How i can be rescued!!!help pls | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

How i can be rescued!!!help pls

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by sixlove, Mar 17, 2012.

 1. sixlove

  sixlove Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 13
  Habarini za maisha kwa ujumla. Hivi karibuni nilipokea ujumbe kutoka kwa mtu fulani akihitaji tuwe marafiki kupitia facebook, sikusita kumkubalia kwani ndivyo urafiki unavyoenea. Siku zikaendelea huku tukiendelea kuwasiliana kupitia e-mail, ndipo siku moja alinitumia email akidai yeye ni mkimbizi na sasa anaishi dakar- senegal kwenye kambi ya wakimbizi, hivyo basi anahitaji kupata partiner ili imsaidie kupata viza za kuja bongo: Kabla sijamjibu akatuma nyingine akidai marehemu baba yake aliweka kiasi fulani cha fedha kwenye akaunti yake kabla hajafa, hivyo aliniomba nimsaidie kufanya transaction kutoka kwenye hiyo benk kwenda kwenye akaunti yangu. Alinitumia anuani za benki kisha akanitaka niwasiliane nao ili wajue kuwa tupo serious na suala hilo. Nilifanya hivyo, kisha bank walitumia email wakitaka niwatumie taarifa zangu, zikiwemo anuani zangu,account no, pamoja na kitambulisho. Nikaingia mkenge nikatuma.

  Kama ilivyo sema usikike, nikampa story msela wangu mmoja, si ndo akanifumbua macho. Akaniambia kuwa huyo mtu ni miongoni mwa watu wezi duniani wanaojulikana kama,,"scammers" hivyo niachane naye. Niliachana nae,


  wanajamvi naomba mnisaidie, nitawaepuka vp watu hawa ukizingatia, wana tarifa zangu zote kikiwemo kitambulisho changu. Nifanye nini?

  1.nifunge akaunti zangu, je itasaidia?  Ushauri wa kina unahitajika.....
   
 2. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  si ubadilishe account,nenda bank waambie tatizo lako,wafunge account ya zamani ufungue mpya......wengi wanataka details wafanye ' identity fraud' siijui kiundani ila sidhani thats is what happened in your case....
   
 3. mgeni10

  mgeni10 JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,112
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Achana nae tu hawezi kuiba wala kuchukua hela yako Bank. tu mwisho wake wangesema utume hela kulipia gharama za kusafirishia hizo hela , ukituma UMELIWA.

  LA MSINGI UNATAKIWA KUFAHAMU KWAMBA KWENYE MAISHA HAKUNA NJIA ZA MKATO
  (Kilichokuchanganya ni hiyo amount aliyokutajia)
   
 4. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2012
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Pole sana! Jitahidi kufanya kazi kwa bidii utatoka tu mkuu!
   
 5. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,129
  Likes Received: 943
  Trophy Points: 280
  Namna nzuri ya kujitoa ni kpuuzia e-mail zake kuanzia sasa hivi. Usiwasiliane naye tena! Habari ulizompa kuhusu akaunti na nyinginezo hatoweza kuzitumia kukuangamiza! Nia yake ni kukutafunia hela kwa kukueleza kuwa kutuma hela kwako inahitaji fedha kadhaa na kukuomba kutuma hicho kiasi.Hivi ndivyo hawa matapeli wa Afrika Magharibi wanavyoliza watu!
   
 6. d

  dandabo JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 303
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Acha kumpotosha mwenzio! Kama akaunti yake inahela akaziondoe fasta la sivyo imekula kwake na uifunge tu hiyo akaunti maana ukiweka tu salio la kueleweka ujue limeenda hilo! Dont try that again
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  kupenda vya dezo jamani.
  Ni lini watanzania tutaamka? Kuna mmoja aliambiwa kashinda mil 3 za Kenya akataka kwenda kutuma details zake.

  Nikamwuliza ulishiriki, akasema hapana.
  Hivi waweza shinda bila kushiriki kitu?
   
Loading...