Huawei Ascend y300 na matatizo ya mic

Wana jamvi hii simu nimenunua kwenye posta dar kwenye tigoshop kama mnavyofahamu inauzwa sana huko. Ila baada ya kuanza kuitumia lwo ikiwa siku kama ua 6 nimeanza kuona matatzo ninapokuwa napokea simu au kupiga. Baada y kuanza kuongea ghafla ninae ongea anakuwa anisikii ila mimi namsikiap vyema.

Sasa hili sijui litakuwa ni tatizo la hizi simu, kwani stori kama hii nimeiskia kwa watu wengine wawili kabla yangu.
- Na mmoja wao alipojaribu kuwarudishia tigo wanamletea longolongo.

Ushauri wenu wana JF.
-mwenye experience nahizi simu.. kama ndio tatizo lake tatizo tutoe ushauri kwa wengine kuziepuka.
- aliyepatwa na tatizo kama hili na njia nzuri ya kuli'overcome.

Cc C6 chief-mkwawa Young Master

Hilo ni tatizo la software ina makosa kwenye coding, kwa kuwa sasa natumia simu! Kesho ntajitahidi kuandika procedure za kufwata ili kulitatua.
 
Last edited by a moderator:
Hilo ni tatizo la software ina makosa kwenye coding, kwa kuwa sasa natumia simu! Kesho ntajitahidi kuandika procedure za kufwata ili kulitatua.

Am waiting ndugu... hii hali inanitesa sana.
 
Hilo ni tatizo la software ina makosa kwenye coding, kwa kuwa sasa natumia simu! Kesho ntajitahidi kuandika procedure za kufwata ili kulitatua.

Unfortunately the software coding would only help for voip calls, anyway am still searching for a solution then i will bring it hapa
 
Mi natumia wiki ya pili sasa.mwanzo nilipata tatizo kama hilo nikawapelekea tigo as ivi iko poa.il a tatizo sijaweza kudownload video.nimejaribu application said I ya tatu

Mkuu PANdigichiza wewe ulinunulia tigoshop ipi!!??
 
Hilo suala screen kufa ni common sana?
Na vipi kuhusu hili tatizo la mic hao mafund wanaweza nisaidia

Screen za smartphone kufa ni kutokana na charger unayotumia, sababu nyingi zina screen mbili ya ndani na ya juu "touch " ambazo hufanya kazi Kwa electric field in between. Kwa hiyo ukiweka charger ilopitiliza ina disturb hizo field ndo mwanzo wa kugusa w inaandika e .
 
Hilo ni tatizo la software ina makosa kwenye coding, kwa kuwa sasa natumia simu! Kesho ntajitahidi kuandika procedure za kufwata ili kulitatua.
wakuu naomba namie soln ya hili tatizo
simu y300 yangu nayo imeanza hili tatizo.

deogan
 
Last edited by a moderator:
Wakuu hata mimi nina experience hilo tatizo kwenye simu yangu siwezi kuongea zaidi ya dakika tatu mic inazingua nilinunua pale mliman cty pale tigo shop ngoja jumatatu niwatilie maguu nikajua ni tatizo la kwangu peke yangu
 
Na vipi kuhusu betri yake, naona kama betri za hizo simu za huawei zinaisha charge mapema sana. Pia ndugu wana jamvi, naomba msaada wenu, nina simu samsung model number GT-S5253 siwezi kusoma/kutuma email. Je, ni kweli kwamba hazina uwezo huo? Kama sio, nifanyeje niweze kusoma/kutuma email? Nitashukuru kwa msaada wenu.
 
Wakuu hata mimi nina experience hilo tatizo kwenye simu yangu siwezi kuongea zaidi ya dakika tatu mic inazingua nilinunua pale mliman cty pale tigo shop ngoja jumatatu niwatilie maguu nikajua ni tatizo la kwangu peke yangu
vipi tatizo lako walirekebisha
 
vipi tatizo lako walirekebisha
nilienda wakaniambia niache simu waipeleke kwa mafundi wao bahati mbaya mimi nilikuwa na data zangu ambazo ni muhimu kwa matumizi ya kesho yake na sikuwa na sehemu yoyote ya kuweka kwa muda ule nafikiri kurudi jumatatu ntakupa mrejesho mkuu
 
nilikumbwa na tatizo hili ila baada ya kufanya factory data reset tatizo likaisha sasahivi natwanga tu bila kikomo
 
Mkuu nieleweshe hiyo firmware ndio inakuwaje?
Na hiyo itamalizaje tatizo la mic

Firmware haina uhusiano na hardware , uimara wa hardware na ubora wa firmware(OS) havihusiani kabisa. kama tatizo ni unayeongea naye hakusikii, inawezekana mic imekufa(imeungua kwa sababu simu zinatumia digital Mic yenye Transistor kwa ndani). pia inawezekana tatizo sio mic bali ni components zingine zinazohusiana na mic kama vile Pre-Amp. Ushauri: peleka pale ulipo nunua . wakizingua tafuta fundi mzuri sio wale mafundi wa vibarazani..
 
nilienda wakaniambia niache simu waipeleke kwa mafundi wao bahati mbaya mimi nilikuwa na data zangu ambazo ni muhimu kwa matumizi ya kesho yake na sikuwa na sehemu yoyote ya kuweka kwa muda ule nafikiri kurudi jumatatu ntakupa mrejesho mkuu

asante.. nami ngoja niwapelekee tu
 
Back
Top Bottom