Huenda kuna waislam wengi duniani wameshazikwa wakiwa hai

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,061
35,977
Ni utaratibu mzuri sana wa kuwahi kuzikana, ukikata moto asubuhi mchana tunazika

Ila nina hakika kuna watu wengi wameshazikwa Ili hali wakiwa wamezimia au wakiwa kwenye coma, hasa vijijini pasipo na hospitali na daktari wa kuthibitisha kifo.

Kuchelewa kuzika ni mbaya ila ina faida zake, maiti inaeza kupiga chafya. Mwaka 2012 mchezaji Fabrice Muamba wa Bolton wakicheza dhidi ya Spurs alianguka uanjani na moyo wake ulisimama kwa dakika 78.

Referee Howard Webb aliahirisha mechi huku machozi yakimtoka, uwanja mzima ni huzuni madaktari wa kizungu na kudra za Mungu jamaa akaamka bwana na kustaafu mpira rasmi.

Angekuwa Afrika tungeshamsahau na mke wake angekuwa single mother tayari, ila jamaa anakula bata tu.
 
Ni utaratibu mzuri sana wa kuwahi kuzikana,ukikata moto asubuhi mchana tunazika
Ila utaratibu huu nina hakika kuna mamilioni walizikwa Ili hali wakiwa wamezimia au wakuwa kwenye coma,hasa vijijini pasipo na hospitali
Chelewa chelewa ni mbaya ila ina faida zake,maiti inaeza kupiga chafya
Ushahidi tafadhali.
 
Kabisa hilo nakubaliana na wewe

Tena kwa africa ndio usiseme tumezika wagonjwa wengi sana waliozimia

Taarifa ya mtu kufa inatangazwa asubuhi kua mgonjwa amekufa alfajiri halafu saa 7 mchana watu wanapanga reli
 
Upo sahihi kabisa,nimekua nikiwaza hivyo.

Mfano nilishuhudia Muscat mshkaji wetu alipata ajali asubuhi saa 3...kufikia saa 11 jioni watu walikua wanafungua turubai pale kwao,yaani ni kwamba shughuli ilishaisha..watu washazika na wameshatawanyika..!

Saa 12 jioni siku hiyo unapita pale kwao nje maisha yanaendelea utadhania hakuna kilichotokea!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom