Imekuwa ni kawaida iliyozoeleka Ocean Road kwa mgonjwa kufika kwenye miadi ya tiba (kama ilivyopangwa) asubuhi saa moja na kuja kupata huduma saa nne usiku.
Hutokea wakati hata hiyo usiku anaweza bado tiba asipate. Hakuna taarifa zozote zinazotolewa kuhusiana na ucheleweshwaji huu zaidi ya kuwa subirini.
"Mazingira wezeshi kabisa ya rushwa."
Wenye pesa zao, ma V8, wenye utambulisho kutoka Zenji huko nk, hao hutibiwa tiba hizo hizo bIla usumbufu na kwa wakati kama wanavyofika na kujiondokea.
Wagonjwa hawa wengi wao ni wazee waliodhoofu sana. Kukaa hospitali bila kula kutokea asubuhi hadi usiku, ni jambo la kushangaza sana.
Kwa wiki kama tatu zilizopota hali ilionekana kutengamaa baada ya malalamiko makali. Hata hivyo hali imeanza kurejea kule kule tena.
Hali hii hadi lini? Au hadi wagonjwa waandamane kama wale wa TRL Dodoma? Hapo hadi Magogoni si ni umbali wa pua na mdomo?
Acheni kusumbua wagonjwa. Kwa nini miadi isiwekwe kumwezesha mgonjwa mmoja kutokaa zaidi ya saa moja kwenye foleni akisubiri?
Rushwa hadi kwa mgonjwa aliye taabani?
Kwani tunakwenda misikitini au makanisani kufanya nini?
Kila mahali shida zile zile za upigaji. Tutafika tukiwa tumechoka sana.
Mola atufanyie wepesi.