Hotuba ya John Pombe Magufuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya John Pombe Magufuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mamaWILLE, Oct 23, 2011.

 1. mamaWILLE

  mamaWILLE Senior Member

  #1
  Oct 23, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mida ya saa 6 mchana leo magufuri alifika igunga. Ulikuwa msafara wa magari 29 yakiserikari na wakandarasi. Mkutano ulikuwa wa serikari maana bendera ya taifa ilikuwapo ktk kiwanja hiki cha sokoine. Nasema hivyo kwani neno ccm oyeee! ndio lilikuwa likitamkwa mara nyingi sana.sasa zamu ya Magufuri ikawadia nae akaanza hivi.
  Magufuri: Ndugu zangu wanaigunga ninawashukru kwa mapokezi na washukuru na kuwapongeza kwa
  uchaguzi umekwisha na sasa kutekeleza kazi kwa wanaigunga
  Maendeleo hayana chama. Likitengenezwa daraja la mbutu, watu wote watapita. chadema, ccm cuf, udp watapita ktk daraja hilo hata fisi nao watapita ucku. Leo nimepita nikitokea tabora nilikuwa nina kikao na makandarasi wa tabora. Tabora kwa sasa kuna makandarasi 6 wanaojenga barabara za tabora.
  Wakati nilipokuja mkumnadi Dr kafumu niliwaahidi kuwa nitajenga daraja la mbutu, manonga, na barabara ya igurubi. Fedha kwa ajili la daraja la mbutu zipo ila ujenzi wake utatumia muda
  Tulitangaza tenda ajili ya daraja hili, 24/8/2011katika magazeti yote ya kiswahi na 25/8/2011katika magazeti ya kiingereza ilikusudi na wakandarari wa nje waje ili tupate mkandarasi mzuri. mpaka sasa tumepata makandarasi 11.
  Nawaomba ndugu zangu tuache itikadi zetu za uchadema na ucc kwani kampeni zimekwisha sasa ni utelekezaji ilani ya ccm.
  Nawaomba ndugu zangu pindi ujenzi ukianza msiwaibie wakandarasi mafuta, na vifaa vya ujenzi kwani daraja ni letu watanzania

  Nawaomba wanaigunga mshilikiane na mbuge wenu dr kafumu atakaye apishwa. Na diwani wa chadema naomba ushilikiane na mbunge wa ccm. Mwelezenu shida zenu dr kafumu.

  Ninawaomba mliokuwa mnagombea ubunge kazi sio ubunge tu. Wengine mnatakiwa muende mkasimamie ujenzi wa daraja ili mpate ajira.

  Leo hii nimekuja na wakandarasi wote ili nikawakabidhi site. Na kwa yeyote anayebisha basi baada ya mkutano twende nae akaone huko huko. Asante sana
   
 2. wijei

  wijei JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Somehow it is impressive
   
 3. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hili daraja hata angeingia wa UPDP lazima lingejengwa coz bajeti yake ipo tayari,tenda ilishatangazwa hata kabla ya kampeni.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  "Uchaguzi umepita, tuache politic tuchape kazi" anasema magufuli lakini badala ya kuanza kuifanya hiyo kazi ni yeye ndiye aliyeitisha huo mkutano kuendeleza siasa za majukwaani. kwani angeenda tu na hao makandarasi akawagaiw site zao na wakaanza kufanya kazi wananchi wasingeona kuwa kazi zinafanyika?
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Igunga ingekuwa chini ya Mbunge wa chama kingine (siyo ccm) Magufuli angefunga safari kupiga hizi porojo? Na swali la muhimu ambalo Magufuli angetakuwa kujibu ni hili, wananchi wa Igunga wanatakiwa washuruku kwa sababu mpokea kodi (serikali) zao anajenga daraja, au serikali kupitia kwa Magufuli walitakiwa wawaombe msamaha watu wa Igunga kwa kula kodi zao kwa miaka 50 bila kujenga daraja?
   
 6. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ningependa kujua idadi ya watu ilikuwaje hapo uwanjani, na kama walikuwa na nyuso za furaha.
   
 7. oba

  oba JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  mzee huyu naye kama atajiingiza kwenye siasa za maji taka ataporomoka, tulimzoea kama mchapa kazi kwa ajili ya watz na siyo porojo za chama gani kinafanya nini!
   
 8. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Huyu inaonekana katumwa na JK kwenda kuwapoza wana-Igunga kwa mauaji ya makada wa CHADEMA wakti wa kampeni, kwa kura zilizochakachuliwa/kuibwa na kuondoka kwa RA baada ya kusakamwa na Magamba kwa Ufisadi. CCM wanajua kabisa hawajawatendea haki wana Igunga wakti wa Uchaguzi na hawakupaswa kushinda.Kwa hiyo hii ni namna ya kuwapoza na kuwabembeleza watu wa Igunga ili wasahau yaliyotokea wakti wa Uchaguzi wa mbunge wao.

  Hata hivyo watu wa Igunga hawahitaji Daraja la Mbutu tu. Bado HAWANA MAJI SAFI NA SALAMA PAMOJA NA ZAHANATI/HOSPITALI ZA UHAKIKA Walipaswa wamwulize ni lini hizo huduma zingine zitawafikia kama CCM kwa miaka 50 wameshindwa kazi hiyo!
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,966
  Trophy Points: 280
  Kwenye kuhusu ujenzi wa daraja hilo,Mh Magufuli alisema...
  Duh!Haya bana.
   
 10. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2011
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Yaani mkuu hapo kwenye red umeeleweka, watu tumeteseka na mto huo wakati wa livu yaani sintosahau halafu eti leo anawaleta makandarasi kuwaonyesha tu huo mto Mbutu tayari keshaanza porojo zake za kisiasa, ukweli RA alijiuzuru wakati Bunge likiendelea na daraja hilo likawa agenda ya haraka na kuchomekwa kisiasa kwenye bajeti ya mwaka huu na bado ukifuatilia kwa makini Dr Mwakyembe hakuweza kutaja bayana kuwa ni shillingi ngapi zitatumika mpaka daraja kukamilika (angalia tarehe ya kutangazwa tenda), Hao makandarasi ni lini wamefanya feasability study ya eneo la mto mbutu? hili ni changa la macho ambalo linaweza chukua miaka minne likiwa limelenga 2015 kwa ajiri ya kupata kura za ndugu zetu wasioelewa, nashukuru wengi hivi sasa ni waelewa wazuri na wanasubiri na ahadi ya maji toka ziwa Victoria kama Mkapa alivyoahidi,...hivi sasa huko vijijini kama Mbutu, Isakamaliwa, Kininginila Ibutamisuzi wakimwona mtu kachafuka na hajaoga wanasema ..." Nekagi akoga minze ga Ngwa'za ulogushika"
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  magufuri oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  ndio maana nampenda magufuri yeye ni mtendaji hana blabla hata kama ni siasa lakini jambo la msingi ni wana igunga kupata daraja na kuwaeleza kwamba kazi imeanza.....bravo magufuri
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  tulikuwa tunalalamika hapa hapa JF kwamba baada ya ushindi wa Igunga CCM wanatumia muda mwingi kujipongeza badala ya kutekeleza ilani ya uchaguzi wa Igunga. kitendo cha magufuri cha kurudi tena Igunga na kuwaeleza alipofikia kinasitahili kupongezwa
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  he did a good job...
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  jamani tuache siasa kwenye masuala ya msingi kitendo hiki cha magufuri ni cha kuigwa na wanaCCM wengine. tumekuwa na kawaida kwamba wanasiasa wanatutusa baada ya uchaguzi kuisha lakini magufuri amekuja kivingine safi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Oct 23, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  sisi wananchi wa kigamboni hatuna uhisiano na siasa za Igunga na kata yangu ya vijibweni iko chini ya CUF kwa upande wa udiwani lakini kasi ya magufuri katika ujenzi wa daraja la vijibweni - kigamboni ni ya kuridhisha....... tumpongeze huyu bwana ni mchapa kazi na mtu muhimu sana kwa chama chake na siasa za tanzania ya leo
   
 17. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #17
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi ni John Pembe au Pombe. Pombe si kileo, hata kwa wenzetu waliotutangulia sijawahi kusikia mtu Mr. Beer au Mr. Alcohol au Mr. Wine japo wapo akina Winehouse. Pombe hatari halafu ndo jina la mtu ama kweli ccm kuna mambo. Halafu kuna mwingine anaitwa Membe, Membe kwetu ni fisi ni jina la dhihaka kwa watu walafi
   
 18. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #18
  Oct 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,530
  Likes Received: 5,679
  Trophy Points: 280
  Mbona hawafanyi hivi kwenye majimbo waliyoshinda cdm? Tunatengeneza nini kama nchi! Siwezi kusifu juhudi zinazokuwa driven na vitu vya kipuuzi.ni sawa na mchezaji mpira asiyeweza kucheza bila kuvuta bangi! Kujituma nje ya kusukumwa na itikadi chafu nasisitiza chafu tena kwa kumwaga damu za watu hata yawe mema ya kiwango gani ni upuuzi tu.mkutano wa serikali ccm oye ndio nini! Nyerere alipo sema mtu akisema anachukia rushwa inabidi hata tukimtazama tuone inatoka moyoni! Tanzania yote kuna matatizo ya kutisha! Why igunga tena sasa? Pesa za huo mradi tena uliohaidiwa kwenye kampeni(kosa kisheria) zimetoka wapi? Anachofanya Magufuli nafananisha na definition ya money laundering! Juhudi za magufuli sasa (ambalo ni jambo jema kwa matokeo yake) ni matokeo ya rushwa hata kama wana igunga watafaidika lakini msingi wake utaendelea kuitafuna igunga!
   
 19. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #19
  Oct 23, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wenzie uwa wanaona ana kiherere kumbe hicho kiherere ndio maendeleo wananchi wanayotaka.Pia wenzie wanapenda sana kuweka UCCM hata kwa mambo ya Taifa.Sio Mbaya Big Up Magufuri
   
 20. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #20
  Oct 23, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,026
  Likes Received: 2,676
  Trophy Points: 280
  Aloo wape nafasi na wenzio mbona unataka kujaza mapost yako tu?
   
Loading...