Hivi amoled display ni nini kwenye simu?

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Ukienda kununua simu utasikia simu hii feature kadhaa wa kadhaa ikiwa na display aina ya AMOLED !! Sasa iyo AMOLED display ni NINI ?

amoled ni moja wapo ya teknolojia ya kioo ambayo inasimama kwa jina la Active matrix organic light emitting diode ni moja wapo ya OLED Display ambayo inatumika kwenye simu mbalimbali za smartphone.

Teknolojia hii ilianza kutumika toka mwaka 2007 ambayo ilianza kutumika kwenye simu , media player , Tv , digital camera na inaendelea kufanya vyema

kutokana na kuweza kutumia low -power , na kutoa ubora wa hali ya juu kitu chochote kwenye taswira ya picha yani 8k resolution nk.

Amoled kimetengenezwa kwa teknolojia ambayo inamfanya mtumiaji hawe na furaha na kile anachokitazama kwani kinakuonyesha kila kitu kwenye taswira yenye ubora sana yani unaweza jihisi wewe uko humo pia.

Ukitumia kioo Cha AMOLED display macho yako yatakua salama juu ya mionzi ya simu dhidi yako, ivyo kumfanya mtumiaji kuweza kulindwa macho yake yasiweze kuathiliwa na mionzi yoyote.

Ubadilika kutokana mazingira ya mwanga ili kufanya macho kuweza kutizama kwa ufasaha zaidi pamoja na kutoa picha yenye mwanga mzuri pale unapotizama video , picha au unapocheza game.
Iyo ndo AMOLED display bhana ulikua unajua au ndo tunakujuza !!

Ebu tuambie ukienda kununua simu wewe huwa unatizama vitu gani ? Tuachie maoni yako !!!!

Teknolojia ni Yetu sote
 
Back
Top Bottom