Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012


I am tempted to agree with you my friedn, save the highlighted text.
 
Kadriki ya taaluma yao na kiapo chao cha kazi wangetakiwa kufunguliwa mashtaka, ila tu serikali ina huruma.

Kiapo cha kazi hakiwahusu madaktari tu bali hata Rais na Serikali yake yote naye waliapa kwamba watatetea na kuyalinda maslahi ya Tanzania na Watanzania. Kama utakumbuka aliahidi kupitia tena mikataba ya uchimbaji wa dhahabu ambayo Watanzania wengi tumelalamika kwamba kinachofanyika ni wizi wa mchana maana dhahabu haina manufaa yoyote katika nchi yetu. Je unadhani msanii Kikwete na Serikali yake anafuata kiapo cha kazi yake kama kiongozi wa nchi katika kutetea na kulinda maslahi ya nchi?
 
Unda kundi la kipinzani liite Lord resistance army, wapelekee hao madikteta wa ulaya waliofanikiwa, watakupa pesa nzuri sana; utamuondoa JK haraka sana na utampeleka hague...OK..

Fanya hivyo mkuu

Ni mara chache sana kupata watu wenye sifa kama hii yako. Watu wengi duniani hawapendi kuonekana haziwatoshi hata kama ni kwa kuigiza. Ndo maana filmu za "Nazi" zinapotengenezwa nafasi ya "kapo" hulipwa pesa nyingi maana ni ya kujitoa muhanga.

wewe naona unacheza nafasi hiyo bila hata malipo. Zinakutosha? au wewe ni "kapo" wa kudumu
 

Kiapo cha dactari kazini na kiapo cha mwalimu shuleni ni tofauti, kwani huyu daktari anachzea uhai wa binadamu.
 
Budget ya kununua V8, maonyesho ya nane nane, na posho za safari.
 

Madaktari wenyewe ndio mnaomuandalia za kupita bila kumuonyesha hali halisi. Pale Muhimbili kwenyewe walimpitisha maeneo yenye vifaa vya dharura vya kisasa na kuficha hali halisi.
 

Tukipanua wigo wa majadiliano tutashtukia tuametoka nje ya mada tunayajadili. Kwa sasa mada ni kuhusu madaktari kurudi kazini au kuacha kazi na wende kutafuta ajira sehemu nyingine ambazo wataona watalipwa kadiri ya matakwa yao. Kwani kwa sasa uwezo wa serikali umeishia hapo na kwamba madai yao ni nje ya bajeti iliyopitishwa na bunge kuwalipa. Serikali ikikopa pesa kwa ajili ya madaktari wabunge wataikosoa kwa kufanya mambo kinyume cha system.

Haya ya madini tafadhali fungua mada nyingine tutaijadili, kuiingiza hapa kunaleta mgongano wa kujadili mada. Tutulie katika mada moja ili kupata hitimisho ndio utaratibu wa debate.
 
Speech ya Rais imeeleweka vizuri kabisa, Ni moja kati ya speechnzuri inayofafanua historia ya tatizo, nafasi ya serikali kwa sasa, options na solution.....I mean imeeleweka vizuri....Is a matter of choice kuna mambo ambayo serikali imeyakataa kuwa haiyawezi na kuna mengine imeyakubali na ameweka bayana asiyeyakubali halazimishwi bali aondoke kwa hiyari yake mwenyewe...
 
Kiapo cha dactari kazini na kiapo cha mwalimu shuleni ni tofauti, kwani huyu daktari anachzea uhai wa binadamu.


Kiapo ni kiapo tu , na kiapo cha Rais ambaye anaiangamiza nchi hukioni? kwa utendaji finyu na kuziacha rasilimali za nchi zikikwapuliwa na wajanja wachache? Hakuna Watanzania wanaokufa kwa kushindwa gharama mbali mbali za maisha ikiwemo ukosefu wa lishe, matibabu kama vile hospitali kutokuwa na madawa au vitendea kazi ambavyo vingeweza kabisa kuokoa maisha ya Watanzania maelfu kwa maelfi katika kila kona ya nchi?

Acha undumilakuwili wa kutaka kuwalaumu madaktari na wakati huo huo kutaka kumfagilia DHAIFU ambaye ndio chanzo cha matatizo yetu chungu nzima.
 

Ndio maana nchi kama Marekani dactari akigoma na kusababisha madhara kwa mgonjwa anafunguliwa mashtaka, na kama mgonjwa akifa anafunguliwa kesi ya mauaji first or second degree murder. Lakin mfanyakazi mwingine wa sekta nyingine atakachofanyiwa ni kufukuzwa tu kazini. Je umeona tofauti ya viapo hivyo vya kazini kwa watumishi.

Kabla ya ajira kuna mkataba ambao unasaini, iwe nchi za Ulaya, Marekani na hapa Tanzania, na kila aina ya kazi ina mikataba yake, huwezi kufananisha mkataba wa daktari wa binadamu na mkulima au mwalimu.
 

Unanichekesha kweli!! lol! unadai Serikali haina uwezo wa kuwalipa madaktari lakini hutaki kuangalia vyanzo mbali mbali vya pesa za kuwezesha Serikali kuongeza ukusanyaji wa pesa ili kukidhi matakwa ya madaktari katika ombi lao la kutaka kulipwa ujira mzuri!!! Nchi ina utajiri mkubwa sana lakini wananchi wake walio wengi ni maskini wa kutupa! Nchi ina wanachi wanaokaribia milioni 45 lakini kwa takwimu za TRA wanaolipa kodi ni wanachi lakini 6 tu!!! halafu unataka tusijadili hili la Serikali DHAIFU kushindwa kuongeza makusanyo ya kodi, na royalties za madini yetu ili kuongeza uwezo wake wa kuboresha hali za maisha ya Watanzania....Hoja yako DHAIFU.

 

Na Rais DHAIFU je ambaye anaachia Utajiri wa nchi unakwapuliwa huku akiwa aliapa kwamba atatetea na kulinda maslahi ya nchi na kisha kujipiga kifua kwamba Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana? Hoja zako za kujaribu kumfagilia DHAIFU ni DHAIFU.
 

Dai la kupinga nyongeza ya madai ya wabunge ni tofauti na hili la madaktari? Pengine wabunge lilikuwa na hoja kwamba wao ni muda mfupi na hawana mafao zaidi baada ya kuacha ubunge kuliko hawa madaktari ambao taaluma yao ni ya maisha. Wabunge tulivimbisha iishipa usoni, lakini la madatari tunanywea hii imekaaje?
 
Sakata la dk.ulimboka nadhani serikali ina agenda ya siri na wanyekyusa, walitaka kumuua dk.mwakyembe na sasa wamehamia kwa dk.ulimboka, rais kikwete usikanyage mbeya tutakuvurumishia mawe kama tulivyowahi kufanya.
 
""Kama kuna mtu wa Serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake binafsi na siyo za Serikali au kwa kutumwa na Serikali."""

Aisee..kwa hiyo kama JK/PINDA ameagiza kama JK/PINDA ana sababu zake binafsi?.
Hapa DHAIFU amesound kama anamjua vile aliyefanya hiki kitu.
 
Naona unajikanyaga kanyaga tu eti Serikali haina uwezo wa kuwalipa madaktari mishahara waliyoiomba. Hivi umefanya tathmini ipi iliyokuwezesha kutoa hitimisho kwamba Serikali haina uwezo wa kuwalipa madaktari mishahara ya sh 3.5 millioni kwa mwezi?
 

Let's do professional debate. udhaifu wa raisi upo jukwaa lingine na hapa tunajadili suala la madaktari kusitisha migomo na kuingia kazini, la sivyo waondoke na kwenda huko wanakofikiria watapata madai yao. Hili la udhaifu wa rais ni mada nyingine inayojadiliwa katika jukwaa hili, tusichanganye sukari na mchanga.

Tunapojadili mada tunatakiwa kuweka kando kwanza hisia binafsi dhidi ya mtu au kikundi, ila tujadili hali halisi ya tukio la sasa na athari zake kwa umma. Vinginevyo tunapopanua wigo tunatoka nje ya wigo wa masumbwi na kwenda kuwarushia masumbwi wasio ulingoni.
 

Wakuu sentensi hii niliyowekea red ni kwamba rais anakubali kuwa ni watu dani ya serikali wamefanya unyama huo halafu anawakana, yaani anaiepusha serikali kuwa si kazi yake, ila ni kazi ya mtu ndani ya serikali?

Au ana maana kuwa ni mahakama ndio imefanya hivyo?

Siwezi kuamini kama kweli rais alisoma hiyo, kama kuna mtu alimwandikia rais hotuba hiyo anatakaiwa kukatwa kichwa. You can not send people to kill and then you abandon them.
 

Sio sahihi kuwafananisha madaktari wa nchi kama marekani na hawa wa bongo ingawa wanakula kiapo cha kazi yao sawa. Malipo ya madaktari wa marekani ni mara mia ya hawa wa bongo na ndio maana hawawezi kugoma kwani wanavitendea kazi vinavyohitajika na malipo yao yanaendana na kazi wanazofanya; na kwavile wanalipwa vizuri na wanavitendea kazi stahiki ndio maana wanawajibika kwa makosa yeyote wanayoweza kumfanyia mgonjwa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…