Hujaijua vizuri Afrika!

Rubawa

JF-Expert Member
Dec 25, 2015
2,055
3,239
HUJAIJUA VIZURI AFRIKA!

TUPO Afrika, bara letu. Utajiri mkuu wa Waafrika ni ubinafsi. Ukimpa madaraka leo Mwafrika, keshokutwa asubuhi utamkuta ameshaifanya Serikali kuwa mali ya ukoo. Baraza la Mawaziri kama kikao cha familia.

Ni Afrika ambayo nyakati za kudai uhuru wazee walipaza sauti kwamba “heri dhiki palipo na uhuru kuliko ukwasi utumwani.” Nimenukuu maneno ya Ahmed Sékou Touré, akiwaambia Wafaransa mwaka 1958. Wafaransa wakakaa kando, Guinea ikapata uhuru. Ndio, ni Guinea Conakry.

Basi, Sékou Touré akaingia Ikulu na kuitawala Guinea kwa miaka 26. Akafia madarakani mwaka 1984. Lansana Conté akafanya mapinduzi, akaingia madarakani, akatawala miaka 24. Naye akafia madarakani mwaka 2008.

Baada ya kifo cha Conté, Kapteni Moise Camara akaongoza mapinduzi na kujitangaza Rais. Naye Camara akapigwa risasi na mlinzi wake. Akiwa kwenye matibabu Morocco, uchaguzi ukafanyika Guinea. Alpha Condé, aliyekuwa mpigania demokrasia kwa muda mrefu, akaingia madarakani.

Jumapili iliyopita, Guinea walifanya uchaguzi. Condé amewania urais kwa muhula wa tatu. Ilibidi kuipindua Katiba na kuondoa kifungu kilichoweka ukomo wa vipindi viwili vya uongozi ili Condé aweze kugombea muhula wa tatu.

Condé, 82, alifungwa jela akipigania demokrasia kipindi cha utawala wa Conté, lakini amekanyaga Katiba na kusababisha vifo vya makumi ya watu ili abaki madarakani. Labda, naye atafia madarakani kama Sékou Touré na Conté , nani anajua? Mungu anajua.

Ni Afrika. Kama Yoweri Museveni na utawala wake Uganda utakaofikisha miaka 35 Januari 29, 2021. Yeye Rais, Mkuu wa Nchi, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu, mwanaye Muhoozi Kainerugaba ni Luteni Jenerali wa Jeshi la Uganda. Mkewe, Janet Kainembabazi ni Waziri wa Elimu na Michezo. Unaona?

Alassane Ouattara, aliingia madarakani mwaka 2010, ikiwa ni baada ya mtangulizi wake, Laurent Gbagbo, kujaribu kung’ang’ania madaraka. Ouattara akaonekana asingegombea muhula wa tatu. Ivory Coast itafanya uchaguzi Oktoba 31, mwaka huu. Ouattara ni mgombea. Wananchi waliandamana, damu ikamwagika. Hakuna kilichobadilika.

HAYO TUMEYAZOEA?

Uroho na ulafi wa madaraka haujawahi kuwa sifa ya mbali kwa watawala wa Afrika. Kutoka kwa kisiki Paul Biya, Cameroon mpaka anguko la aibu la Robert Mugabe, Zimbabwe. Anzia kwa Denis Sassou Nguesso, Jamhuri ya Congo (Congo Brazzaville) hadi Teodoro Obiang Mbasogo, Equatorial Guinea.

Baada ya kufika Equatorial Guinea, sasa tuingie ndani kidogo tukayaone ya Afrika. Rais Teodoro Obiang yupo madarakani tangu mwaka 1979. Miaka 41 imekatika. Aliingia madarakani baada ya kumpindua na kumuua mjomba wake, Francisco Macías Nguema.

Mwaka 1968, Macías Nguema, aliipatia uhuru nchi yake kutoka kwa Hispania. Baada ya uhuru, Macías Nguema akaifanya Serikali ya Equatorial Guinea kuwa mali ya familia yake. Wizarani na Jeshini akajaza wanafamilia. Baadaye wanafamilia wakageukana. Teodoro Obiang akampindua na kumuua mjomba wake, Macías Nguema.

Zikafuata zama nyingine za familia kujitanua madarakani. Nchi maskini yenye utajiri wa mafuta, familia moja inafilisi mkate wote. Wananchi wanaishi katikati ya umaskini mkubwa. Nani anajali?

Sasa, katika mgawo wa vyeo kwa familia, yupo Teodoro Nguema Obiang. Ni mtoto wa damu wa Rais Teodoro Obiang. Teodoro Nguema ndiye Makamu wa Rais wa Equatorial Guinea. Hivyo, baba Rais, mtoto Makamu wa Rais. Ladha hii hupatikana Afrika tu. Zingatia, Equatorial Guinea sio taifa la kifalme.

Maisha ya Teodoro Nguema ni tamthiliya iliyokithiri ufahari. Wananchi wa Guinea wanapigika, yeye anavyoishi unaweza kudhani ni maisha ya kufikirika, kama James Bond katika maandishi ya galacha wa Uingereza, Ian Fleming.

Leo, BBC wameripoti kuwa Teodoro Nguema yupo likizo Maldova, akila raha za daraja la kwanza duniani. Kwa siku analipa hoteli dola 50,000 (Sh116 milioni). Wakati huohuo, Equatorial Guinea, nchi ndogo yenye watu takriban milioni 1.5, wengi wao, leo hii ama wameshinda njaa au watalala bila kula.

Mwaka 2017, Mahakama Ufaransa ilimhukumu Teodoro Nguema kifungo cha miaka mitatu jela (hakuwepo mahakamani). Ni baada ya kumkuta na hatia ya kupora mali za Equatorial Guinea na kwenda kuwekeza Ufaransa. Mahakama ilitaifisha majumba na magari ya kifahari ya Teodoro Nguema. Jumla ya mali zote zilikuwa dola 178 milioni. Sawa na Sh413 bilioni.

Mwaka 2014, Voice Of America (VOA), waliripoti kuwa Serikali ya Marekani ilitaifisha mali za Teodoro Nguema zenye thamani ya dola milioni 38 (Sh88.2 bilioni). Mali hizo ni pamoja na jumba la kifahari alilonunua ufukweni, jijini Malibu, California, vilevile baadhi ya vitu vya Michael Jackson, ikiwemo glovu, ambazo alinunua kwenye mnada.

Uamuzi wa kumnyang’anya mali hizo Teodoro Nguema ulifuata baada ya kumbaini kwamba mwaka 2011, aliingia Marekani na dola 80 milioni (Sh185.6 bilioni), alizozipata kwa njia zisizo halali, kisha kuzitumia kuwekeza nchini humo.

Mwaka 2018, mali za Teodoro Nguema, zenye thamani ya dola 16 milioni (Sh37.2 bilioni), zilitaifishwa Brazil. Polisi nchini humo walimbaini Teodoro Nguema na watu wake ambao hawakuwa na utambulisho wa kidiplomasia, kuingia Brazil na fedha taslimu dola 1.5 milioni (Sh3.5 bilioni), vilevile saa za kifahari zenye thamani ya dola 15 milioni, sawa na Sh34. 8 bilioni. Sheria ya Brazil fedha taslimu ambazo mtu anaruhusiwa kuingia nazo ni dola 2,400, Sh5.6 milioni.

Mwaka 2017, Serikali ya Uswis ilitaifisha magari ya kifahari na boti lenye anasa nyingi . Mali zote hizo ni za Teodoro Nguema. Jumla ni thamani ya mali zilizotaifishwa ni dola milioni 100. Ni sawa kabisa na Sh232 bilioni.

Pamoja na mali nyingi kutaifishwa, lakini bado hatetereki. Anaendelea kutumbua. Mwaka 2018, alipost picha Instagram akiwa na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, akasema ndio watu wenye nguvu kubwa ulimwenguni. Ni yeye na Putin.

Alipo, Teodoro Nguema, anasubiri baada ya baba yake, Teodoro Obiang, aapishwe kuwa Rais wa Equatorial Guinea. Ni Afrika. Bara letu. Unaweza kushangaa; akina Mwalimu Julius Nyerere na Nelson Mandela ilikuwaje wakawa viongozi wa Afrika sawa na akina Teodoro Obiang? Iliwezekanaje?

Ndimi Luqman MALOTO

FB_IMG_1603151965969.jpg
View attachment 1605581

Sent from my ANE-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Hapo hujamtaja MOBUTU. Ila saa nyingine huwa nafikiria hawa madikteta hawapaswi kulaumiwa. Unakuta kiongozi wa nchi unajitahidi kuendeleza nchi yako kwa nia njema lakini unazidiwa mbinu na MABEBERU unatambua kabisa hata ufanyeje mtaendelea kuwa masikini tu unajiongeza unaamua kula raha ww na familia yako na washkaji hadi MFE.
 
Umeeleza vizuri ila naomba nikukumbushe(sio kukurekebisha maana sina uwezo huo) kwamba Ahmed Sekou Toure alipinduliwa akiwa nje ya nchi kwa matibabu (ingawa kiuhalisia alikua amekimbia) na Lansana Beavogui aliyekua makamu wake ambaye naye baada ya kushika hatamu za uongozi kwa siku zisizozidi tano alipinduliwa na Lansana Conte. Ni hayo tu Kiongozi wangu, otherwise ni bandiko zuuuri sana
 
Good.bandiko murua kabisa inasikitisha sana na kibaya zaidi ndivyo tulivyo afrika kubadilika haiwezekani..yan hatueleweki wanaojifanya watetezi nao wakiingia madarakani hali itakuwa ni hiyohiyo yan atakula adi apasuke
 
View attachment 1605582View attachment 1605581

Sent from my ANE-LX1 using JamiiForums mobile app

Umeandika vizuri mkuu. Big up
 
Hii inasikitisha sana.
Katika watu wa ajabu basi asilimia 95 ya waafrika ni watu wa ajabu.

Mwafrika ana vitu hivi hapa.
Uchoyo
Ujinga
Umasikini
Roho mbaya
Chuki
Ubinafsi
Ujeuri
Kutokujitambua
Kutokujielewa
Majisifu
Ukatili
Upumbavu na nyongeza ni low IQ.

Na baadhi ya hayo yaani ikiwemo chuki na ukatili mwafrika huyo atamfanyia mwafrika mwenzake na siyo mtu mwengine.

sasa najiuliza huyu mwafrika ni mtu wa aina gani na kwanini yuko hivi yaani jibu ni ngumu kulipata ila litapatikana.

What is wrong with us?
 
Good.bandiko murua kabisa inasikitisha sana na kibaya zaidi ndivyo tulivyo afrika kubadilika haiwezekani..yan hatueleweki wanaojifanya watetezi nao wakiingia madarakani hali itakuwa ni hiyohiyo yan atakula adi apasuke
Unaweza kubadirisha kila kitu bila kuwa mwanasiasa.
 
Hapo hujamtaja MOBUTU. Ila saa nyingine huwa nafikiria hawa madikteta hawapaswi kulaumiwa. Unakuta kiongozi wa nchi unajitahidi kuendeleza nchi yako kwa nia njema lakini unazidiwa mbinu na MABEBERU unatambua kabisa hata ufanyeje mtaendelea kuwa masikini tu unajiongeza unaamua kula raha ww na familia yako na washkaji hadi MFE.
Then hukuwa na nia ya kweli kuendeleza hiyo nchi.

Mtu mwenye nia atafanya chochote ili afanikiwe anachokitaka.
 
HUJAIJUA VIZURI AFRIKA!

TUPO Afrika, bara letu. Utajiri mkuu wa Waafrika ni ubinafsi. Ukimpa madaraka leo Mwafrika, keshokutwa asubuhi utamkuta ameshaifanya Serikali kuwa mali ya ukoo. Baraza la Mawaziri kama kikao cha familia.

Ni Afrika ambayo nyakati za kudai uhuru wazee walipaza sauti kwamba “heri dhiki palipo na uhuru kuliko ukwasi utumwani.” Nimenukuu maneno ya Ahmed Sékou Touré, akiwaambia Wafaransa mwaka 1958. Wafaransa wakakaa kando, Guinea ikapata uhuru. Ndio, ni Guinea Conakry.

Basi, Sékou Touré akaingia Ikulu na kuitawala Guinea kwa miaka 26. Akafia madarakani mwaka 1984. Lansana Conté akafanya mapinduzi, akaingia madarakani, akatawala miaka 24. Naye akafia madarakani mwaka 2008.

Baada ya kifo cha Conté, Kapteni Moise Camara akaongoza mapinduzi na kujitangaza Rais. Naye Camara akapigwa risasi na mlinzi wake. Akiwa kwenye matibabu Morocco, uchaguzi ukafanyika Guinea. Alpha Condé, aliyekuwa mpigania demokrasia kwa muda mrefu, akaingia madarakani.

Jumapili iliyopita, Guinea walifanya uchaguzi. Condé amewania urais kwa muhula wa tatu. Ilibidi kuipindua Katiba na kuondoa kifungu kilichoweka ukomo wa vipindi viwili vya uongozi ili Condé aweze kugombea muhula wa tatu.

Condé, 82, alifungwa jela akipigania demokrasia kipindi cha utawala wa Conté, lakini amekanyaga Katiba na kusababisha vifo vya makumi ya watu ili abaki madarakani. Labda, naye atafia madarakani kama Sékou Touré na Conté , nani anajua? Mungu anajua.

Ni Afrika. Kama Yoweri Museveni na utawala wake Uganda utakaofikisha miaka 35 Januari 29, 2021. Yeye Rais, Mkuu wa Nchi, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu, mwanaye Muhoozi Kainerugaba ni Luteni Jenerali wa Jeshi la Uganda. Mkewe, Janet Kainembabazi ni Waziri wa Elimu na Michezo. Unaona?

Alassane Ouattara, aliingia madarakani mwaka 2010, ikiwa ni baada ya mtangulizi wake, Laurent Gbagbo, kujaribu kung’ang’ania madaraka. Ouattara akaonekana asingegombea muhula wa tatu. Ivory Coast itafanya uchaguzi Oktoba 31, mwaka huu. Ouattara ni mgombea. Wananchi waliandamana, damu ikamwagika. Hakuna kilichobadilika.

HAYO TUMEYAZOEA?

Uroho na ulafi wa madaraka haujawahi kuwa sifa ya mbali kwa watawala wa Afrika. Kutoka kwa kisiki Paul Biya, Cameroon mpaka anguko la aibu la Robert Mugabe, Zimbabwe. Anzia kwa Denis Sassou Nguesso, Jamhuri ya Congo (Congo Brazzaville) hadi Teodoro Obiang Mbasogo, Equatorial Guinea.

Baada ya kufika Equatorial Guinea, sasa tuingie ndani kidogo tukayaone ya Afrika. Rais Teodoro Obiang yupo madarakani tangu mwaka 1979. Miaka 41 imekatika. Aliingia madarakani baada ya kumpindua na kumuua mjomba wake, Francisco Macías Nguema.

Mwaka 1968, Macías Nguema, aliipatia uhuru nchi yake kutoka kwa Hispania. Baada ya uhuru, Macías Nguema akaifanya Serikali ya Equatorial Guinea kuwa mali ya familia yake. Wizarani na Jeshini akajaza wanafamilia. Baadaye wanafamilia wakageukana. Teodoro Obiang akampindua na kumuua mjomba wake, Macías Nguema.

Zikafuata zama nyingine za familia kujitanua madarakani. Nchi maskini yenye utajiri wa mafuta, familia moja inafilisi mkate wote. Wananchi wanaishi katikati ya umaskini mkubwa. Nani anajali?

Sasa, katika mgawo wa vyeo kwa familia, yupo Teodoro Nguema Obiang. Ni mtoto wa damu wa Rais Teodoro Obiang. Teodoro Nguema ndiye Makamu wa Rais wa Equatorial Guinea. Hivyo, baba Rais, mtoto Makamu wa Rais. Ladha hii hupatikana Afrika tu. Zingatia, Equatorial Guinea sio taifa la kifalme.

Maisha ya Teodoro Nguema ni tamthiliya iliyokithiri ufahari. Wananchi wa Guinea wanapigika, yeye anavyoishi unaweza kudhani ni maisha ya kufikirika, kama James Bond katika maandishi ya galacha wa Uingereza, Ian Fleming.

Leo, BBC wameripoti kuwa Teodoro Nguema yupo likizo Maldova, akila raha za daraja la kwanza duniani. Kwa siku analipa hoteli dola 50,000 (Sh116 milioni). Wakati huohuo, Equatorial Guinea, nchi ndogo yenye watu takriban milioni 1.5, wengi wao, leo hii ama wameshinda njaa au watalala bila kula.

Mwaka 2017, Mahakama Ufaransa ilimhukumu Teodoro Nguema kifungo cha miaka mitatu jela (hakuwepo mahakamani). Ni baada ya kumkuta na hatia ya kupora mali za Equatorial Guinea na kwenda kuwekeza Ufaransa. Mahakama ilitaifisha majumba na magari ya kifahari ya Teodoro Nguema. Jumla ya mali zote zilikuwa dola 178 milioni. Sawa na Sh413 bilioni.

Mwaka 2014, Voice Of America (VOA), waliripoti kuwa Serikali ya Marekani ilitaifisha mali za Teodoro Nguema zenye thamani ya dola milioni 38 (Sh88.2 bilioni). Mali hizo ni pamoja na jumba la kifahari alilonunua ufukweni, jijini Malibu, California, vilevile baadhi ya vitu vya Michael Jackson, ikiwemo glovu, ambazo alinunua kwenye mnada.

Uamuzi wa kumnyang’anya mali hizo Teodoro Nguema ulifuata baada ya kumbaini kwamba mwaka 2011, aliingia Marekani na dola 80 milioni (Sh185.6 bilioni), alizozipata kwa njia zisizo halali, kisha kuzitumia kuwekeza nchini humo.

Mwaka 2018, mali za Teodoro Nguema, zenye thamani ya dola 16 milioni (Sh37.2 bilioni), zilitaifishwa Brazil. Polisi nchini humo walimbaini Teodoro Nguema na watu wake ambao hawakuwa na utambulisho wa kidiplomasia, kuingia Brazil na fedha taslimu dola 1.5 milioni (Sh3.5 bilioni), vilevile saa za kifahari zenye thamani ya dola 15 milioni, sawa na Sh34. 8 bilioni. Sheria ya Brazil fedha taslimu ambazo mtu anaruhusiwa kuingia nazo ni dola 2,400, Sh5.6 milioni.

Mwaka 2017, Serikali ya Uswis ilitaifisha magari ya kifahari na boti lenye anasa nyingi . Mali zote hizo ni za Teodoro Nguema. Jumla ni thamani ya mali zilizotaifishwa ni dola milioni 100. Ni sawa kabisa na Sh232 bilioni.

Pamoja na mali nyingi kutaifishwa, lakini bado hatetereki. Anaendelea kutumbua. Mwaka 2018, alipost picha Instagram akiwa na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, akasema ndio watu wenye nguvu kubwa ulimwenguni. Ni yeye na Putin.

Alipo, Teodoro Nguema, anasubiri baada ya baba yake, Teodoro Obiang, aapishwe kuwa Rais wa Equatorial Guinea. Ni Afrika. Bara letu. Unaweza kushangaa; akina Mwalimu Julius Nyerere na Nelson Mandela ilikuwaje wakawa viongozi wa Afrika sawa na akina Teodoro Obiang? Iliwezekanaje?

Ndimi Luqman MALOTO

View attachment 1605582View attachment 1605581

Sent from my ANE-LX1 using JamiiForums mobile app
Mawazo ya vichwa vyao ni umate umate tu tuwaache maana kustaafu kwao hadi wafariki
 
  • Thanks
Reactions: Gef
Binadamu tupo Species tofauti,Nadhani hiyo Species huku kwetu bado haijapatikana! Tunapakana matope tu mitandaoni...na siku ikigundulika mtu wa hivyo huku kwetu kwa ushahidi kabisa kama huyo Teodoro Patachimbika.
 
Back
Top Bottom