hujafa hujaumbika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hujafa hujaumbika

Discussion in 'JF Doctor' started by Redey, Jan 14, 2011.

 1. R

  Redey Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanajamvi kwa mara nyingine naomba mchango wenu kimawazo. Kuanzia jtatu wiki hii nasikia maumivu makari sana upande mmoja wa shavu like shoti ya umeme au kama vile moto unaniunguza. Nimetembelea vituo vya afya na wamenipa dawa lakini sioni nafuu. Swali langu kwenu wenyeufahamu na tatizo hili-
  nini kifanyike ili kuondokana na hili tatizo, au ni wapi naweza pata uhakika wa matibabu sahii. Natanguriza shukrani. Kweli natabika make kula hata kuongea kwangu sasa ni mateso makubwa. Weekend jema...
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  I googled it na nimekutana na majibu haya:

  Source: Doctors Lounge - Neurology Answers
   
 3. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  tatizo lako ni dogo njoo uombewa wengi wenye tatizo kama lako wamepona
   
 4. Sadukayo

  Sadukayo New Member

  #4
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  tatizo lako si dogo sana kama baadhi ya wadau wanavyodhani. Kutokana na maelezo yako na taaluma yangu, tatizo lako linaitwa "trigeminal neuralgia" huwa halina maelezo ya kuridhisha kuhusu chanzo chake lakini kuna sehemu fulalni ambayo inapoguswa tatizo huanza, sehemu hii inaitwa, "TRIGGER ZONE". Matibabu yake ni kama mdau mmoja hapo juu alivyo-suggest. Tumia dawa zizazotibu mishipa ya fahamu(nerves) na zenye vitamini. (Dawa kama Neurobion forte) inaweza kusaidia, ikishindikana hapo nenda hospitali kama Muhimbili kitengo cha matibabu ya kinywa na meno, ulizia mtaalam mwenye ujuzi ufuatao(maxillofacial surgeon), au neurologist kama wazo la hapo juu. Ugua pole!
   
Loading...