Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Binadamu wana tabia ya kinafiki sana, wanacheka na wewe na kukushauri Kisha wanautoa ushauri wao nje kwenda kukuangamiza. Tangu aingie mama Samia suluhu uvujaji wa Taarifa umepungua Jambo linaloonyesha Kwamba waliokuwa wanavujisha siri ni watu wale wale waliokuwa wanapaswa kuzihifadhi.
Naamini Mama Samia hana timu mpya sana na wala waliomzunguka siyo ndugu Wala rafiki yake Bali ni Watumishi wale wale waliomzunguka JPM. Watumishi hawa wanasali na wana imani lakini kikubwa wanautambuzi wa mema na mabaya. Wengi wa watendaji kwenye ofisi hii nyeti wameapa kuiilinda nchi ndipo wamlinde kiongozi wa nchi. Ikitokea kiongozi mwenye nchi akaisaliti nchi watu hao lazima watatafuta namna ya kuvujisha taarifa kudhibiti damage.
Kwa muktadha huo naanza kuamini wbado Wapo Wazalendo ikulu ambao pamoja na kukabidhiwa nafasi nyeti wanaweza kutoa taarifa wanazodhani zinaliumiza Taifa ili wananchi wajue na mwenye nchi ajue wananchi wanamjua kuliko anavyojijua.
Kosa lililofanywa na mfumo ni kupambana kuzuia taarifa zisitoke badala yakudhibiti uharibifu wa Taifa letu. Uwekezaji uliofanywa kudhibiti Siri ulikuwa mkubwa na wanufaika wanaweza kuwa ni walewale waliovujisha Siri ndio walipewa jukumu lakujitafuta bila kujua ni vigumi kujipata.
Nimshukuru Mama Samia kuua mradi huu wakupambana na watoa Siri badala yake akaamua kutenda yaupendezayo mfumo Hadi ukaona hakuna damage. Asipotoke akaendelea kudhibiti maana anaowatumia kudhibiti ndio hao hao wanaovujisha Siri ili waendelee kupewa kazi ya kudhibiti.
Nasema ni system kwa sababu hata wizi wa mabilioni uliofanywa kupitia EPA na Escrow haukujulikana kwa serikali kudhamiria ujulikane ila watu wachache Wazalendo walivujisha Siri na nyaraka watu wakanyanyuka nazo Bungeni nakumfanya Mzee wa Msoga asafiri nje akatulie Kwanza kutafakari anapangua vipi siri zilizovuja.
Wabarikiwe watoa siri wanaotufanya tujue mianya ya wizi na kuwafanya Wazalendo kuiziba. Leo hii hata taarifa za uteuzi hazivuji japo sasa nazo zinakosa vetting ya kutosha hadi makapi nayo yanapitishwa na kuwapa agenda Wasaga sumu kupata agenda mitandaoni.