Hotuba za Rais Samia hufuatiliwa sana na Watanzania

Screenshot_20230626-101500_(1).png
 
Lucas mwashambwa kwani ukisema tu ukweli utanyimwa ugali?

Hata kwa hari ya kawaida tu, huoni clip za Magufuli ndo zinatembea kuliko za mama SA100?

Nani sasa atafuatilia wakati maagizo yake ni kama anacheza filam yaani watendaji hawayachukulii uzito?

Kiufupi, watu hawamuelewi. Bora aongee Msukuma Bungeni kuliko Mama ikulu.
 
Lucas mwashambwa kwani ukisema tu ukweli utanyimwa ugali?

Hata kwa hari ya kawaida tu, huoni clip za Magufuli ndo zinatembea kuliko za mama SA100?

Nani sasa atafuatilia wakati maagizo yake ni kama anacheza filam yaani watendaji hawayachukulii uzito?

Kiufupi, watu hawamuelewi. Bora aongee Msukuma Bungeni kuliko Mama ikulu.
Maagizo yapi ya mh Rais wetu ambayo hayajafanyiwa kazi na watendaji wa chini?
 
NISAIDIE KUPATA MCHONGO
Nina degree ya
COMMUNITY ECONOMIC DEVELOPMENT.
Naitafutia uzoefu ili badae niweze kuwa na chochote kwenye CV na kuombea Kazi.
Nisaidie hata Internship tu.
Location :KIGOMA ila kokote kama kuna uhakika mimi nitafika.
Msaada waungwana, mniinue
Taasisi
Social Work
Mashirika(NGOS)
kokote kule aisee
0628849189
 
Rais pekee aliekuwa anafatiliwa na wat na kusikilizwa ni JPM. Huyu wasasa hata akitoa hotuba huwa naona post kuwa kasema hiki au kile. Niliangalia hotuba yake alipoenda kawe na kusema "tunachanja au hatuchanji" nikaona niendelee na majukumu yangu. Sijawahi fatilia na mtaani kachokwa mapema na watu wanasema haongozi yeye ila washauri wake. Au niache maana mleta mada umeamusha hisia ingawa najua hata wewe baada ya miezi usipoangalia jina la mleta mada unaweza kumtukana, kumbe umepost mwenyewe
 
Ana hotuba moja hivi za faraja za kujenga na zakutupa matumaini ss wananchi...kusema ukweli akiongea Jambo huwa linafanyika bila danadana yyte. Abarikiwe Sana na MUNGU,
Hakika Mungu ambariki Sana Rais wetu na kumpatia maisha marefu yenye heri na Amani.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hotuba za Rais Samia Hufuatiliwa Sana na mamillion ya watanzania,wengi Sana husitisha shughuli zao pale wanapofahamu siku fulani na muda fulani atakuwa mahali fulani kwa ajili ya kushiriki tukio fulani na atapata nafasi ya kutoa hotuba yake. Hii Ni kutokana na watanzania kutambua ukweli kuwa Rais Samia Ni kiongozi mkweli Sana,Ni kiongozi mwenye hofu ya Mwenyezi MUNGU,Ni kiongozi mcha Mungu ambaye wakati wote huzungumza ukweli awapo mbele ya hadhira bila kujari watu watapokeaje hotuba yake.

Ni kiongozi ambaye huwa hazungumzi ili kuwafurahisha watu,bali huzungumza ukweli ili watu wajuwe na wawe na nafasi ya kujuwa muelekeo wake na mtizamo wake au hatua ambazo anatarajia kuchukua juu ya Jambo fulani kisera au kisheria au kibajeti au kupitisha Jambo fulani au kuondoa Jambo fulani. Ni kiongozi ambaye kwake nyeupe Ni nyeupe na nyeusi Ni nyeusi na chafu Ni chafu na Safi Ni Safi yaani huusema na kuutamka ukweli bila hofu Wala wasiwasi ya kumkwaza mtu.

Ndio maana kunapotokea taharuki ya Jambo fulani katika Taifa letu mamilioni ya watanzania huwa na shauku kubwa Sana ya kutaka kupata Neno kutoka kwa Rais,utasikia ukipita mitaani watu wakisema tuna Imani na tunamwamini mama yetu na hawezi kutuangusha na atakuja kusema neno na mioyo yetu itatulia na kukunjuka.

Watanzania wanafahamu na wanamfahamu mama yetu na Rais wetu kuwa Ni mama , kiongozi na Rais wa ulimi mmoja na siyo ndimi mbili,Ni kiongozi aliyejijengea heshima kubwa Sana katika hili ndani na nje ya Taifa letu.jambo hili limemfanya kuaminika,kupendwa , kuungwa mkono,kusikilizwa na kufuatiliwa Sana na watanzania hotuba zake pale anaposimama kuongea sehemu yoyote Ile katika mipaka ya Tanzania na nje ya mipaka ya Taifa letu.

Ndio sababu wakati wote watanzania wanatamani kumsikia Rais akizungumza juu ya Mambo makubwa yanayokuwa yanaleta Taharuki na mgawanyiko ndani ya jamii,sauti na Neno la Rais Samia huleta matumaini, Tabasamu na faraja katika mioyo ya watanzania, sauti na maneno yake huleta utulivu ndani ya Taifa,huleta mshikamano na umoja wa kitaifa,huzima upotoshaji na kuwaacha wapotoshaji wamejawa na aibu katika nyuso zao.

Ndio maana hata alipokuwa jijini Arusha tuliona shauku ya watanzania wakisema Sema mama yetu,.Katika hili napenda kusema ya kuwa Rais Samia amepata kibali kikubwa Sana kutoka kwa Mwenyezi MUNGU Cha kukubalika mbele za watu,anaaaminika kuwa kiongozi mwenye uzalendo mkubwa Sana na mwenye uadilifu mkubwa usiotiliwa mashaka na mtu yeyote yule ndani ya Taifa letu.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.



Sikujua kwamba Mimi sio Mtanzania, huwa nilikuwa nikifanya kazi nikiona hotuba naacha kila kitu, namsikiliza, sasa hivi nikiona hotuba yake wakati nafanya kazi, nabadili kwenda trace Music
 
Back
Top Bottom