Hosteli za Magufuli kutumika kama karantini za kuweka wageni kutoka nchi zilizoathiriwa na Corona

Hapa Dar niko kabla ya Makonda, nimezaliwa na kukulia hapa hapa, natembea na kwenda popote bila ruhusa ya mtu yoyote. Tena hapa nilipo naona kama kesho inachelewa nione wa kunizuia.
Problem ni JF kuruhusu matumizi ya pseudo identities. Wewe hapa utajimwambafai. Nani anakujua? Inawezekana ukakamatwa na bado ukasema hujakamatwa. Nani anakujua? Kama wewe ni mtemi, badili usajili wako humu na badala yaTindo weka jina lako la NIDA halafu kesho uzurure uone kama utarudi nyumbani kabla ya siku 14 kuisha! Kama wewe mtemi kweli na huogopi, narudia tena, weka jina lako la NIDA hapa! Hapo ndio utajua Serikali ipo kazini!
 
Hostel za MAGUFULI hazina cafeteria chakula watakula wapi? Wanafunzi wanaoishi pale wanakula kwa mama lishe
Tuko seriuos kiasi cha kutosha?

Yaani wenzetu wanafunga mipaka na viwanja vya ndege alafu sisi tunaendelea kuwapokea wageni!!

Kwa umasikini wetu, kujikinga kwa gharama yoyote ndio ponepone yetu maana hata mataifa makubwa yanaelemewa na huu ugonjwa ndio sembuse sisi.

Na je, huu si ushahidi kuwa vyuo bado sana kufunguliwa?

Kingine nachojiuliza, ni nini yatakuwa madhara ya kutumia hizo hostel ambazo zitakuja kutumiwa na mamia ya wanafunzi endapo kuna vimelea vitasalia baada ya karantini kwisha?

Sitashangaa kuona au kusikia baadhi ya wanafunzi wakisita kuzitumia hizo hostel hata kama zitapigwa dawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli amehamia Dodoma kwa nini lile jengo la Ikulu ya zamani lisitumike kama kituo cha kushikilia wagonjwa wa korona kwa muda? Hizo hostel ni hatari kwa sababu wanafunzi watarudi kuishi humo

Yaani haujui vidudu vina span life?

Pathetic
 
Cafeteria inashushwa kutoka mbinguni au inatengenezwa?

Misibani wanafanyaje? Hakuna mahema, na temporary structures?
Mkuu;
Nakuona unajitahidi sana kutoa elimu kwa hawa jamaa wajinga jinga waliojaa hapa Jamiiforums!

Nakupongeza sana kwa uvumilivu wako.

Jamiiforum ya sasa imejaa watu wajinga ambao hawajui kama niwa wajinga.
 
Back
Top Bottom