Hivi kwa sasa CHADEMA inawezaje kudai Mungu yuko upande wao wakati imethibitika kutoka kwenye maelezo ya Naibu katibu mkuu wake kwamba ni chama cha kishirikina?
Aisee,watu wengine bwana hata hatuwaelewi,eti cdm ni chama cha washirikina.Chama kipi hakhna ushirikina? Haujui kuwa watu wanasaka urais mpaka Nigeria kupitia chama cha mafisadi,majangiri na wezi?
Mkuu mimi sina hofu hata kidogo, ninachokiamini kutoka moyoni kabisa ni kwamba Kamanda wetu HAWEZI KUSHINDAile kesi ya kesho kwa sababu:-
1. Rais Jakaya Kikwete ana mkono katika LEMA KUVULIWA ubunge na ndiyo maana aliyasema yale aliyoyasema wakati anafungua mkutano fulani Arusha wakati huo lema akiwa kwenye M4C Mtwara au Lindi.
2.Kikwete anaamini kuwa CHADEMA kuongoza jimbo la Arusha, ilihali ni mji wa Kitalii, siyo halali.
3. ...........................
4. .............................
5. ..............................
Zipo sababu nyingi lakini hakuna hata moja nyenye mashiko. Ni ujinga na Ubabe wa kipumbavu tu. Ninachokiamini na ambacho kinanipa matumaini ni kuwa, hata tukirudia uchaguzi arusha bila kampeni na CHADEMA tukasimamisha mtu yoyote yule, tutashinda. Na hata kwa upande mwingine, mimi sikuupenda uamuzi wa CHADEMA kukata rufaa mahakama ya rufani ilihali walifahamu kuwa kesi ile iliingiliwa na RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE.
Rejea yale ambayo LEMA aliyapublish baada ya Kikwete kuongea yale ARUSHA kwenye ufunguzi wa mkutano. Muda huu tungelishakuwa na mbunge ARUSHA na kama wote tunavyofahamu, Lema anakubalika sehemu kubwa katika nchi hii, angeliweza kufanya kazi za ndani za chama ambazo ndizo zina faida kubwa kwa chama kwa ajili ya Mwaka 2015!!!
Ni mtazamo tu!!!!!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.