Hoteli mpya ya Lowasa ktk plot ya serikali

Hoteli mpya ya Lowasa ktk plot ya serikali

ndugu hiyo sehemu ilishauzwa...uliza vizuri hiyo ndio serikali na nafikiri si swala la kumlaumu lowassa laumu serikali yako...NIC IMEUZA NYUMBA HAPA KATI MOJA WAPO WALIKUWA WAKIPIGA KELELE KANUNU MKULU WETU SO HAYA MAMBO YA KUGAIANA YAPO SWALA NA WEWE FAITI UINGIE KWENYE SISITIMU UJIGAWIE...NAMAANISHA KILA MTU SASA AJITAHD KUINGIA KWENYE MLO UKIWASUBIIRI HAWA UTAKUTANA WAJUKUU WANAKUFA MASKINI
 
m2 anaemtetea lowasa simwelewi. pale dodoma alichukua kiwanja eneo la area d karibu na kwa feruzi wakati akiwa waziri mkuu akapiga greda kwa mkwara alipotimuliwa akalitelekeza.eneo hilo lilikuwa hifadhi ya mji.huyu ndiye lowasa anaetetewa na wana ccm.
 
ndugu hiyo sehemu ilishauzwa...uliza vizuri hiyo ndio serikali na nafikiri si swala la kumlaumu lowassa laumu serikali yako...NIC IMEUZA NYUMBA HAPA KATI MOJA WAPO WALIKUWA WAKIPIGA KELELE KANUNU MKULU WETU SO HAYA MAMBO YA KUGAIANA YAPO SWALA NA WEWE FAITI UINGIE KWENYE SISITIMU UJIGAWIE...NAMAANISHA KILA MTU SASA AJITAHD KUINGIA KWENYE MLO UKIWASUBIIRI HAWA UTAKUTANA WAJUKUU WANAKUFA MASKINI

Yes! Hata kama Lowasa ni mbaya, afanyeje wakati swala la kuuziana kiswahiba lilianzishwa na Mkapa? Kwenye system kama hii survival yako ni kuwa na mahusiano na wakubwa. Sasa Lowasa yuko nao , aache kutumia mwanya kwa sababu tu ni Lowasa? No. Hata ungekuwa wewe ungefanya hivyo.
Hapa kinachotakiwa ni kupata uongozi thabit ambao utabadilisha mfumo huu wa kishikaji ili watu sasa waanze kufuata sheria.
Tena ikibidi, kama akatokea kiongozi, basi afanye tume ya maridhiano, ili hao waliojigawia mali waweze kuomba radhi, ikiwa ni pia kukubali kurejesha baadhi ya mali hiyo serikalini. Kujaribu kuwafunga, itakuwa kazi sana , maana ngazi zote wameshiriki wizi , ikiwa ni pamoja na majeshi yetu. Hivyo hawatakubali kuachia kirahisi. Patachimbika!
 
JK kasema " Lowasa ni mtu safi, yaliyopita si ndwele tugange yajayo, watu wa Monduli wampe kura awe mbunge wao" naongeza na atampa uwaziri wa fedha:A S 13: Hili ni JAMBAZI bwana, sioni cha ajabu kuona Kalembo kuwa katika hilikwani huyu ni Shemeji yake Mama Salma kwa hoi kapewa ukuu wa mkoa na mlozi mwenzake na anafanya madudu kma kawa.
 
Lowassa ni "addict" wa ardhi, viwanja na majengo. Daniel Yona anamfuata kwa mbali kisha FT Sumaye.
 
Msighafilike ndugu zangu kwani kwenye maandiko matakatifu tunajifunza yafuatayo:-

PROVERBS 13:11 Wealthy gained by dishonesty will be diminished but who gathers by labour will increase

Kwa hiyo baada ya Dr. Slaa kuingia madarakani tu mali zote hizo za wizi zitarudishwa kwa amri ya mahakama zetu bila zengwe na kifungo kinamsubiri cha muda mrefu. huyo jambazi.
 
Kwa kweli mi nipo Morogoro, na kwa bahati (mbaya sijui) huwa hiyo barabara napita almost kila siku, hivyo imekuwa rahisi kukusanya vipandevipande vya taarifa kutoka kwa watu. Awali eneo hilo lilikuwa mali ya LITI na lilipakana na eneo la Magereza. Inasemekana hata hivyo ilikuja kuibuka mgogoro baina ya taasisi hizo mbili juu ya umiliki wa eneo hilo (miaka ya 90). Sintofahamu hiyo ilipelekea manispaa kuamua kulichukua eneo hilo na kuligawa viwanja miaka hiyo hiyo na waliobahatika walilipia hadi sh 500,000 kwa kiwanja kimoja (miaka ya 90). Wakati zoezi hilo likikaribia kumalizika, aliyekuwa Principle wa LITI alipeleka malalamiko Wizarani, na ikaamuliwa kuwa eneo hilo libakie kuwa la Serikali. Waliokuwa wamelipia viwanja walitakwa radhi na Manispaa na baada ya kufuatilia kwa miaka kadhaa (mostly waliopata viwanja walikuwa 'wakubwa' hivyo hakukuwa na kuandamana au nini sijui) walifanikiwa kupewa viwanja vingine maeneo ya Kilimanjaro (ni eneo hapa Moro).

Eneo libakia kuwa chini ya umiliki wa serikali, sehemu moja ikiangaliwa na LITI na nyingine ikiangaliwa na Magereza (ingawa halikuendelezwa). Binafsi SIJUI ni nini kilifanyika, lakini mwaka juzi eneo lile lilianza kuendelezwa kwa kujengwa, na hapo ndipo duru mbalimbali zikaripoti kuwa panajengwa Hotel ya kitalii, inayomilikiwa na Lowassa. Kuwa alifanyaje hadi akalipata, haieleweki vizuri, kila mtu anaeleza kivyake, lakini watu wote niliosikia wakielezea wanasema linamilikiwa na Lowassa, na kuan wakati amekuwa akionekana katika eneo hilo (binafsi sijawahi kumuona). Kinachowahuzunisha watu hapa ni pale wananchi wa kata lilipo walipoomba eneo hili wajenge shule ya kata wakakataliwa na kwenda kupewa eneo maeneo ya nanenane, kilomita kadhaa, mbali na kata hiyo, hivyo inawalazimu wanafunzi kutumia usafiri hasa wa dala dala kufika shule, wakati eneo lililopo katani mwao amepewa 'mwekezaji'.

Sambamba na hilo, lipo eneo jingine kilomita kadhaa nje ya mji wa Morogoro, kuelekea Kilosa, ambalo kwa miaka ya karibuni limezungushiwa fence ya seng'enge na linasemekana ni la Lowassa tena. Ni eneo kubwa ambalo kwa mwendo wa kawaida utaendesha gari takribani dakika ishirini, kutokea mwanzo hadi mwisho ukipita barabara iliyopakana na eneo hilo kwa upande mmoja. Kwa hiyo hapa tunaongelea ekari elfu kadhaa, au kilomita kadhaa za mraba. Inasemekana kuwa mmiliki wa eneo hili anataka kulifanya zoo ya kisasa (kama za sauz). Hii inawezekana kwa sababu eneo hili limepakana na Mikumi National park, na kwa bahati (mbaya pengine), linabeba mto mkubwa usiokatika maji hata kiangazi, ambao wanyama wa mikumi hufika kunywa maji hasa majira ya kiangazi.

Eneo hilo lililopo nje ya mji wa Morogoro lipo kata ya PARAKUYO Lipo mbele ya Ranch ya mkata nie eneo kubwa sana na ndani ya eneo hilo kuna nyumba zaidi ya 40 za makazi ya watu na makanisa mawili na msikiti mmoja.
 
Back
Top Bottom