HUKO DRC NI VlTA KATI YA TANZANIA NA RWANDA(PROX WAR)

HUKO DRC NI VlTA KATI YA TANZANIA NA RWANDA(PROX WAR)

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,663
Reaction score
167,602
[h=3]HUKO DRC NI VITA KATI YA TANZANIA NA RWANDA(PROX WAR)[/h]





PROX WAR au Proxy Warfare ni vita inayopiganwa kwa kupitia sehemu nyingine. Katika vita 'ya kawaida' mapigano huwa kati ya nchi na nchi.Kwa mfano, Vita ya Kagera ilkuwa kati ya Tanzania na Uganda, na mapambano yalitokea katika nch zote mbili.


Katika proxy war hali ni tofauti. Nchi A inaweza kupigana vita na nchi B katika nchi C.Yaani kwa ufasaha zaidi, kwa mfano, kuna mapambano katika nchi C kati ya jeshi la nchi hiyo na waasi, kisha nchi A inapeleka askari wake kuilisaidia jeshi la serikali la nchi C, na nchi B inapeleka askari wake (au inasaidia kwa siri) kusaidia waasi wanaopigana na serikali ya nchi C.


Naomba ieleweke kuwa mie sio nabii wa waangamizi, kwa kimombo 'prophet of doom.' Ninachoongelea hapa kinatokana tu na hali halisi ilivyo kwenye mapigano yanayoendelea nchi DRC kati ya jeshi la Serikali ya nchi hiyo na kikundi cha waasi cha M23.


Nchi yetu imetoa wanajeshi kadhaa kushirikiana na Malawi na Afrika Kusini kuunda kikosi cha kulinda amani nchini DRC. Lakini kuna taarifa kuwa waasi wa M23 wanapewa sapoti na Rwanda (kama ni kweli au la,mie sina hakika...lakini lisemwalo lipo...kwanini Rwanda ituhumiwe na si Kenya au Msumbiji?)


Sasa tukiangalia hali ya uhusinao kati ya Tanzania na Rwanda katika siku za hivi karibuni, na tukijikumbusha kauli ya Rais Paul Kagame kuwa "atamsbiri (Rais Jakaya) Kikwete mahala mwafaka kisha amtandike" kuna uwezekano "mahala hapo mwafaka" kuwa ni DRC.


Kwanini ninasema hivyo? Uwezekano wa Rwanda kuivamia Tanzania au Tanzania kuivamia Rwanda ni mdogo sana,kutokana na sababu mbalimbali. Lakini nchi hizo mbili zinaweza 'kupigana vita kirahisi' kupitia mapigano yanayoendelea kati ya Jeshi la DRC linalosaidiwa na 'Kikosi cha Kimataifa' (kinachojumuisha Jeshi la Tanzania) na waasi wa M23 (wanaodaiwa kusaidiwa na Rwanda.)


Vyovyote itakavyokuwa, vita ni kitu kibaya, natunapaswa kuombea kistokee kwa gharama yoyote ile.Mwanafalsafa mahiri wa 'Sanaa ya Vita' (Art of War), Mchina SUN TZU anatahadharisha kuwa "vita ni suala la uhai na kifo, barabara inayoelekea kwenye usalama au maangamizi..."


Kuna wanaojidanganya kuwa Rwanda "ni kijinchi kidogo kisicho na uwezo wa kupambana na Tanzania." I wish wangekuwa sahihi.Kwa mujibu wa SUN TZU,ushindi katika vita yoyote ile unategemea sana matumizi ya mashushushu (wapelelezi) wa ndani na wa nje.


Hivi tunafahamu kuwa tuna Wanyarwanda wangapi Tanzania ambao wapo mahsusi katika kufanikisha azma yoyote ile ya nchi yao?Kwa maafisa wetu uhamiaji ambao bia mbili tatu tu wapo tayari kumpa mtu passport ya Kitanzania, tuna maadui wangapi wanaotengeneza idadi yetu kukaribia milioni 50?




Soma hapa Sun Tzu's Art of War - Chapter 13: The Use of Spies kufahamu zaidi kuhusu matumizi ya mashushushu katika vita, kwa mujibu wa SUN TZU.(na jaribu kupigia mstari uhusiano wetu wa Malawi na uwezekano wao kuwa mojawapo ya aina hizo za mashushushu)


Anyway, kama nilivyobainisha hapo awali, mie sio nabii wa majanga.Ningependa sana askari wetu waliokwenda huko DRC watimize jukumu lao haraka na kurejea nyumbani wakiwa salama WOTE. Nilichoeleza kuhusu PROXY WAR ni uchambuzi tu unaozingatia hali halisi.




 
acha kupotosha wanaopigana ni jeshi la serikali ya congo na waasi. majeshi ya kigeni yapo kulinda aman asa kwa kulinda raia
 
kuna maafisa wengi wa usalama kutoka rwanda nafikiri ndio kinampa kiburi kagame lakini hajui kuwa akijaribu vita ndio kiama chake labda atumie mbinu ya kupandikiza uongozi
 
Kuhusu mashushu its very true,,hata sisi kuna wa tz kibao huko rwanda,,na pia vita ya sasa ni kati ya fdrc na m23,,,brigade ya sadc bado haijakamilika mpaka baada ya wiki 2,,
 
Shushu wa Rwanda kuipeleleza Tanzania ili kuiangamiza ni sawa na Shushu wa Tanzania kwenda kuipeleleza Israel kwa lengo la kuipiga. Ili ushinde vita kuna factors nyingi zaidi ya ushushu wa kung'amua adui ana nini. Je, ukikuta ana ndege ya aina ya 'drone' utaweza kuinunua????
 
I am impressed with your analysis, as you have declared your player for the proxy war not to uprise.I even criticize our involvement in external affairs while we have our internal weakness which needs effective concentration.The big powers are volunteers in Congo social unrest, we just play the song without understanding the tune!
 
unaandika kama umelala mbona unapotosha sana.
 
Huu ni uchambuzi mzuri sana mkuu sasa unapoanza kujitetea unaharibu maana yote!
 
Majeshi ya kigeni yanalinda amani hawapo kivita kule... Vita ni kati ya m23 na serikali ya kongo..
 
Nimevutiwa sana na posti za wengi wenu, lkn nimemuona mkuu Bujibuji kuwa na thinking mind nzuri, ameona uwezekano wa Wanyarwanda kujipenyeza, lakni pia kutafuta aliyoiita SUN TZU kuwa njia ya kupelea maangamizi Tanzania, hapa lazima tuwe makini njia za maangamizi ni nyingi sana. Kwa kifupi kila dola katika dunia inapenda itambulike, Rwanda inajua ni kwa njia ipi dunia itaitambua, Alexander Wendt anamsemo wake, "anarchy is what state make of it", mtu mwelewa aTarefer matuKio meengi duniani kivita nk, world war. hata great lake Crisis ya miongo michache. Si ajabu hata museven akajiunga na rwanda, Kimsingi ni kwamba rwanda hata kama kwa siri anaisiadia m23, mjue hayuko peke ake.
 
I am impressed with your analysis, as you have declared your player for the proxy war not to uprise.I even criticize our involvement in external affairs while we have our internal weakness which needs effective concentration.The big powers are volunteers in Congo social unrest, we just play the song without understanding the tune!

MAKALA umenena, tunatabia ya kujifanya tunajali sana. charity begin at home nadhani ndivyo, tuna matatizo mengi sana ndani, nadhani tulipaswa kuieleza UN kuwapo na shida zetu,

Lakini mkuu Makala Jr kumbuka hawa jamaa hawatumii fedha zetu, sana sana kisiasa serikali itasema imekusudia mambo hata
  1. kuwapa exposure askar wetu, amabo wanakaa muda mrefu bila majaribio
  2. kusaidia jumuia za kimataifa na ndio maana tulipekea askari, lebanon, darful, algeria, comoro, na sasa DRC
  3. AJIRA hii inawawezesha wakirejea wanakuwa sio wa kawaida, malipo kule ni international teams, wengi wanaukata kimaisha
  4. ingawa viapo vya jeshi vinaeleweka kufa na kupona


vita mbaya ni ile inayohusicha battle field yenu, na gharama zenu, pale DRC IKUMBUKWE KUWA ILE SI VITA NI
kuleta amani
 
naamini jeshi letu liko makini kama wew common individual umeweza kuyajua hayo sijui kama ni expert au ni msaada wa wikipedia naamini maafisa wetu wanajua zaid kuhusu hiyo porxy war
ndio kuna ideology ya kuto mdarau mshindani wako hata kama ni mdogo bado nna imani na jeshi letu
 
JAMAA alichosema vingine ni vya Kweli tunatakiwa tuamke sasla sivyo, Rwanda watatusumbua, kagame anatoa kauli chafu na za vitisho, wanyarwanda wamejaahuku kwetu, hapa ninapoishi sinza waPo wengi tu,, pamoja na wamalawi, sijui uhamiaji wanafanya nini.
 
Mungu aepushie mbali, manake hayo yanaweza kuwa majanga yakaturudisha nyuma zile enzi za mwalimu za kufunga mkanda kwa miezi kumi na nane wakati maisha yenyewe kwa sasa ni kama tumefunga mikanda.
 
Umbumbumbu na upotoshaji usio na msingi unapelekea chuki zisizo maana!
 
acha kupotosha wanaopigana ni jeshi la serikali ya congo na waasi. majeshi ya kigeni yapo kulinda aman asa kwa kulinda raia

Soma alichokiandika tena usipoelewa rudia tena kusoma usipoelewa baada ya kurudia mara tatu, jipe muda wa siku mbili then rudia tena kusoma usipoelewa mwulize yeyote akufafanulie jamaa alichokiandika .....KISS
 
Majeshi ya kigeni yanalinda amani hawapo kivita kule... Vita ni kati ya m23 na serikali ya kongo..
hivi majeshi ya kongo yenyewe hayawezi kulinda amani yao?
 
Alichosema Bujibuji ni kweli kabisa. Vita tunayopigana na waasi, na kwa kuwa tumepewa mandate ya kujibu mapigo askari wetu wanaposhambuliwa na m23 (tofauti na Darfur), ni wazi kwamba tunapigana na Rwanda. Ukali wa Kagame dhidi ya Kikwete unatia shaka. Nadhani matusi na kejeli anavyotoa ni kama jipu limepata pa kutokea. Hasira hizi nyuma yake inawezekana ni za Tanzania kupeleka majeshi DRC ili kupambana na majeshi yake yanayopora madini na rasilimali nyingine huko. Vyovyote iwavyo, vita hii ni muhimu Tanzania kushiriki. Ikitokea fursa, sitasita kuwaunga mkono wapiganaji na makamanda wetu!
 
Back
Top Bottom