Hotuba ya Polepole kwa lugha yetu huku mtaani

Kusini pride

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
1,762
Reaction score
4,070
Uchambuzi wa hotuba ya mheshimiwa Polepole kwa lugha inayoweza kueleweka huku uswahilini kirahisi.

Kwa ufupi, Polepole amelalamika kuwa utaratibu wa familia wa kula pilau pamoja kwenye sinia moja kwa ustaarabu na maadili umeharibiwa; ameshutumu utaratibu wa zamu na ratiba za wapishi kupuuzwa na wapakuaji wa nyama kugawa kwa upendeleo. Kwa maoni yake, anapowatazama wana familia wakinyang’anyana nyama kwenye sinia anaiona nyumba ni kama haina mwenyewe.

Maoni kuhusu hotuba yake: Tukizingatia kuwa alikuwa ni mmoja wa wapishi, inawezekana anayoyasema ni ukweli.

Mapungufu ya hotuba yake: Hotuba ilijielekeza kwa wana familia wachache ambao huchuchumaa kulizunguka sinia peke yao; haikugusia ubaya wa kuwaweka baadhi ya wanafamilia nje ya uzio wa sinia pamoja na kwamba huwa wanatozwa michango ya kununulia nyama na mchele kila siku.
 
Mzee wq ubwabwa ataelewa?
 
Back
Top Bottom