HTC unveils revamped HTC One

HTC unveils revamped HTC One

-mkuu blink feed si ndo mpya???? Mbona wasema ndo selling point?

-Hio sense ipo lakini sidhani kama inadRive selling maana by second quarter htc wanaanza kula loss. Mauzo yao yanashuka kama maporomoko ya maji bora nokia kuliko htc kwa sasa kama trending itaendelea hivi maybe mwakani hatutakua na htc.

Mkuu unaona nokia wamechemsha ila anashkilia 75% ya windows phone na bado anakua. Ina maana kila wp8 inavokua na nokia anakua so siku wp8 ikiwa kubwa na android kubwa. Nokia ana wp8 na samsung ana android htc atakua mgeni wa nani?

Na angalia apss za nokia huzikuti platform yoyote ni zake mwenyewe labda hii here map ndo kaanza kuieka kwenye ios na mozilla so we muone tu nokia kachemsha ila time itatuambia.

Mkuu nakushauri tembelea nokia beta lab apps za nokia zinapopikwa nenda kaangalie unique talent wale jamaa hawaangalii jamii inapenda nini? Wanaangali tubuni nini jamii itapenda
 
-mkuu blink feed si ndo mpya???? Mbona wasema ndo selling point?

-Hio sense ipo lakini sidhani kama inadRive selling maana by second quarter htc wanaanza kula loss. Mauzo yao yanashuka kama maporomoko ya maji bora nokia kuliko htc kwa sasa kama trending itaendelea hivi maybe mwakani hatutakua na htc.

Mkuu unaona nokia wamechemsha ila anashkilia 75% ya windows phone na bado anakua. Ina maana kila wp8 inavokua na nokia anakua so siku wp8 ikiwa kubwa na android kubwa. Nokia ana wp8 na samsung ana android htc atakua mgeni wa nani?

Na angalia apss za nokia huzikuti platform yoyote ni zake mwenyewe labda hii here map ndo kaanza kuieka kwenye ios na mozilla so we muone tu nokia kachemsha ila time itatuambia.

Mkuu nakushauri tembelea nokia beta lab apps za nokia zinapopikwa nenda kaangalie unique talent wale jamaa hawaangalii jamii inapenda nini? Wanaangali tubuni nini jamii itapenda

HTC Vs Nokia (@Chief Mkwawa)
Chanzo cha graphs na tables zote ni (unless stated differently): Academic Mintel (Global Market Research in Europe, America and Asia| Consumer Trends | Product Innovation | Mintel), Mintel ni leading Market Research Company, ila unahitaji kuwa mwanachama ku-access data, research reports na insights. Ripoti niliyoitumia imetoka Mwezi wa Februari 2013. Kwa hiyo ni latest Data

Kabla kuanza hoja naomba niweke wazi kuwa lengo ni kuelimishana ili tufaidike sote. Natumai kupitia mijadala hii tutajenga mahusiano na mashirikiano mazuri.


Umiliki wa Simu (Idadi ya Wateja)
Refu.png


Nokia kwa sasa wanashikilia nafasi ya 2 na HTC wanashikilia nafasi ya 5 (tofauti na dhanayako kwamba HTC ni kampuni ndogo sana. Lakini cha msingi zaidi a ni kwamba kutoka mwaka 2011 kwenda 2012 market share ya Nokia imeshuka kwa 5% na ile ya HTC imepanda kwa 1%. Kwa hiyo unaweza kuona Nokia ndio wanaoelekea kuporomoka sio HTC. Lakini cha msingi zaidi ni kwamba kinachoifanya Nokia kuwa na idadi kubwa ya mauzo ni kule kutengeneza vimeo vingi vinavyotumia Symbian, Hivyo ukiangalia Strategy ya Nokia na Samsung inafanana wakati Strategy ya HTC ni tofauti kabisa ambapo wao wanatengeneza Smartphone tu, sio vimeo vya elfu Sh. 14,000. Ushahidi wa hili angali simu za bei rahisi zinazoongoza kwa mauzo UK ni hizi:

Screen Shot 2013-02-25 at 22.37.38.png

SOURCE: Pay As You Go Mobile Phones - The Carphone Warehouse

Kuhusu Hoja ya Windows Phone
Ni kweli kwamba Nokia ndio Market leader wa Windows Phone. Lakini ukweli ni kwamba Windows Phone bado ziko taabani (6% tu ya mauzo ya simu zote) yaani ni wa mwisho katika eco sysytem kubwa tena sio tu wa mwisho bali wamepitwa hata na kampuni inayo-struggle vibaya sana yaani Blackberry. Hivyo kwa sasa hata ingekuwa Nokia wanauza 100% ya Windows Phone zote basi bado ni share ndogo sana katika soko zima.
Struggling Windows Phone.jpg

Matumizi katika Ad Campaign
Screen Shot 2013-02-25 at 22.20.09.png

Nadhani utakuwa unafahamu umuhimu wa Branding. Ni kweli kwamba Nokia inashikilia nafasi ya nne kwa ujumla. Lakini angalia jinsi HTC ilivyoongeza Adspend kutoka 2008 - 2012, yaani kuna ongezeko la 1,598% wakati Nokia inaongoza wameshuka kwa 39%. Hii inaonyesha kuwa HTC wako serious katika masuala ya Branding, na Nokia ama wanacheza au hali ni ngumu inawalazimu wateremke chini, Ni LG tu ndio walioporomoka zaidi ya Nokia.



Hivyo HTC ni kampuni ambayo imefanya kosa kubwa la kujisahau walipokuwa market leaders enzi za Windows Mobile (market leaders in smartphone) lakini sio kampuni yenye uwezo mdogo au inayoporomoka kwa wakati huu.
Faida

HTC Net Profit After Tax (Q4 2012) $1 Billion - Q4 2012 (source HTC Financial Report)
Nokia Net Profit After Tax (Q4 2012) EUR 784 million (Source Nokia Financial Presentation)

Sasa hapa ndio unauona ukweli, kwamba pamoja na kuwa Nokia wanauza simu nyingi lakini wanawazuga investors/shareholders kwa vimeo ambavyo havina faida. Angalia HTC wanavyokwenda sambamba na Nokia katika faida. (784 Euro ni sawa na $ 1.024), kwa hiyo namba tano kwa mauzo na namba 2 wanatofautiana $0.024 bl tu katika faida!

Na kwa muelekeo unavyokwenda naamini Quarter hii Nokia watapitwa na HTC kwa profit. Hii ndio hali halisi kaka. Kama una-doubt any of the info/data/ basi sema naweza kukutumia source halisi.
Niwie radhi kwa urefu wa makala.
 

Attachments

  • Nokia inaporomoka .jpg
    Nokia inaporomoka .jpg
    21.9 KB · Views: 32
Kwa kuhusu hoja zako kwamba mwakani hatutokuwa na HTC naamini unaona wazi kuwa HTC is there to stay. Kuhusu apps sijui 1000 za Nokia kama nilivyosema mwanzo kuwa Nokia kushughulika na apps ni kupoteza muda, off course wanatakiwa wawe na apps kadhaa kwa ajili ya core service zao mfano google wana apps kama 50 na apple pia idadi kama hiyo halafu uwanja wamewaachia developers wafanye mambo yao.

Rational customer haweza kuchagua simu eti kwa sababu handset manufacturer ana apps 1000, lakini watu wanachagua simu (iPhone) kwa sababu platform ina apps 1,000,000 au Google kwa sababu android na apps 700,000. Na ndio maana kuna wakati Apple walikuwa na tangazo "There is an app for that"

Angalia jinsi Windows Phone ilivyo na ukame wa apps (150,000) tena Apps muhimu kama vile Hulu au Instagram hazipatikani kwenye WP. Kwa hiyo lets hope developers wataendelea kutoa apps lakini mwaka mzima wa 2012 WP imetoa apps mpya 75,000 ambapo Android na iOS hutoa idadi hiyo katika muda wa mwezi au chini ya hapo.

Kuhusu hoja kwamba WP inakua, ukweli ni kwamba wako mashakani kupoteza nafasi ya tatu kwa blackberry (hao BB wenyewe taabani) hivyo competitor wao sasa hivi ni BB sio Android wala iOS. Yaani platform yenye kampuni moja tu BB inakwenda sambamba na platform nzima yenye kampuni kadhaa (wote wana 6% market share by OS) hapo ndio unaweza kuona WP iko dhaifu kiasi gani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom