- Thread starter
- #101
Waarabu walitangaza mipango ya ukanda maalum wa ushoroba ambao utaunganisha rasi (Peninsula) ya Arabia na Israeli. Itaunganisha India na Ulaya na njia za meli baharini, mitandao ya reli, mabomba ya nishati, nyaya za mawasiliano fiber optic.
22 April 2026
Yerusalem, Israel
Milei, akitembelea Knesset, anasema Argentina itahamisha ubalozi wake hadi Yerusalemu mwaka wa 2026
Rais wa Argentina anakaribishwa kwa uchangamfu na Netanyahu, Ohana na Lapid, ambao wote wanasifu msimamo wake wa kuunga mkono Israeli, wanamkaribisha kama 'rafiki wa kweli
Rais wa Argentina Javier Milei akicheka huku Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akizungumza wakati wa kikao maalum cha Bunge kwa heshima ya kiongozi huyo mgeni wa Amerika Kusini, Juni 11, 2025. (Yonatan Sindel/Flash90)'
Rais wa Argentina Javier Milei, ambaye yuko katika ziara ya siku tatu nchini Israeli, alizungumza katika kikao maalum cha mkutano wa bunge Knesset kilichofanyika kwa heshima yake Jumatano, ambapo alitangaza kwamba nchi yake itahamisha ubalozi wake kutoka eneo la Tel Aviv hadi Yerusalemu mwaka huu.
Alikaribishwa kwa uchangamfu katika kikao cha bunge na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, Spika wa Bunge Amir Ohana na Kiongozi wa Upinzani Yair Lapid, ambao wote walisifu kwa dhati uhusiano mzuri ambao umeibuka kati ya Israeli na Argentina chini ya uongozi wake.
"Javier, wewe ni rafiki wa kweli. Kwa ziara hii, tunaleta uhusiano wetu katika kilele kipya. Kuna umbali wa Kilomita 12,000 kutoka jiji la Buenos Aires Argentina na hapa Israel jijini Yerusalemu," Netanyahu alimwambia kiongozi huyo wa nchi ya bara la Amerika Kusini aliyetembelea. "Lakini Umbali huu mkubwa unalipwa na ukaribu wa mioyo yetu."
Milei, ambaye alitangaza kwa mara ya kwanza nia yake ya kuhamisha ubalozi wakati wa ziara yake ya kwanza ya kitaifa nchini Israeli mnamo Februari 2024, alitangaza katika kikao cha bunge la Knesset kwamba "mwaka 2026 tutafanya rasmi uhamisho wa ubalozi wetu kwenda jiji la Yerusalemu Magharibi uwe na ufanisi."
Ubalozi huo wa Argentina kwa sasa upo Herzliya, nje kidogo ya Tel Aviv.
Rais Milei alifungua hotuba yake kwa ujumbe wa huzuni, akihutubia shambulio la kigaidi lililoongozwa na Hamas la Oktoba 7, 2023 kusini mwa Israeli, ambapo watu wapatao 1,200 waliuawa na 251 walichukuliwa mateka, na vita vilivyofuata katika Ukanda wa Gaza, ambao sasa uko katika mwezi wake wa 21.
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu (kushoto) akizungumza pamoja na Rais wa Argentina Javier Milei (katikati) katika kikao cha bunge mjini Yerusalemu, Juni 11, 2025. (Yonatan Sindel/Flash90)"Dunia ilishuhudia ukatili mkubwa" mnamo Oktoba 7, alisema. "Tuliamini kwamba hatimaye tumekomesha ukatili huu - janga la Oktoba 7 lilituamsha kutoka kwenye ndoto hii."
"Argentina iko upande wenu katika siku hizi ngumu," aliwaambia wabunge wa Knesset. "Kwa bahati mbaya, hilo haliwezi kusemwa kuhusu sehemu kubwa ya jumuiya ya kimataifa ambayo inadanganywa na magaidi na kuwageuza waathiriwa kuwa wahalifu."
Kiongozi huyo wa Argentina anayeendelea na ziara Israel alisema kwamba Buenos Aires (Argentina) itaendelea kudai kwamba mateka hao waachiliwe huru, wakiwemo wale wanne wenye uraia wa Argentina.
Pia alitumia fursa hiyo kumkosoa mwanaharakati wa hali mabadiliko ya hewa na mazingira Greta Thunberg, ambaye alikamatwa na kufukuzwa nchini Israel mapema wiki hii baada ya kusafiri kwa meli hadi eneo hilo kwa lengo la kuvunja kizuizi / kikwazo kwa Gaza.
Mamluki Thunberg "alikuwa kama bunduki iliyokodishwa kwa ajili ya kuleta taharuki kidogo ya vyombo vya habari, akidai kwamba alitekwa nyara wakati kuna mateka katika hali zisizo za kibinadamu huko Gaza," alisema, kulingana na tafsiri ya matamshi yake kutoka Kihispania yaliyotolewa na Knesset.
"Ulimwengu unaruhusuje genge la kigaidi la mauaji kuendelea kuwashikilia raia wasio na hatia mateka?" aliuliza. "Wakati jumuiya ya kimataifa nafiki ikiwapa genge la kigaidi Hamasa sifa zote nzuri na mbaya , hakuna usawa wa kimaadili hapa."
Kisha alichukua sauti chanya zaidi, na akageukia kuelezea "miujiza mingi" ambayo Israeli na Wayahudi wameifanya.
"Muujiza wa kwanza ni kuanzishwa kwa Taifa la Israeli baada ya Mauaji ya Kimbari (Holocaust), na wa pili ni kunusurika kwa Israeli baada ya majaribio ya mara kwa mara ya kuliangamiza," alisema.
Alipendekeza kwamba muujiza wa tatu uliofanywa na Israeli ulikuwa ule wa "mapinduzi ya kilimo yaliyofanya jangwa kuchanua kwa mazao, asali na maziwa."
"Mmefanikiwa kulima chakula kwenye ardhi ambayo hakuna kitu kingine kilichokua au kumea," alisifu rais Milei.
Rais wa Argentina Javier Milei (kushoto) akizungumza katika kikao cha bunge mjini Yerusalemu, Juni 11, 2025. (Yonatan Sindel/Flash90)Kwa upande wake, Netanyahu alimshukuru rais Milei kwa "kusimama nasi bega kwa bega katika kampeni dhidi ya nguvu za giza," na akatangaza kwamba Israeli na Argentina "zitafanikisha mambo makubwa" pamoja.
Mkikabiliana na "uchokozi wa kikatili na usio wa kawaida wa Hamas, mlisema kwa maneno waziwazi bila kumungunya neno - tuko upande wenu katika vita dhidi ya nguvu za giza," Waziri Mkuu alisema.
Rais wa Argentina Javier Milei (Kulia) akimkumbatia Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu (Kushoto) wakati wa hafla ambayo alihutubia bunge Knesset, Juni 11, 2025. (Menahem KAHANA / AFP)Alimwambia rais wa Argentina kwamba Hamas inajaribu "kukandamiza utu wa binadamu na haitasita kufanya hivyo kwa njia yoyote ile."
"Ninaweza kuwahakikishia kwamba tutaendelea kupigana nao. Israeli ni ngome ya demokrasia katika eneo hili la Mashariki ya Kati," alitangaza. "Hatutaanguka, wala hatutasalimu amri, tutashinda, na tutawarudisha walio hai na wafu wote. Tutahakikisha kwamba Gaza haitishii tena Israeli."
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na wajumbe wa serikali wakihudhuria kikao maalum cha kumkaribisha Rais wa Argentina Javier Milei katika kikao cha Bunge, Juni 11, 2025. (Yonatan Sindel/Flash90)Sifa kwa uongozi wa Argentina chini ya rais Milei ilirudiwa na Lapid na Ohana, ambao walitangaza kwamba alikuwa "rafiki bora zaidi wa Taifa la Israeli na Wayahudi" katika historia ya nchi yake.
"Mara kwa mara, mmechagua kupendelea ukweli kuliko faraja, imani kuliko kuiga, na dira ya maadili kuliko kuwa sehemu ya walio wengi kufuata mkumbo kiotomatiki," Ohana alisema. "Kwa kusimama bega kwa bega na taifa la Israeli, mmewaunganisha watu wa Argentina katika hadithi ya kudumu milele ya Wayahudi."
Rais wa Argentina Javier Milei atembelea Ukuta wa Magharibi katika Jiji la Kale la Yerusalemu, mnamo Juni 9, 2025. (Chaim Goldberg/Flash90)Lapid alimhutubia Milei kwa Kihispania kutoka kwenye jukwaa la bunge Knesset, akimwambia kwamba, "kwa kuwa waziri mkuu hajui Kihispania, naweza kukuambia kwa siri kwamba hatukubaliani katika karibu kila kitu. Lakini kuna mambo mawili ambayo tunakubaliana."
"La kwanza ni kwamba Wayahudi wana haki ya kujilinda. Israeli haitasalimu amri wala kuinama. Wala mbele ya ugaidi wala mbele ya uongo," alisema kiongozi huyo wa upinzani. "La pili ni kwamba urafiki na uungaji mkono wako kwa Israeli unakubaliwa nasi sote bila kujali tofauti za kiitikadi za vyama ."
Akibadilisha lugha hadi Kiebrania, Lapid alitumia fursa hiyo kuanzisha shambulio la kisiasa la kificho dhidi ya Netanyahu kwa kusifu mageuzi ya kiuchumi ya Milei.
Milei "sio tu rafiki mkubwa wa Israeli, pia ni mwanasiasa wa mrengo wa kulia mwanamabadiliko wa kiuchumi," alisema Lapid, akibainisha kuwa "jambo la kwanza" alilofanya alipochukua madaraka lilikuwa kufunga "wizara zote zisizo za lazima" za serikali yake.
"Leo, wana wizara nane za serikali. Nchi yenye watu milioni 46. Inatosha kwao. Kupunguza idadi ya watumishi wa serikali, kuwafukuza wasaidizi, kupunguza marupurupu, kupigana na utamaduni wa uvivu na kuishi kwa ufahari kwa gharama ya wengine kupitia kodi," Lapid alisema, akiongeza: "Tujifunze kutoka kwa mtu aliyekuja kututembelea leo."