HUKO DRC NI VlTA KATI YA TANZANIA NA RWANDA(PROX WAR)

HUKO DRC NI VlTA KATI YA TANZANIA NA RWANDA(PROX WAR)

bastola.JPGMkuu Bujibuji unapaswa kuanza kufanya maandalizi ya aina hii!
 
Mtoto acha kupiga mayowe. Acha waje waone wenyewe!.
 
Majeshi ya kigeni yanalinda amani hawapo kivita kule... Vita ni kati ya m23 na serikali ya kongo..

Hata darfur tunalinda amani. km hujui heri kupigana kuliko kulinda amani sehemu ambayo upande wa pili una bifu.na yawezekana chuki ya kagame ni sisi kuwepo drc.chezea maslahi ya mtu wewe?
 
acha kupotosha wanaopigana ni jeshi la serikali ya congo na waasi. majeshi ya kigeni yapo kulinda aman asa kwa kulinda raia

kwa taarifa yako, tofauti na vikosi vingine vya UN askari wa UN waliopo KONGO wanaruhusiwa kupigana wanapohisi wapo hatarini.
 
HUKO DRC NI VITA KATI YA TANZANIA NA RWANDA(PROX WAR)







PROX WAR au Proxy Warfare ni vita inayopiganwa kwa kupitia sehemu nyingine. Katika vita 'ya kawaida' mapigano huwa kati ya nchi na nchi.Kwa mfano, Vita ya Kagera ilkuwa kati ya Tanzania na Uganda, na mapambano yalitokea katika nch zote mbili.


Katika proxy war hali ni tofauti. Nchi A inaweza kupigana vita na nchi B katika nchi C.Yaani kwa ufasaha zaidi, kwa mfano, kuna mapambano katika nchi C kati ya jeshi la nchi hiyo na waasi, kisha nchi A inapeleka askari wake kuilisaidia jeshi la serikali la nchi C, na nchi B inapeleka askari wake (au inasaidia kwa siri) kusaidia waasi wanaopigana na serikali ya nchi C.


Naomba ieleweke kuwa mie sio nabii wa waangamizi, kwa kimombo 'prophet of doom.' Ninachoongelea hapa kinatokana tu na hali halisi ilivyo kwenye mapigano yanayoendelea nchi DRC kati ya jeshi la Serikali ya nchi hiyo na kikundi cha waasi cha M23.


Nchi yetu imetoa wanajeshi kadhaa kushirikiana na Malawi na Afrika Kusini kuunda kikosi cha kulinda amani nchini DRC. Lakini kuna taarifa kuwa waasi wa M23 wanapewa sapoti na Rwanda (kama ni kweli au la,mie sina hakika...lakini lisemwalo lipo...kwanini Rwanda ituhumiwe na si Kenya au Msumbiji?)


Sasa tukiangalia hali ya uhusinao kati ya Tanzania na Rwanda katika siku za hivi karibuni, na tukijikumbusha kauli ya Rais Paul Kagame kuwa "atamsbiri (Rais Jakaya) Kikwete mahala mwafaka kisha amtandike" kuna uwezekano "mahala hapo mwafaka" kuwa ni DRC.


Kwanini ninasema hivyo? Uwezekano wa Rwanda kuivamia Tanzania au Tanzania kuivamia Rwanda ni mdogo sana,kutokana na sababu mbalimbali. Lakini nchi hizo mbili zinaweza 'kupigana vita kirahisi' kupitia mapigano yanayoendelea kati ya Jeshi la DRC linalosaidiwa na 'Kikosi cha Kimataifa' (kinachojumuisha Jeshi la Tanzania) na waasi wa M23 (wanaodaiwa kusaidiwa na Rwanda.)


Vyovyote itakavyokuwa, vita ni kitu kibaya, natunapaswa kuombea kistokee kwa gharama yoyote ile.Mwanafalsafa mahiri wa 'Sanaa ya Vita' (Art of War), Mchina SUN TZU anatahadharisha kuwa "vita ni suala la uhai na kifo, barabara inayoelekea kwenye usalama au maangamizi..."


Kuna wanaojidanganya kuwa Rwanda "ni kijinchi kidogo kisicho na uwezo wa kupambana na Tanzania." I wish wangekuwa sahihi.Kwa mujibu wa SUN TZU,ushindi katika vita yoyote ile unategemea sana matumizi ya mashushushu (wapelelezi) wa ndani na wa nje.


Hivi tunafahamu kuwa tuna Wanyarwanda wangapi Tanzania ambao wapo mahsusi katika kufanikisha azma yoyote ile ya nchi yao?Kwa maafisa wetu uhamiaji ambao bia mbili tatu tu wapo tayari kumpa mtu passport ya Kitanzania, tuna maadui wangapi wanaotengeneza idadi yetu kukaribia milioni 50?




Soma hapa Sun Tzu's Art of War - Chapter 13: The Use of Spies kufahamu zaidi kuhusu matumizi ya mashushushu katika vita, kwa mujibu wa SUN TZU.(na jaribu kupigia mstari uhusiano wetu wa Malawi na uwezekano wao kuwa mojawapo ya aina hizo za mashushushu)


Anyway, kama nilivyobainisha hapo awali, mie sio nabii wa majanga.Ningependa sana askari wetu waliokwenda huko DRC watimize jukumu lao haraka na kurejea nyumbani wakiwa salama WOTE. Nilichoeleza kuhusu PROXY WAR ni uchambuzi tu unaozingatia hali halisi.



Mkuu, ingependeza kama ungenitendea haki kwa kuweka chanzo cha bandiko hili, yaani blog post hii D.R.C kuwa uwanja wa 'VITA WAKALA' (Proxy War) Kati ya Tanzania na Rwanda? ~ Kulikoni Ughaibuni
 
Acha tanzania tutolewe manundu maana tumeZidi kiherehere
 
Watanzania DRC haielekei kama wameshaanza kupigana. Vita imeanza juzi,baada ya kusita kwa miezi tisa.
 
Back
Top Bottom