Huduma za maabara katika Hospitali Mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Singida zinatolewa katika Jengo la Jiko na Kufulia nguo

Kibabe

New Member
Jul 20, 2023
2
1
Katika hali ya kushangaza Mh Naibu Waziri wa Afya Mh Molleli alielekeza huduma za Hospitali ya rufaa ya Mkoa kuhama katika majengo yaliyokuwa ya kitumika hapo awali ambapo huduma za maabara na vipimo zilikuwa zinatolewa katika jengo lenye hadhi na vifaa vya kutosha. Matokeo ya kutekeleza maelekezo ya Mh Naibu Waziri Menejimenti ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa waliamua kuhamishia huduma za maabara na vipimo katika jengo ambalo ni jiko la kupikia na jengo la kufulia nguo kitu ambacho ni hatari kwa Afya za Wananchi.

Sio tu huduma za maabara hata huduma za kulaza wagonjwa waliopasuliwa na wagonjwa wa magonjwa ya ndani wanalazwa katika Korido na vyumba ambavyo sio wodi kitu ambacho ni hatari kwa afya za wananchi.
 
Back
Top Bottom