Huku tozo kibao wakiwekewa wananchi. Wakazi wa Liwale wanunua ndoo ya maji sh 1000/-

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Hizi tozo zinatusaidia nini sasa?

Tunakamuliwa na bado hata maji hatupati

---
Liwale.jpeg

Mamlaka ya Maji safi na mazingira Wilaya ya Liwale, Mkoani Lindi (LIWASA) imeombwa kuzalisha kwa wingi huduma ya maji kwa lengo la kuwatatulia wananchi kero za upatikanaji wa huduma hiyo kwa jamii.

Ombi hilo limetolewa na baadhi ya wakazi wa mji wa Liwale walipokuwa wakizungumza na mwandishi wa East Africa TV alipotembelea wilaya hiyo na kudai kukabiliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu na kwamba wanalazimika kutumia maji yaliyotuwama kwenye mito.

Zaidi ya mwezi sasa hatupati huduma hii ya maji safi na salama kwa matumizi ya binaadamu” Walieleza wakazi hao.

Wakazi hao wameongeza kuwa kwa sasa hulazimika kununua dumu moja lenye ujazo wa Lita 20 kwa bei ya Sh. 1,000 hadi Sh. 1,500. Wameiomba Mamlaka ya Maji safi, salama na mazingira Liwale (LIWASA) kuzalisha rasilimali hiyo kwa wingi ili wananchi waweze kunufaika na huduma hiyo mhimu.

Changamoto ya upatikanaji wa maji ndani ya mji wetu ipo tena ni kubwa, kwani tunakaa wiki mbili hadi nne bila kupata maji, badala yake tunakunywa yaliyotuama mitoni”Alieleza Ridhiwani, Mkazi wa wilaya hiyo

Chanzo: EastAfrica TV
 
Waliipenda wenyewe..mpka ujinga uwatoke akilini wajue adui wao wajwanza ni ccm..

#MaendeleoHayanaChama
 
Hizi tozo zinatusaidia nini sasa?

Tunakamuliwa na bado hata maji hatupatiView attachment 2345666
Habari kama hizi ni ushahidi mwingine kwamba tozo ni muhimu sana kiasi kwamba hatuwezi kubaki kubembeleza watu wa Mjini ambao wamekuwa makupe wa kuwanyonya watu wa Vijijini Kwa zaidi ya miaka 60 sasa..

Huu ni ushahidi mwingine ambao Mwigulu anatakiwa kuutumia anapojenga hoja maana moja ya Kazi za tozo ni kupeleka Maji Vijijini..

Na target ni kwamba by 2025 watu wa Vijijini wapate maji safi na salama kwa 85% na umbali usiozidi km 1..

Tozo haziwezi kuwawikia wote mwaka mmja lakini ndio maana ya kuwa na target..
 
Huna akili
 
Siku moja Mwigulu atakufukuza hapo kwake ukajitegemee, hapo ndio akili zitakurudia
 
Back
Top Bottom