Serikali ya ccm na wabunge wake wamekuwa wakiwatangazia wananchi eti huduma za afya kwa watoto chini ya m5,wajawazito na wazee matokeo yake wanakuja na kukuta huduma hazipo, matokeo yake manesi na madaktari wanabaki kutukanwa eti hawatoi huduma nzuri, mara nyingi madaktari wanawaandikia wagonjwa mahitaji wakanunue. Lakini pia hata wagonjwa wengine wanalipia huduma matokeo yake hata huduma wanayolipia hawapati je haya ndo maisha bora? Tufike mahali tuwerealistic wahudum wa afya wanapata matusi na wengine wanapigwa na relatives eti hawatoi huduma, hawa wahudumu watoe nin kama madawa, canula na drips hazipo. Wa jf tuelimishe jamii ielewe kudai haki zao. Kumtukana nes au dr si kutatua tatizo ila tatizo ni watwala hawatoi hela. Kazi kukazana kulipa dowans wananchi wao wanakufa kila siku.