Hoteli ya Kapuya yashambuliwa, mwanawe chupuchupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoteli ya Kapuya yashambuliwa, mwanawe chupuchupu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dingswayo, Sep 24, 2009.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3699

  MTOTO wa Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, hajulikani alipo, kajificha ili wananchi wasimdhuru.

  Kijana huyo aliyetajwa kwa jina la Baraka aliwatoroka wananchi wenye hasira muda mfupi baada ya mlinzi katika hoteli ya baba yake kudaiwa kumuua mwanafunzi kwa kumpiga risasi kwenye ukumbi wa disko Jumapili usiku.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Emson Mmari,amesema,walitaka kumshambulia mlinzi huyo, akawatoroka, walipomkosa wakataka kumshambulia Baraka, akakimbia kujikoa na hadi sasa haijulikani yupo wapi.

  "Huyu Baraka kwa taarifa nilizozipata, wananchi baada ya kumkosa mlinzi wake, walimsaka na kurusha mawe kwenye dirisha la chumba chake, lakini aliwatoroka na kuingia kwenye gari na kukimbia," amesema Mmari jana.

  Amesema,wameshindwa kupata thamani ya hasara kwa vile wenye jengo hilo hawapo,kwa sababu Baraka angewasaidia kuwaeleza thamani ya vitu hivyo haijulikani aliko.

  "Sisi huyu hatumtafuti ila amekimbia hasira za wananchi ambao walitaka kumdhuru," amesema.

  Kwa mujibu wa Mmari, Polisi wa Tabora walizuia wananchi hao wasiichome moto hoteli ya Millennium inayomilikiwa na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana,Profesa Juma Kapuya, Jumapili usiku,imefahamika.

  Wananchi walipandwa na jazba baada ya mlinzi wa hoteli hiyo kudaiwa kumuua mwanafunzi aliyekuwa anacheza disko kwenye ukumbi wa hoteli hiyo wakataka kuichoma moto hoteli hiyo.

  Amesema jana kuwa, baada ya mwanafunzi huyo kuuawa, wananchi walipandwa na jazba, wakavunja viti, vyombo vya muziki, na vioo vya madirisha ya hoteli hiyo ili kulipiza kisasi.

  Mmari amesema, hata magari yaliyokuwa eneo hilo, pikipiki, na baiskeli viliharibiwa,maduka yaliyopo kwenye jengo hilo yalivunjwa,na kwamba wanachi hao walipora vitu vilivyokuwa humo.

  Amesema,baada ya uharibifu huo, baadhi ya wananchi waliandaa mpango wa kuliunguza jengo hilo, lakini kwa bahati nzuri polisi waliwahi kufika na kuvuruga mpango huo.

  "Polisi waliitwa na walipofika eneo hilo waliwatawanya wananchi hao wenye hasira, lakini kuna uharibifu mkubwa umefanywa na watu hao na wengine walishaandaa mafuta wakitaka kulichoma jengo hilo maarufu kama Millennium House," amesema Mmari.

  Amesema, polisi wameendelea kuweka ulinzi kwenye hoteli hiyo ili yasitokee madhara zaidi.

  "Tumeweka ulinzi kuzuia hasara zaidi," alisema na kuongeza kuwa bado hajajua hasara iliyopatikana kutokana na uharibifu huo.

  Akielezea chanzo cha vurugu ndani ya disko hilo, Mmari alisema ni msuguano kati ya mlinzi na baadhi ya vijana waliokuwa kwenye disko na katika ugomvi huo, baadhi ya vijana walijaribu kumnyang'anya silaha.

  Amesema, mlinzi huyo alipofyatua risasi na kumpata kijana mmoja na ndipo wananchi wakapandisha hasira na kumfanya mlinzi huyo akimbie.

  Hata hivyo, Kamanda Mmari amesema, mlinzi huyo amekamatwa mjini Tabora, yupo polisi.

  Mwanafunzi aliyeuawa kwenye tukio hilo anatajwa kwa jina la Majuto aliyekuwa anasoma katika sekondari ya Ushokola mjini Kaliua na alizikwa Jumatatu.

  Kamanda Mmari amesema,polisi wanafanya uchunguzi wa awali kuhusu mauaji ya mwanafunzi huo,utakapokamilika watamfikisha mahakamani mlinzi kumfungulia mashitaka ya mauaji.
   
  Last edited by a moderator: Sep 25, 2009
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Duu, huku kwetu Tabora twafa sana kwenye Madisco. Yaani twapenda kujirusha siye utafikiri ndiyo mkoa tajiri kuliko yote. Huyu Kapuya na yeye, Mu-Islam gani mwenye miradi kama hii ya Bar, Disco, Acudo nk nk?

  Braza Kapuya, tafuta miradi mingine itakayotoa ajira watu wengi zaidi na siyo kuwakamua hata hivyo visenti vichache walivyo navyo. Kama una miradi mingine yenye kutoa ajira kubwa Tabora basi narudisha heshima......
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sikonge,
  Huyu Kapuya anaumbuliwaga na majanga tu. Hatukujua anamiliki mgodi wa madini mpaka alipoibiwa mitambo yake. Sasa tumejua anamiliki pia disco la Millenium.
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  na bado tutajua mengi tu, bado hajafumaniwa
   
 5. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  kapuya ni kati ya wanasiasa matajiri sana hapa tanzania, lakini utajiri wake haujulikani nini chanzo chake
   
 6. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Haramu ni mbaya sana, inakuumbua hata kama uko mafichoni.
   
 7. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #7
  Sep 25, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Waziri Kapuya yupo New York. I am sure atasikitika sana kusikia Majuto ameuawa,hasa ukifiria kwamba yeye ni Waziri wa Vijana.
  Amina Kapuya anasema amefurahi kusikia kwamba ni mlinzi ndiye atakayefunguliwa mashtaka,na kwamba siyo Baraka.[is this the gaffe on my part?]
   
 8. Bambo

  Bambo JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 237
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  sasa mnaweza kuona je waziri huyo anatumia percentage ngapi ya muda wake kuwaza kuhusu nchi ili percentage inayobaki awaze ya kwake!!!! Akudo,migodi,bar,night clubs n.k..Tatizo la Rais wetu ni utekelezaji wa anayoyasema ni ziro nakumbuka kuna wakati alisema kama unataka kuwa kwenye biashara achana na siasa ili usije ukachanganya biashara zako na madaraka..!!nchi yetu ni masikini na nafasi za kazi ni chache ni bora kuwapa uwaziri watu ambao watatumia muda wao kwenye mambo ya kitaifa..
   
 9. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  sasa si bora huyu kawekeza hapa nchini kuliko hao wanaozificha tu huko nje,tena nao bora wangewekeza nje tungepata sifa ya kuwa na wawekezaji wa kibongo huko nje na kufaidi kodi,lakini wao wanazificha tu huko ili wananchi wa huko waende kukopa katika mabenki ya huko,
   
 10. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #10
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sasa huyo Baraka ana kosa gani kama aliyeua ni mlinzi? Wananchi nasi bwana!!

  Poleni wafiwa
   
 11. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,215
  Likes Received: 2,078
  Trophy Points: 280

  Sure. Majanga ndio yanafichua haya!

  Braza, chanzo chake hicho hapo juu!
   
 12. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Mambo ya kukosa kazi na kufuata mikumbo huwa hakuna reasoning. Ni kutenda halafu kufikiria ni baada ya kitendo
   
 13. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hiyo miradi sio yake ila ameafungulia wanae. Na yeye hausiki kabisaaaaa.


  Inachosikitisha ni Alhaji
   
 14. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Mkuu hivi unawaambia hawana reasoning na hawana kazi wakazi wa hapa kaliua? hivi unamjua BARAKA ATHUMANI KAPUYA FULL BOSS vizuri? ungekuwa na hata hint juu ya huyu mtu usingesema hivyo bali ungesema hao wananchi wa kaliua wamewekewa Nsamba na akina kapuya jinsi walivyo lichukulia suala hili kwa upole.Naamini tukio hili lingetokea Dar au sehemu nyingine huyu bwana angekuwa marehemu tayari.
  N:B Nsamba ni dawa za mapenzi za kinyamwezi zinazowafanya watu wanakuwa kama makondoo kwa wapenzi wao,huwasikiliza kufuata maagizo bila kuuliza.
   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu Burn,
  Kwanza asante kwa hilo neno la NSAMBA. Nakumbuka ule wimbo wa ngoma ya HIARI ya Moyo wanaocheza Mduara akina mama kwenye sherehe hasa za harusi na wanaimba "nalitumila nsamba ya kumlomo" yaani "natumia nsamba ya mdomoni aka maneno matamu".
  Sasa hebu tupe basi data mambo yalivyokuwa na huyu Baraka ambaye kwa haraka haraka naona kama ni Mungu mtu wa Kaliua. Itabidi nimpigie simu Dogo ambaye alikuwa mwalimu huko na sasa karudi Sikonge/Mibono.
   
Loading...