi kuwa meli ilipakia abiria wengi kuliko uwezo wake, kama hakuna ushahidi kuwa meli ilipakia mizigo kuliko uwezo wake, nini kilichobakia zaidi ya kuwaachilia huru washitakiwa wote wanne.

Mahakama ikaona washitakiwa wote wanne hawana hatia , ikaamuru waachiliwe huru mara moja.
Aiseee sio mchezo kweli kulikuwa na mkono wa MTU kama Sumaye alivyosema ,USA ndio iliyotoa taarifa ya Meli kuzama....Kuna Gaidi wa Al qaeda alizama kwenye MV Bukoba.
 
Back
Top Bottom