Hotuba ya kukumbukwa ya Marehemu Regia Mtema Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya kukumbukwa ya Marehemu Regia Mtema Bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paparazi Muwazi, Jan 18, 2012.

 1. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  MHE. REGIA E. MTEMA – MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KWA WIZARA YA​
  Mheshimiwa Naibu Spika, ninawashukuru Ukoo wote wa kina Mtema na Kihaule; wazaziwangu Dkt. & Mrs. Estelatus Mtema na ndugu zangu wote kwa upendo wao mkubwa. Kwa namnaya pekee, namshukuru sana pacha wangu mpenzi ninayefanana naye Bi. Remija Mtema, kwaUpendo na msaada mkubwa kwangu. Hakuna raha duniani kama kuzaliwa mapacha hasa
  mnaofanana. (Makofi)


  Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuwashukuru viongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani;Mheshimiwa Freeman Mbowe, Mheshimiwa Kabwe Zitto, Mheshimiwa Tundu Lissu, kwa kuniamini
  na kuniteua kuwa Waziri Kivuli wa Wizara hii. Naahidi sitawaangusha hata kidogo. (Makofi)

  Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho lakini kwa umuhimu mkubwa napenda kutoa shukrani
  zangu za dhati kabisa kwa rafiki yangu mpendwa, Mheshimiwa John John Mnyika, Mbunge waUbungo kwa kunilea vema, kunifundisha ujasiri, uchapakazi na uadilifu wakati tukiwa tunaiongozaIdara ya Vijana CHADEMA Makao Makuu. Hivi nilivyo leo ni sehemu ya malezi yake. Nakushukurusana Kamanda! (
  Makofi)

  Mheshimiwa Naibu Spika, tunakutana leo ikiwa imebaki miezi minne tu kuelekeakuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Tangu Uhuru, wafanyakazi wa Tanzaniawamekuwa na mchango mkubwa katika siasa na ujenzi wa Taifa. Tanzania tunayoiona hii leoisingewezekana kama si kwa mchango wa wafanyakazi.

  Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wa wapigania haki za wafanyakazi kama marehemuMzee Rashid Mfaume Kawawa, Mzee Abdul Sykes, Mzee Dosa Aziz na Michael Kamaliza hauwezikusahaulika kwani wameacha alama ya kudumu katika historia ya Taifa letu.Mheshimiwa Naibu Spika, sisi sote humu ndani, tunasimama katika mabega ya mashujaawafanyakazi waliotutangulia, pamoja na wale ambao leo bado wanatoka jasho kulisimamishaTaifa letu.

  Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mchango wao mkubwa kwa Taifa hili, wafanyakaziwa Tanzania bado hawavuni kile walichopanda, bado hawajafaidi vizuri matunda ya jasho lao, wala matunda ya uhuru wa nchi yao. Madai mengi ya wafanyakazi yanahusiana na mambo yamaslahi, usalama, haki, usawa na utu wao.

  Madai haya mengi ni ya muda mrefu na yanapaswakupatiwa ufumbuzi. Hatuwezi kujenga Taifa la kisasa kwenye nchi ambayo wafanyakazi
  wamekata tamaa. Hotuba kamili isome hapa: http://www.parliament.go.tz/POLIS/PAMS/Docs/HS-4-41-2011.pdf
   
 2. J

  Japhet Mukala New Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  very sad,truely we lost visionary,
   
 3. K

  Kisinga Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuna pengo kubwa katika aliyoyafanya
   
 4. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  dunia kweli mapito
   
 5. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Saa zingine uneweza fikiria kukata rufaa lakini haiwezekani kila chenye mwanza kina mwisho na mapenzi ya Mungu lazima siku zote yatimizwe. Tunaamini Mungu ataleta Regia wengine wengi
   
 6. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mungu ailaze roho ya marehemu Regia mahala pema peponi, AMIN.
   
 7. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tenda mema siku zote huwezi jua muda wala saa utakapoitwa mbele ya haki.
   
 8. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  RIP Regia, Duh! Ungekuwa hai kuna mambo ningeomba utufafanulie

  ........ndiyohiyo
   
Loading...