Hujuma stendi ya Mabasi ya Nyegezi ( Mwanza)

Hujuma stendi ya Mabasi ya Nyegezi ( Mwanza)

mzalendo moyoni

New Member
Joined
May 2, 2012
Posts
1
Reaction score
0
Serikali imewekeza Fedha nyingi saana ambazo ni kodi zetu sisi walala hoi kwenye ujenzi wa Stand hii ya Nyegezi lakini leo nimesikitika kukuta chooni hakuna maji na ni kwazaidi ya miezi Sita(6).

Mkandarasi anayetoa huduma amejibu kwa wepesi tuu kwamba amewapigia simu watu wa mamlaka na akatulia. Maana yake kwake yeye sio tatizo kukosekana maji kwenye eneo analotoa huduma.

Kupitia mahujiano nae, imebainika kwamba anakwepa kulipa maji kwa mamlaka( kununua huduma ya Maji kutoka kwa Mamlaka ya Maji Mwanza) kwakuwa ameshindwa kufanya udhibiti wa maji na kufanya gharama anazoingia kulipia maji kwa mamlaka kuwa kubwa hivyo kachagua njia mbadala ya kuweka pipa nje.

Athari za pipa ni kubwa mnoo hasa kwenye maambukizi ya maradhi kwa watumiajo wa choo kile ijapokuwa anapokea pesa kwa huduma.

Maswala madogo madogo kama haya (Housekeeping) kama yanakuwa hayana tija lakini yana athari kubwa ni muhimu waliopewa dhamana kwenye maeneo hayo kuyashughulikia otherwise kila siku kodi zetu zitakuwa zinatumika kufanya kazi ambaoz tayari zimefanywa ila waliopewa dhamana wanashindwa kuyasimamia.
 
Mbona nimepita hapo jana na nmeingia kwenye vyoo maji yapo na siyo jana tuu mi ni mtumiaji wa mara kwa mara wa hiyo stendi ,wewe unataka kusema kero hiyo miezi sita isisemwe popote na yeyote miezi yote ,watakaokuamini watakuwa viazi
 
Kama Airport ya kimataifa ya JNIA haina maji vyooni sembuse stand ya nyegezi??!
 
Back
Top Bottom