Houth wa Yemen yapiga Kusini ya Israel. Na wao wakatiwa intaneti

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,183
10,917
Hapo jana wanamgambo wa Houth wa Yemen kwa mara nyengine walifanya mashambulizi ya kuvizia kusini mwa Israel kwenye mji wa bandari wa Eliat.

Tofauti na mashambulio ya awali ambayo yaliweza kusitishwa angani moja na israel yenyewe na jengine na kibaraka wao Saudia.Shambulio la hapo jana lilifika lilipokusudiwa bila kuonekana na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye jengo moja mjini humo.

Kilichofuatia usiku ni kupunguzwa kwa kasi ya mawasiliano ya intanent ya kampuni ya TeleYemen ambayo hupokea mawasiliano kutoka mkonga wa baharini unaoendeshwa na kampuni ya GCX.

Shambulio hili la kuvizia kwa droni ni utekelezaji wa ahadi ya kiongozi wa kundi hilo ya kupiga maeneo yenye maslahi ya Marekani na Israel mpaka hapo watakapositisha vita dhidi ya Palestina vinavyoendelea huko Gaza.

Hilo ni shambulio lao la pili lililofanikiwa baada ya hapo juzu kuidondosha baharini droni ya Marekani ya muundo wa MQ-9 Reaper.
 
una kazi yoyote mjini au maana akili hizi ungezitumia kutaftia pesa ungesaidika sana,mambo ya israel,yemen ,gaza yanakusaidia nini wewe
 
una kazi yoyote mjini au maana akili hizi ungezitumia kutaftia pesa ungesaidika sana,mambo ya israel,yemen ,gaza yanakusaidia nini wewe
Afadhali mimi kuliko ile kazi unayofanya wewe kuwafurahisha mayahudi wanopenda ile kitu
 
Back
Top Bottom