HOTEL MAARUFU KIRUMBA VALLEY BADILIKENI.

7spirits

JF-Expert Member
Dec 1, 2015
612
514
Siwataji kwa jina ila kwa muktadha tajwa hapa nafikiri mnajijua.
Kwenu siku hizi hata sabuni za kuogea ni shida, achilia mbali kuweka hata kanda mbili za kuogea, taulo na karatasi laini za chooni.
Chakula inabidi mteja aje hotelini amekula kabisa huko atokako na akitegemea hapo kwenu basi ajiandae kulala njaa na kama hakunyoosha nguo basi ajiandae kuvaa nguo isiyonyoshwa na hakuna uhusiano mzuri kwa mteja akitaka huduma ya kunyooshewa nguo.
Kama hamjijui, ni ninyi mliowahi kutwaa tuzo ya hoteli bora jijini Mwanza miaka mitatu/minne iliyopita ila miaka ya karibuni mmekuwa hamsikilizi wateja utadhani ni guest bubu...bei zenu hazilingani na huduma yenu, mtu akiweka oda ya chakula kama amebahatika kukikuta oda itachukua hata masaa manne kuandaliwa chakula, Air Conditions zimejikatia tamaa, chai asubuhi mnaleta hadi maembe mabichi utadhani wateja wote waliolala hapo ni wajawazito....!!!!!!!
Ni nini kimewapata au ndiyo namba za kirumi zinasomeka????? Nawashauri kama ushindani ni mkali kibiashara au kama namba zinasomeka kwa Kirumi basi badilisheni matumizi ya hayo maghorofa hata mpangishe hostel badala ya hotel isiwe tena kama mtu analala hotelini kama amelala kwa msamaria mwema kumbe analipia. Meneja husika, jamani elfu 65,000/=, 55,000/=, 45,000/= si hela ndogo kwa maisha ya kitanzania.
 
Back
Top Bottom