Huduma mbovu Train ya Deluxe

The Spirit of Tanzania

JF-Expert Member
Mar 7, 2020
534
924
Wakuu heshima kwenu;

Katika mashirika ya Serikali ambayo yanapaswa kuwa na huduma za kueleweka ni hili la huduma za usafiri,hasa nikimaanisha train maana ndio kuna mkono wa serikali ukitoa lile shirika lenye zile mashine zirukazo angani.

Lakini katika hali ya kushangaza train ya deluxe kutoka kaliua kwenda dar imeondoka jana kaliua ila hadi muda huu haijafika dar,katikati hapo kabla ya kufika dodoma wasafiri wamekaa zaidi ya masaa matatu wakiwa wamesimama haisemwi tatizo nini,baada ya kufika Dodoma imeondoka saa 3 hivi kuelekea Dar,ila kufika Mpwapwa imesimama masaa matano, yaani tokea saa 6 mchana na wafanyakazi wa train kwa kujua wanafanya uhujumu wameipeleka train ambako hakuna huduma hata za chakula wala mawasiliano ndio wakasimama.

TRC mbona hamtendei haki watanzania?

Hizi train za umeme si mtaua watu tu ikiwa zilizopo zimewashinda kuendesha?

Kwanini mnatoa huduma mbovu kiasi hiki?

Mbona shirika zuri hili linakufa kizembe?
Chukulia mtu atatoka mwanza atafika Dar,wewe uliyeanzia tabora haujafika
 
wanataka life kuharibu legacy ili mababery yabinafisshiwe
kuna muda nawaza hivi hawa wenye uongozi haya mashirika ya serikali wana akili sawa sawa?,
yaani kuna mambo yanafanyika unajua kabisa huu ni uhujumu tu;
train walipoipeleka hata migahawa hakuna,na inasemekana walijua kuna tatizo mapema mbele,wameenda kuificha porini;
 
Sitaki kusema bora kupanda bus maana vipato havilingani.
Yote kwa yote wahusika wafanyie kazi tena kwa haraka zaidi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom