KERO Huduma duni RITA Call Center; Haitoi msaada wala majibu

KERO Huduma duni RITA Call Center; Haitoi msaada wala majibu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa mujibu wa maelezo yao @ritatanzania kituo cha miito (CALL CENTER) inakuwa wazi kuanzia saa mbili asubuhi hadi sa 10 jioni, changamoto ni kwamba ukipiga simu ndani ya muda huo hawapokei, sometimes inaweza kuita then wanakata.

Maana ya kuweka baadhi ya huduma zao zifanyike kwa mtandao ni kusogeza huduma karibu na wananchi, lakini unakuta mtu amelipia huduma ya kusajili cheti kipya 20,000 lakini kinakaa zaidi ya miezi miwili acount status haibadiliki, unachukua uamuzi wa kupiga simu ili ujue changamoto ni nini hawapokei, unafunga safari kutoka kijijini kilomita nyingi hadi ofisi zao za wilaya, ukifika kule wanakupandishia mabega.

Changamoto zetu tutaziwasilishaje ikiwa call center inahuduma mbovu? @ritatanzania AU CHANGAMOTO HII NI MIMI TU, JE NA NYIE WATANZANIA WENZANGU MNAKUTANA NA CHANGAMOTO KAMA YANGU? TUKIPAZA SAUTI WANATUGWAJIMANIZE 😭

Hiki cheti kipya kina zaidi ya mwezi na wiki status ipo verified, nilishalipia 20,000 SINA KWA KUZIPELEKA CHANGAMOTO ZANGU ILI NIPATE MSAADA.

Namba ya huduma kwa Mteja 0800 117 482

=======================

Malalamiko mengine ya Wananchi niliyaona kwenye ukurasa wake wa Instagram
rITA.jpg

Ritaa.jpg

Screenshot 2025-06-14 092041.jpg

Screenshot 2025-06-14 092145.jpg
 
Mimi Toka wiki lililopita nahangaika na Hawa jamaa, hadi ikamibidi nifungue Uzi humu.. vyeti wanatoa wao halafu wanataka Tena tuverify.. nimeshindwa kupata usajiri wa NHIF kwa mke wangu na mwanangu kisa ni hao wapiuzi RITA
 
Kwanz ivi hii ni ainq gani ya kodi
Kwamba cheti wametoa wao na bado ukita kukitumia kwa mfanooo hawa madogo wa f6 kuombeq mkopo utasikia fanya verification ambapo utalipa tena ela...

Lakin pia hata macho kwa macho huduma zao ni duni saaan na zenye dharau kubwa kwa wale waendao kukutana nao offisini kwao
Kwan nishawahi fuatiliq marekebisho ya cheti change cha kuzaliwa pale posta
Kufika pale mapokezi na kueleza shida angu naambiwa rudi baada y siku 7 ili tu wakiangalie kam kip kweny system
Nikawa mpole nikaludi baada ya sik 7 nafika naambiwa chet chako kipo kwa system haya ludi tareh fuln kuanza process.
Kirahisi tyu mt anakwambia ivo na ukiuuliza wanakukata jicho na kuomba uwapishe wengine wahudumiwe
 
Back
Top Bottom