Hotuba ya Rais Kikwete Sept 30, 2012

Hotuba ya Rais Kikwete Sept 30, 2012

Huyu jamaa nchi ilishamshinda,kwa kifupi sijawahi kuona Rais "rahisi" kiasi hiki
 
Dr. Slaa alisema kwamba huyu jamaa ni janga la kitaifa. Ukweli unaendelea kudhihirika kadri siku zinavyosonga mbele.
 
Keshawasafisha polisi,na yeye ni amiri jeshi mkuu.Kamati ya Nchimbi haina maana na ni upotevu wa pesa za wananchi.

Pili, since hajaonyesha kuwa neutral, ni wazi ni kama ameingilia kazi ya kamati hiyo.

Mwisho, kuna pahala nimesoma akisema kwamba askari aliyuwa tayari keshafikishwa mahakamani, na akasema tu wasiwe wanatumia nguvu za ziada,sasa tutegemee kamati iseme tofauti na yeye?

Kweli rais huyu ni janga la Taifa, na hii miaka iliyobaki hadi 2015 ni mingi sana kwa mwendo huu! Kiukweli ni kama ameilaumu chadema. Kumbe yale yanayozungumzwa humu na kina zomba ndo vile na yeye anaamini? Ukimya wake ulikuwa una walakini.

Ama kweli mh rais ana roho kutu!

kwakua upeo wako wakufikiri hapo ndipo ulipoishia huna sababu yakulaumiwa
 
Last edited by a moderator:
Toeni tamko basi,tatizo la CDM mnapenda kudandia issue na kuzifanya kuwa agenda ya chama chenu.Mwangosi alishakufa amezikwa sasa mnataka JK afanye nini au yeye ndie aliemtuma akafanye kazi za chama?
 
Toeni tamko basi,tatizo la CDM mnapenda kudandia issue na kuzifanya kuwa agenda ya chama chenu.Mwangosi alishakufa amezikwa sasa mnataka JK afanye nini au yeye ndie aliemtuma akafanye kazi za chama?
Maneno yenu humu ndani siyadharau kabisa kwasababu ndivyo JK anavyoona, hata hotuba yake maneno yamefanana sana na haya yenu humu ndani,pengine nyie ni watu wake wa karibu sana,ama pengine anaweza akawa na id humu maana kwa jinsi alivyo,hilo linawezekana,tena jinsi mna chuki na Slaa,inawezekana ni yeye mlimkosakosa ile siku.

JK awe makini akiondoka madarakani,aombe Mungu upinzani wasichukuwe,ama hata ikiwa ni ccm,basi iwe ccm ya watu wake ndo ichukuwe nchi,la sivyo,inawezekana akatakiwa kujibu mambo mengi sana.
 
Niliposikia kamanda Kamuhanda anatamba redioni kuwa hawezi kujiuzulu kutokana na tukio la kuuawa kwa Mwangosi, ingawa inajulikana wazi kuwa yeye ndiye alisimamia kikamilifu 'OPERESHENI UA MWANGOSI' basi tafsiri ya moja kwa moja tuliyopata wananchi ni kuwa, kamanda Kamuhanda alisimamia zoezi lille la mauaji kwa maagizo ya mkuu wa nchi. Naungana mkono na wote walliosema kuwa, kutokana na hotuba hiyo ya Rais, hakuna sababu ya kuendelea kupoteza hela za walipa kodi, kwa zike Tume za Nchimbi na ile ya IGP kuendelea na ile kazi waliyopewa, kwa kuwa haitawezekana wao watoe taarifa ya kupingana na maelezo ya Mkuu wao wa nchi. Nadhani kwa sasa, hatua peke yake iliyobaki ni kwa wanasheria wanaharakati, kuangalia namna gani suala hili linaweza kufikishwa ICC. Kwa kuwa hata yule polisi corporal aliyefikishwa mahakamani, naye wakati wowote ule, anaweza akaachiwa huru. Inawezekana pia hata wale polisi waliokuwa wakimkinga asipigwe picha, wakati anapelekwa mahakamani, yakawa yalikuwa maagizo ya JK mwenyewe!!!
 
Dr. Slaa alisema kwamba huyu jamaa ni janga la kitaifa. Ukweli unaendelea kudhihirika kadri siku zinavyosonga mbele.

Mimi naona huyu Daktari wa Kanoni Slaa ndiye janga la Taifa kuanzia maadili mpaka utendaji, kuna tuhuma zake nyingi hata ndani ya chama chenu msome TUNTEMEKE utaelewa, halafu jiulize kwanini CCM walimkataa huyu? kuna siku utakuja jionea.
 
Last edited by a moderator:
kiongozi wa nchi anawasifia wazungu kupitiliza, speach yake karibu yote ni kutulainisha tuone ardhi yetu sii mali kama hatutawapa wawekezaji wakubwa wa kilimo na uzalishaji wa mbegu, anayalenga makampuni ya kizungu!!! Huyu mtu ni hatari kwa taifa letu. Hana nafasi ya kuyaongelea ya taifa letu, anasuka dili tukishtuka hatuna ardhi.
Huyu bwana ni habari mbaya!!!!!
 
Hotuba zake zilishakosa tija long time...hakuna tofauti akiongea na asivyoongea.
 
Kunatakiwa kuwepo maandamano ya kutokuwa na imani na rais.

Sasa wewe kili siku unalalamika tu humu JF, kama kweli una uchungu na nchi anzisha maandamano ya kumpinga rais sio kubweka JF huku umejificha nyuma ya Laptop.
 
Wakuu hiyo hotuba ilikuwa imeandikwa au alikuwa anatoa kichwani?coz ni kisummarise yote mliyoandika hapa hata robo page haifiki!ndiyo hotuba ya miezi miwili?Twifwileeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee:crying:
 
Mkulu hakutakiwa awe rais,hilo siyo siri.Rais gani anafanya na kuongea ujinga kama hivi.

Kwanza mwanzoni alitakiwa ayalaani yale mauwaji,awape pole wafiwa.Atoe onyo kuwa matumizi ya nguvu hayatakiwi especially kwa wananchi wasiokuwa na silaha.

Halafu labda aseme wataangalia kuhusu training ya maofisa wa polisi kuhakikisha kuwa wako well equiped kulinda amani na si kufanya mauwaji.

Yeye amesema eti polis hao hawana tofauti na polisi wengine duaniani.Binafsi sijawahi kuona hayo ya polisi kulipuwa wananchi.Na hata ya kuwapiga risasi,huwa hayatokei kwenye shughuli za kisiasa.NI mambo ya crimes etc.

Pia yeye kama rais,ameshindwa kumwajibisha yule kamanda?Mkuu wa polisi wa mkoa?Huyu mtu ni janga kubwa kabisa kwa taifa.

Kama hakutakiwa kuwa rais si ukamtoe madarakani au unaogopa polisi? Zaidi ya hapo endelea kubweka tu humu JF unadhani watanzania wote wana akili kama zako.
 
Washauri wake wamemshauri vibaya, bei ya mchele, sukari n.k ziko vile vile tangu aingie madarakani.
 
Tukumbuke maneno ya Sumaye mwaka 2005, aliposema kiongozi anayetaka kuingia Ikulu, kwa kutumia vyombo vya habari kuwachafua wengine, atakapopata madaraka, atatumia risasi kudumu madarakani!!

Tuliyoshuhudia Arusha mwaka jana na hivi karibuni Msamvu-Morogoro na Nyololo-Iringa, ni utimilifu kamili wa utabiri wa waziri mkuu huyo mstaafu. Kwa maana hiyo wa-TZ tushinikize Tume zilizoundwa na IGP Mwema na waziri wa mambo ya ndani, Nchimbi zivunjwe, ili zisiendelee kufuja pesa za walipa kodi.

Kwa kuwa hakuna uwezekano Tume hizo zikaja na taarifa zitakazokwenda kinyume na msimamo wa Rais wa nchi!! Babala yake wanasheria wanaharakati wazalendo, waagalie vifungu vya sheria vitakavyotuwezesha kama Taifa, kuwafikisha wauaji wa raia wasio na hatia kwenye mahakama ya kimataifa, the Hague!!
 
Back
Top Bottom