Hujaijua vizuri Afrika!

Waache watumbue, ni muda wao.
Hata wewe ukipata nafasi utatumbua na kufuja mali kwa kwenda mbele
Haya ndiyo mawazo ya baadhi ya Waafrika... Wakitoka hapo wanawalaumu makaburu...
 
Ni mu-Afrika pekee katika binadamu wote aliyejaa ubinafsi na ujinga usio na kifani.
Ukiiba leo Africa dola bilioni na kuziingiza kwenye nchi za mabeberu, hawakuulizi kitu. Wanajua peso hizo zitakuza chumi zao. Sasa, jaribu kuzitoa hapo ndio utaona mziki wake na matokeo yake ndio hayo. Utatafutiwa kesi ya kubambikizwa ili baadae wataifishe pesa hizo na mara zote mijizi hii ya Africa huambulia patupu.
 
Kama mababu walithubutu kumuuza mtoto wao kwa mzungu/ mwarabu kwa vipande vya Shanga nguo nk, unatarajia nini kwa sisi watoto wao? Waafrika wengi wameshindwa kuutengeneza utajiri kwa akili yao badala yake wanatumia cheti cha mzungu,rushwa,bunduki,uchawi na fitna.
Mi nashangaa wanaodhani ccm itatoka madarakani kwa kura.Hizo raha zote za bure wawaachie wapinzani, ukweli ni kwamba waliopo madarakani wanajipatia pesa za bila jasho.Nchi wameifanya Mali yao, wanaamua wanavyotaka na hakuna wa kuwazuia kwa sababu wanamiliki vyombo vya siraha. UK's fungus mdomo unafyekelewa mbali.
 
mwalimu wangu wa historia aliwahi kutuuliza " hizi habari na taarifa zinazoenea worldwide ni kwasababu ziliandikwa na vyombo vya habari vya huko kwa wenzetu, tuna uhakika gani hua ni za kweli ama ni propaganda tu?, akatupa mfano kwa kutuuliza kuhusu idd amin, baadae akatuambia kua waganda walikua wanamkubali sana idd amin ila alikua labelled kama dikteta na blah blah zingine,"..

mantiki yake kubwa ilikua ni ukitaka uhalisia wa historia uliza wakongwe angalau utapata uhalisia.. sasa mpaka hapo sina cha kuchangia kuhusu mada yako maaana na doubt information za hao marasis wote uliowataja mkuu.
 
Umasikini wa africa, vita na ugaidi ni vielelezo tosha kwamba hayo ni ya kweli na yanatokea.
 
Makala safi sana hii mkuu. Hongera brother. Ukipata muda pia unaweza ukapitia makala yangu hapo chini ambayo nayo pia inahoji mustakabali ya bara hili pendwa la Afrika.

Je, wanaharakati wa kisiasa barani Afrika wanapigania kwa dhati mabadiliko ya kidemokrasia au maslahi yao binafsi?

Sasa ni miaka 60 baada ya Uhuru wa Bara letu. What kind of future do African politicians hold for their fellow countrymen in the next 60 years (2080)?
 
Mimi nadhani hii hali inatokea kwa sbb ya rushwa au mali na matendo maovu walofanya unakuta wanawaza wakimaliza mud itakuwaje. Ila akiwa na hela hatetereki pesa ni kila kitu hata mlima unaweza hamishwa
 
Unaweza kubadirisha kila kitu bila kuwa mwanasiasa.
Kwa bara hili la afrika huwezi badili mambo bila mikono ya wanasiasa...mtajitutumua lakini mwishoni wanasiasa wataingia tu,na hii inatokea kwa kuwa tumekuwa tumekuwa mabingwa wa kusema kuliko kutenda na hiyo ndiyo tabia inayotumaliza bila kujua
 
Kwa bara hili la afrika huwezi badili mambo bila mikono ya wanasiasa...mtajitutumua lakini mwishoni wanasiasa wataingia tu,na hii inatokea kwa kuwa tumekuwa tumekuwa mabingwa wa kusema kuliko kutenda na hiyo ndiyo tabia inayotumaliza bila kujua
Ni kweli wengi wanasema bila kutenda sababu hawana plan za kukamilisha kauli zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…