Huawei yajidhatiti

Huawei wajitoe kwenye siasa maana hawatakuwa na mwisho mzuri walianza australia haikuwa shida sasa U S A naona ataipokea U K na wengine ila watu wamebase kwenye mobile phone hususani smartphone lakini huko sio sababu ban lilianzia kwenye telecom infrastrure hasa hii ya 5G ambayo imeonekana kuwa loophole nyingi zinazowapa nafasi ya udukuwaji hili janga limewapata nchi ya australia na walishapiga ban muda mrefu sana sema halikuwa main stream
 
May be. Ila Dunia ya sasa ipo huru sana. Hao fasebuk twita, IG ni wafanya Biashara. Wanatafuta Fursa ipo wapi na wanaitumia. Sidhani kama Marekani atakuwa na say juu apps Social networks ambazo ni za US
Hata google ni mfanyabiashara lakini linapokuja swala la national interest basi anakosa ujanja mana Taifa kama taifa kuna muda linamkingia kifua au kumpa promotion zaidi, Ninachokiona Huawei atakuja na OS yake ila developers wa Apps kubwa kubwa kama Whatsapp, Insta, Twitter, YouTube waka goma kuingia ktk Store za Os yao hio na hapo ndio inakuwa mwisho kabisa nani yupo tayari kutumia gadgets bila western apps
 
Hakuna jipya hapo.Mzungu ni mnafiki sana.Hawajapenda kitendo cha China kuanza kuisambaza 5G.
 
vipi kuhusu tecno zetu hizi nazo si za china wasije wakazuia tu hapa!
 
hii vita ipo siku mmoja wapo atashindwa na upande wangu namuona marekani akielekea shimoni. Wachina wanaona mbali sana ndo maana walianza hata kuundanda GPS System yao mapema isije tokea siku 'cha bure' wakanyimwa kukitumia kama wanavyopigwa ban kwenye OS tu.
 
Kuhusu huawei kuzindua 5G siyo tatizo kwa Marekani
Tatizo ni huawei kuweka mfumo wa kiupelelezi kwenye device zao
Mengine ni stori za vijiweni tu
 
Wote wanakula hasara kubwa Sana. Mabilioni ya dollar. Wamerekani wanajadiliana kuhusu mkataba huo. Wanaona hasara watu bilioni Moja duniani. Na wanasubiri uwamuzi wa serikali ya uchina watakavyolipiza
 
Hawa jamaa wasipo angalia hili ndo anguko lao,,Yani kama nawaona vile..Wacha tuone mtanange unakuaje..Tunaanzia kwenye P40
Wachina wakifanikiwa basi marekani itakuwa imejimaliza yenyewe hapo USA tumbo joto maana wanategemea app za android kufanya ujasusi Ila Kwa vyovyote mchina atashinda nyuma ya swala ili zipo serikali hivyo serikali ya China aiwezi kukubari kushindwa ukizingatia China ni tajiri
 
Mpelelezi mkuu duniani ni USA.Kila kampuni ya kimawasiliano ya kimarekani FBI wana back doors zao.USA aache kuihadaa dunia.
Kuhusu huawei kuzindua 5G siyo tatizo kwa Marekani
Tatizo ni huawei kuweka mfumo wa kiupelelezi kwenye device zao
Mengine ni stori za vijiweni tu

Sent from my TA-1024 using JamiiForums mobile app
 
Kujizatiti mkuu sio kujidhatiti.
 
Compatible Kwa apps za Android wakati nimesikia wamewekewa vikwanzo kua hawaruhusiwi kutumia apps za Android kwenye os yao kama vile whatsapp facebook instagram and twitter.
Hhh umeskia sio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…