HP kufungua kiwanda Tanzania

mkuu jk wenu alishafanya mazungumzo na don bill gates, ktk mazungumzo yao alimuomba aisaidie tz kujenga udom, alienda google ktk mazungumzo na madon aliwaomba waisaidie tz kuconnect shule za msingi kwa internet, kuisaidia computers and other devices na si kuanzisha google center tz. sasa hapa kwa data nilizokupa unaweza ukahisi mwenyewe mazungumzo yalihusu nini kama si kuomba msaada wa kutujengea barabara,zahanati etc
 
Ni ndiyo za alinacha, jamaa wa HP wanajua kuwa jamaa anapenda publicity za ku pose na ma CEOs wa multinationals kama hizi so wakamua tu kumsanifu. Wazungu walisema 'If wishes were horses even beggars would ride'.
Economic indicators zote ziko prohibitive ku-invest Tanzania at least kwa miaka hii ya JK. Angalia nchi haina reliable source of eneergy, tax regime iko very discouraging, inlation iko around 20 pc, per capita income ni chini ya dola 500 kwa mwaka. Miundo mbinu ya barabara ni the worst ktk continent.
Kilichopo hapa ni biashara za wakinga na wachaga tu kwenda Gwangzou na Hongkong kufunga mzigo na kuleta Kariakoo. Forget about swing serious Foreign Direct Investment ya calible ya HP, IBM etc
 
zing, unachobisha nikipi, nadhani hujui wat hapened ths week in south africa. It was an economic forum ambayo makampuni mbalimbali na nchi zote duniani walikutana na kujadili njia za kukuza uchumi wa nchi zao. And thats were jk aka meet na uongozi wa HP na kumpa mkakati wao wakutaka kupanua zaidi wigo wa kampuni yao mpaka tanzania na kufanya tanzania kuwa base ya products zao kwa kufungua kiwanda cha kuzalisha bidhaa zao hapa na spare parts zake.

Na hii plan sio kama Jk ameomba, wao ndio wametoa hyo proposa na jk amewakaribisha.

Realm Kama mwana IT napenda kuona HP, IBM Acer Tshiba japo wanakuwa na service center zao Tanzania badala ya kutimia third party. Hii habari uliyoleta ya Kiwanda inapendeza masikioni na nihibari tunazotaka kusikia lakini kama walivyochangia wadau . Kiiwanda hawawezi hata service center tu ni kazi.

  • Mazingira hayo hayapo hapa kwetu mfano una jamaa kagusi ni umeme.... Nitashangaa sana nikiiona hii habari kwenye magazeti sababu JK atakuwa anazidi kuabika.

  • Elewa wenzetu kampuni zao hawafanyi decision za ksiasa. strategic decison zao wanfanya baada ya kuridhika na mambo mengi. Hawa Sio richmond kwa hiyo hawawezi kuja. Hizo ni story kama za kwenye kahawa. but uombe uzima may be by 2020 watakuwa wameshapata site/eneo la kuwekeza tanzania
 
@ zing,
Kwanza thanx 4 ur understanding, pili kufungua kiwanda hapa tz inawezekana japo ita take tme. So ts a plan haijajulikana lini dats
 
zing, unachobisha nikipi, nadhani hujui wat hapened ths week in south africa. It was an economic forum ambayo makampuni mbalimbali na nchi zote duniani walikutana na kujadili njia za kukuza uchumi wa nchi zao. And thats were jk aka meet na uongozi wa HP na kumpa mkakati wao wakutaka kupanua zaidi wigo wa kampuni yao mpaka tanzania na kufanya tanzania kuwa base ya products zao kwa kufungua kiwanda cha kuzalisha bidhaa zao hapa na spare parts zake.

Na hii plan sio kama Jk ameomba, wao ndio wametoa hyo proposa na jk amewakaribisha.

...Ili hoja yako iwe na mashiko, toa sababu au misingi ya kiuchumi na soko ambayo itawafanya wawekeze hapa.

...Otherwise ni wishful thinking!
 
Acha kudanganya umma wewe! Yaani HP watoe plan ya kufungua kiwanda halafu kusiwe na habari sehemu yoyote kwenye mtandao?
Ufungue kiwanda nchi haina hata umeme wa uhakika, hao HP wamedata?
Mgao ndio huo umeshatangazwa tena
 
Siyo rahisi kufungua viwanda huku kwasababu wamagharibi hawana tabia yakuwekeza huku kwetu kwenye mambo ya tekinolojia wao huja kuchukua malighafi tuu.

Pia ieleweke wao bado wanahulka za kuiona Afrika bara la giza kwahiyo hawawezi kuleta makampuni yao ili yatoe ajira. Kama tungekuwa na viongozi mahiri ambao wangesimamia maslahi yetu na kujenga viwanda ungewaona wakijipendekeza huku kwetu (kama wanavyofanya Brazil na China) kwasababu ya kuogopa ushindani lakini kwasasa sahau tuu.

Jamani maendeleo tutaleta wenyewe haya mambo ya kupapatia makampuni ya watu eti watujengee kwetu ni hadithi za alinacha tuu.
 
:bange:Wengi wanaobisha inaonekana sio wafuatiliaji wa habari,so ni kuwaacha kama walivyo wamezoea u-thomas.
 
Nafikiri watafungua magodown kama distribution center, kama ilivyo Gilbratar kwa toyota
 
Hicho kwanda kitakuwa kinatengeza nini Power adaptor za HP au ni kiwanda cha ku reclycle cha HP.
Je wametaja timing ya kufungua hiki kiwanda ni kati ya mwaka gani na mwaka gani? Au ni objectives without plan

Nafikiri watafungua magodown kama distribution center, kama ilivyo Gilbratar kwa toyota

hata distribution center ni ngumu sababu usafiri wetu wa anga na logistic na conection zake hata within africa ni mgumu. Dar Airport sio the Hub. Na distribution center mara nyingi iko mji ambao ni hub.

Kenya na south africa maybe na ethiopia ziko kwenye better position kuwa ditribution as far as africa is concerned. Unless tunaongelea siasa na kutaka kujiliwaza watanzania tuna kazi kubwa ya kufanya kuvutia wawekezaji wa kweli. La sivyo zaidi ya madini tutaendelea kuwapata kina RICHMOND tu
 
Hayo maongezi yalikua rasmi au ni porojo za kupitisha muda wakati wa chai? Kuna mambo watu wanaongea wakati wa chai ili kupitisha muda tu. Kwa umeme huu wa mgao haingii akilini kabisa kua HP watashawishiwa kuweka kiwanda chao hapa.

Wazungu wasivyojua kutofautisha waafrika, pengine walidhani Kikwete ni waziri wa South Africa....

Na tungojee hilo likiwanda...
 
Alikua anauza chai za kijivua magamba kwa wale wafuasi wenye mawazo magando na wavivu wa kufikiri. Nchi yenyewe umeme mgao!!!!!!!!!!
 
Kenya ndipo yalipo makao makuu ya HP kwa nchi za Africa mashariki na kati, mauzo ya computer za HP Tanzania ni madogo sana ukilingalisha na mauzo ya hp Kenya na Uganda.
 
Kenya ndipo yalipo makao makuu ya HP kwa nchi za Africa mashariki na kati, mauzo ya computer za HP Tanzania ni madogo sana ukilingalisha na mauzo ya hp Kenya na Uganda.

Unakumbuka kuwa mwaka 2006 alipokuwa transit kwenye safari ya kwenda Cuba pale Madrid alipata nafasi ya kutembelea kwenye makao makuu ya Real Madrid. Baada ya maongezi akasema kuwa Real Madrid FC ingetembelea kufanya michezo ya kirafiki na SSC na Yanga ifikapo Julai 2006.

Wakati huo Real Madrid ilikuwa na vichw vinne bei mbaya yaani Beckam, Zidane, Raul na Roberto Carlos, je muliwaona wakija TZ?
 
Nadhani kawaomba waje kuwekeza ktk kiwanda cha kutengeneza Mabox ya kupekia kompyuta na printa zao au kawaomba msaada SIPIYU kwa ajili ya shule za msingi.
 
Back
Top Bottom