Hoteli mpya ya Lowasa ktk plot ya serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoteli mpya ya Lowasa ktk plot ya serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MchunguZI, Oct 6, 2010.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Naona mzee huyu Ufisadi hawezi kuacha.

  Pitapita yangu ilinifikisha mjini Morogoro.

  Kwa wenyeji nilipita njia ya Boma road kuelekea kwa mkuu wa mkoa. Kushoto ktk iliyokuwa bustani ya matunda ya LITI, nilikuta majengo makubwa kabisa yakijengwa.

  Bila kutegemea niliambiwa ni Hotel ya Lowasa inayojengwa ktk eneo la taasisi ya serikali!

  Sijui kama kuna sheria inayoruhusu mtu binafsi kupewa miliki ya viwanja vya serikali lakini hapo imewezekana na taarifa nilizopata, JK anajua na mkuu wa mkoa aliyeko Tanga sasa hivi bw. Said Kalembo alisaidia sana juu ya kutolewa kwa eneo hilo na viongozi wa LITI kulazimishwa kushuhudia kwa maandishi kwamba eneo hilo ni mzigo kwao!

  Pamoja na ufisadi, naanza kutia mashaka juu ya ubora wa akili ya mtu huyu, maana hata kibaka mtaani akizomewa huonyesha uso wa aibu. HUYU VIPI!
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Lowassa hana aibu. Anaiona Tanzania nzima kama ni Lowassa Inc. Mtu huyu hatari kupewa usukani wa kuendesha nchi, Mwalimu Nyerere alisema siku nyingi.
   
 3. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mchunguzi, jitahidi upate ripoti yenye ushahidi zaidi kwani ya kusikia yanaweza kuwa mengi zaidi ya ukweli. It may be difficult in te beggining but try since upo karibu. Hata kama itakuchukua mwaka.
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Lowasa again...!!!!
   
 5. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndo niya yangu na ni bahati mbaya kwamba sikuchukuwa jina lilioandikwa ktk kibao cha ujenzi. Uhakika nilionao ni kwamba hilo ni eneo la bustani ya LITI kwa miaka mingi na kinachojengwa siyo majengo ya serikali maana sikuona nembo yoyote ya ki-serikali, bali jina la kienyeji.

  Kwa vyovyote vile, mjenzi ni powerful kiasi cha kuweza kuingia eneo la serikali ndo maana alipotajwa sikusita maana majirani wanasema jamaa huyu yupo pale kila wakati kwa kujificha ficha. Nipe siku mbili nitaleta kitu cha ziada.
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kuwa na wtu kama Lowasa katika uongozi wa nchi ni sumu sana ya maendeleo ya nchi kwani sheria zinafanya kazi tu kama kuna maslahi kwake. Mwanzoni mwa miaka ya tisini akiwa Waziri wa ardhi alionekana kuwa mtunza sheria sana za ardhi ndipo akapata umaarufu, lakini kumbe alikuwa ndumila kuwili aliyekuwa anatumia vyombo vya habari kujitangaza kuwa anasimamia sheria za ardhi halafu baadaye anapokea rushwa kutoka kwa wahindi ili wajenge kwenye viwanja mbalimbali kinyume cha sheria. Uharibikaji wa mipango miji Dar ltunaoona leo hii umechangiwa sana na Lowasa huyo ambaye alikuwa waziri wa ardhi wakati ujenzi binafsi ulipoanza kwa kasi hapo Dar wakati wa utawala wa Mwinyi. Tangu Lowasa achafue utaratibu wa ujenzi mijini, tatizo hilo limekuwa kansa kubwa sana; ndiyo maana Dar ya leo hii pamoja na kuwa inapata majengo mazuri kila kukicha, lakini bado mji wenyewe uko shaghla baghla kiasi cha kuwa mmoja wa miji kumi mibovu duniani.
   
 7. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Sasa umeshanichanganya. Yale majengo yanajengwa kwenye kiwanja cha Magereza au LITI. Kulikuwepo na kamgogoro wa hicho kiwanja na EL alikuwa anasimamia ujenzi mwenyewe 2009. Niliwahi kusikia huu mgogoro lakini nilipuuzia sikuamini. Ila kulikuwepo na taarifa kabwana mdogo fulani au wa ardhi au magereza ilibidi ahamishwe kukwepusha shari yake.

  Pamoja na kusema hayo, EL ni mwekezaji mzuri katika miliki(real estate investor). Inawezekana anaiba lakini walau amerejesha kwa kuweka kwenye ardhi ambayo haihamishiki! Hilo tu! Hilo tu! Hilo tu! Watu wa namna hii hawana aibu, hawana woga, hawajali, hawasikii, hawachoki! Kuna watu wanaovamia viwanja vya watu na kujenga, na wanaotesha nyumba hawa, wanachukua gari kadhaa zinawasha taa usiku, vijana wanajenga! Hii tabia sijaipatia maelezo. Inabidi aje mtaalamu wa saikolojia au tuseme sayansi ya tabia atusaidie tuwaze kuwaelewa watu wa namna hii. Maana hata iweje raha yake ni kuwa amefanikisha huo uwekezaji, watu wapige kelele hana habari. Na sio kwamba atalala kwenye hayo majengo au nini. Na kwa nini utumie pesa yako (kama ni yako kweli) kwa shida na manyanyaso kwa kiwango hicho. Hili linahitaji utafiti wa kiwango cha juu kung'amua hawa binadamu wa aina ya Lowasa, Manji na Mushi
   
 8. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  :A S angry::A S angry::A S angry::A S angry::Cry:
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  SISI waDANGANYIKA wasahaulifu sana huyu LOW AS ... (LOWASA) ni mtu mbaya sana hata MWalimu Nyerere ktk kitabu chake alimkataa akasema huyu mtu si msafi, hafai kuwa kiongozi ktk nchi hii, lkn cha kushangaza JK akamfanya awe waziri mkuu. no maana tupo hapa tulipo hakuna kinachofanyika bali ni wizi tu wa mali ya umma mchana kweupeeeeeeeee. CHADEMA tutakapo chukua nchi watu kama hawa lazima wafikishwe kizimbani.
   
 10. m

  mgololafinyonge Member

  #10
  Oct 7, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  How far are you sure ni Lowassa? Kama we are sure kabisa we can fight for our right mtoa mada lete evidence so that we can be sure
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ikitaifishwa na serikali ijayo itaongeza pato la nchi.
  Thanx Lowasa kwa kuanza kurudisha tarrrtib. ila ujue sisi ni simba ambao tunajua harufu ya prey
   
 12. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Siamini kabisa,lakini sitaki kupuuza kabisa, kwa kuwa waswahili wanasema lisemwalo lipo kama halipo linakuja.kwa kuwa mtoa taarifa amekili kuwa hiyo ni hearsay,taarifa hii inatia mashaka kidogo.Kama ni kweli basi lowasa anatisha, anaweza kunywa hata uji wa mgonjwa!pamoja na kusemwa kote huku!
   
 13. A

  Anold JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Mimi sioni tatizo kama amefuata taratibu zote anazotakiwa mwekezaji yeyote afanye.Isitoshe Lowasa ni mtanzania mwenzetu hivyo hakuna ubaya wowote akimiliki eneo
  katika nchi hii ukilinganisha na hao wanaoitwa wawekezaji wakigeni ambao
  wanafilisi Tanzania yetu na pesa yote kuondoka nayo. Fikilia wawekezaji wa migodi n,k hao ni wageni lakini wanatunyoa kipara watanzania bila aibu wala huruma. akipewa eneo Kaburu au Mzungu hiyo haina tatizo ila akipewa mtanzania mjasilia mali huyo ni fisadi. Acheni tabia hizo za wivu wa maendeleo na fitna kwa watanzania. Watanzania wengi tunafikiri umaskini na kutojishughulisha ni dalili za usafi na uadilifu, sitaki kuamini hivyo, nijuavyo mimi uwoga wa kuthubutu ndiyo umetusukuma hadi kuwatafuta wawekezaji wa kigeni tukiamini kuwa sisi hatuwezi! huo ni ujinga tena ujinga mkubwa. Sitaki kuthubutu kuamini kuwa serikali inaweza kukubali mtu binafsi au kiongozi atumie eneo la serikali bila taratibu kufuatwa, nakushauri ndugu uliyeandika tuhuma hizo ungefanya utafiti wa kutosha badala ya kutuambia umeambiwa. Je kama huyo aliyekuambia hakufanya utafiti wa kutosha hutakuwa umepotosha umma? Katika mambo haya nafikiri umakini unahitajika ili kumtendea haki mtu badala ya kukurupuka na kuropoka maneno ambao huna uhakika nayo (aani maneno ya kuambiwa).

  jambo la msingi ambalo lingefanyika kwanza ni kutaka kujua uhalali wa majengo hayo katika eneo serikali. Nani mmiliki, nani katoa kibali n.k.
   
 14. A

  Anold JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Acheni majungu
   
 15. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #15
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kwa kweli mi nipo Morogoro, na kwa bahati (mbaya sijui) huwa hiyo barabara napita almost kila siku, hivyo imekuwa rahisi kukusanya vipandevipande vya taarifa kutoka kwa watu. Awali eneo hilo lilikuwa mali ya LITI na lilipakana na eneo la Magereza. Inasemekana hata hivyo ilikuja kuibuka mgogoro baina ya taasisi hizo mbili juu ya umiliki wa eneo hilo (miaka ya 90). Sintofahamu hiyo ilipelekea manispaa kuamua kulichukua eneo hilo na kuligawa viwanja miaka hiyo hiyo na waliobahatika walilipia hadi sh 500,000 kwa kiwanja kimoja (miaka ya 90). Wakati zoezi hilo likikaribia kumalizika, aliyekuwa Principle wa LITI alipeleka malalamiko Wizarani, na ikaamuliwa kuwa eneo hilo libakie kuwa la Serikali. Waliokuwa wamelipia viwanja walitakwa radhi na Manispaa na baada ya kufuatilia kwa miaka kadhaa (mostly waliopata viwanja walikuwa 'wakubwa' hivyo hakukuwa na kuandamana au nini sijui) walifanikiwa kupewa viwanja vingine maeneo ya Kilimanjaro (ni eneo hapa Moro).

  Eneo libakia kuwa chini ya umiliki wa serikali, sehemu moja ikiangaliwa na LITI na nyingine ikiangaliwa na Magereza (ingawa halikuendelezwa). Binafsi SIJUI ni nini kilifanyika, lakini mwaka juzi eneo lile lilianza kuendelezwa kwa kujengwa, na hapo ndipo duru mbalimbali zikaripoti kuwa panajengwa Hotel ya kitalii, inayomilikiwa na Lowassa. Kuwa alifanyaje hadi akalipata, haieleweki vizuri, kila mtu anaeleza kivyake, lakini watu wote niliosikia wakielezea wanasema linamilikiwa na Lowassa, na kuan wakati amekuwa akionekana katika eneo hilo (binafsi sijawahi kumuona). Kinachowahuzunisha watu hapa ni pale wananchi wa kata lilipo walipoomba eneo hili wajenge shule ya kata wakakataliwa na kwenda kupewa eneo maeneo ya nanenane, kilomita kadhaa, mbali na kata hiyo, hivyo inawalazimu wanafunzi kutumia usafiri hasa wa dala dala kufika shule, wakati eneo lililopo katani mwao amepewa 'mwekezaji'.

  Sambamba na hilo, lipo eneo jingine kilomita kadhaa nje ya mji wa Morogoro, kuelekea Kilosa, ambalo kwa miaka ya karibuni limezungushiwa fence ya seng'enge na linasemekana ni la Lowassa tena. Ni eneo kubwa ambalo kwa mwendo wa kawaida utaendesha gari takribani dakika ishirini, kutokea mwanzo hadi mwisho ukipita barabara iliyopakana na eneo hilo kwa upande mmoja. Kwa hiyo hapa tunaongelea ekari elfu kadhaa, au kilomita kadhaa za mraba. Inasemekana kuwa mmiliki wa eneo hili anataka kulifanya zoo ya kisasa (kama za sauz). Hii inawezekana kwa sababu eneo hili limepakana na Mikumi National park, na kwa bahati (mbaya pengine), linabeba mto mkubwa usiokatika maji hata kiangazi, ambao wanyama wa mikumi hufika kunywa maji hasa majira ya kiangazi.
   
 16. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 853
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 80
  Wadau tue makini na maoni tunayotoa....There is so much prejudice against Lowasa....Mdau Mchunguzi naomba ufanye mambo mawili....kwanza tafuta evidence kwamba kweli mmiliki ni Lowasa...pili tafuta evidence kwamba taratibu zilifuatwa katika kummilikisha Lowasa eneo hilo(kama itathibitika kweli yeye ndie mmiliki)... Baada ya hapo tutaweza ku-analyse issue hii!!!!! The isssue so hot that hearsays can't draw clear-cut conclusions
   
 17. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,184
  Trophy Points: 280
  CCM ina wenyewe, na wenyewe ndio hao sasa.
   
 18. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,184
  Trophy Points: 280
  Hii kitu nliisikia hapa jamvini tangu mwaka jana.
  Lisemwalo lipo, kama halipo LINAJONGEA
   
 19. s

  smilingpanda Member

  #19
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  it looks like most of the people are cought with this election thing so everything gets politicised.Lowassa is building a hotel that's good news,he is giving back the money he stole to you,he is going to create jobs for your brothers and sisters, he is going to pay taxes,improve the influstructure.
  my point here is why can't we be positive when it's necessary guys, stop politisizing everything, it's gross!
   
 20. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  nchi ishauzwa hii ni kungoja receipt ambayo nayo inaweza kuwa feki
   
Loading...