Hosteli za Magufuli kutumika kama karantini za kuweka wageni kutoka nchi zilizoathiriwa na Corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,033
9,923
Hosteli za Magufuli kutumika kama karantini

Serikali imetangaza rasmi kwamba wasafiri wote kutoka nchi za nje zilizoathirika na ugonjwa wa Corona watalazimika kukaa karantini kwa muda wa siku 14 katika hosteli za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam maarufu hosteli za Magufuli.

Akizungumza katika hosteli za Magufuli, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema wasafiri hao watafikia katika hosteli za Magufuli ambazo zipo katika eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam.

“Lengo ni kuhakikisha tunadhibiti mienendo ya wasafiri hawa.Tumeona taarifa ambazo zimetoka kule Iringa, kuna baadhi ya wasafiri tuliwaweka hotelini wakatoroka sasa ili kudhibiti mienendo ya wasafiri hawa na kuwalinda Watanzania wengi tumeona kuna ulazima wa kuwaweka sehemu moja ambako kutakuwa na ulinzi wa saa 24 na mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda atasimamia kwa karibu chini ya Wizara ya Afya,” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy Mwalimu amewataka wananchi waelewe kwamba wasafiri hao si wagonjwa kwa sababu wanatoka kwenye nchi zenye maambukizi yenye virusi vya Corona (Covid-19) hivyo wasichukuliwe kama ni wagonjwa.

“Tunawachukulia kwamba miongoni mwao kuna mmoja, wawili au watu watatu wakawa na maambukizi ya virusi vya Corona. Tutawaweka hapa kwa siku 14 kwa lengo la kuwaangalia afya zao, itakapofika siku 14, wale ambao hawajaonyesha DALILI zozote tutawaruhusu waende majumbani kwao lakini wale watakaoonyesha dalili ndani ya siku tano, sita, Saba, nane hadi siku ya 14 tutachukua sampuli na kuwapima ili kujiridhisha Kama wana virusi vya Covid-19,” amesema Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa kwa mujibu wa taarifa za maambara Hali ya wagonjwa waliopata maambukizi ya Covid-19.“Tuko vizuri, watu waliopata maambukizi ni 20, tumepata kifo kimoja, wagonjwa watatu wamepona na wamesharudi nyumbani.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameishukuru Wizara ya Afya kwa namna ambavyo Imekuwa ikipambana kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa Corona nchini.
 
Tuko seriuos kiasi cha kutosha?

Yaani wenzetu wanafunga mipaka na viwanja vya ndege alafu sisi tunaendelea kuwapokea wageni!!

Kwa umasikini wetu, kujikinga kwa gharama yoyote ndio ponepone yetu maana hata mataifa makubwa yanaelemewa na huu ugonjwa ndio sembuse sisi.

Na je, huu si ushahidi kuwa vyuo bado sana kufunguliwa?

Kingine nachojiuliza, ni nini yatakuwa madhara ya kutumia hizo hostel ambazo zitakuja kutumiwa na mamia ya wanafunzi endapo kuna vimelea vitasalia baada ya karantini kwisha?

Sitashangaa kuona au kusikia baadhi ya wanafunzi wakisita kuzitumia hizo hostel hata kama zitapigwa dawa.
 
Magufuli amehamia Dodoma kwa nini lile jengo la Ikulu ya zamani lisitumike kama kituo cha kushikilia wagonjwa wa korona kwa muda? Hizo hostel ni hatari kwa sababu wanafunzi watarudi kuishi humo
Kwa hiyo wagonjwa wa COVID-19 wanaolazwa kwenye hospitali baada ya ugonjwa kuisha wodi hazitatumika tena kulaza wagonjwa wengine wenye magonjwa mengine kwa sababu wodi zitakuwa ni hatari?

Tatizo lako ni ujinga na hujui kuwa ni mjinga! Kumbuka ujinga sio tusi!
 
Magufuli amehamia Dodoma kwa nini lile jengo la Ikulu ya zamani lisitumike kama kituo cha kushikilia wagonjwa wa korona kwa muda? Hizo hostel ni hatari kwa sababu wanafunzi watarudi kuishi humo

Sasa mkuu hapa ndio umetoa ushauri gani au ni kiburi tu? FYI marais popote pale ulimwenguni huwa wana kuwa na Ikulu ndogo ndogo ndani ya nchi sasa chijui unapapenda sana Magogoni au ndio umburukenge wenyewe?
 
Huyo ni Nyumbu wa Ufipa. Lazima apinge lolote linalofanywa na serikali. Ajabu, kama serikali ingesema wakae Kempiski kwa gharama zao, angepinga na kusema kwanini wasiwekwe Magufuli Hosteli kwakuwa wanafunzi hawapo. Sasa wanapelekwa huko anapinga! Labda anataka wapelekwe kwenye Makao Makuu ya Chadema Ufipa!
Naona malipo yamerudi, congratulations mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwananchi Newspaper tweet:

Serikali imesema wasafiri kutoka nchi zilizoathirika na ugonjwa wa corona watalazimika kukaa karantini kwa siku 14 katika hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam maarufu hosteli za Magufuli #M
Hivi kumbe bado Kuna ndege za kigeni zinatua Dar au tunamaanisha wageni watakao vuka kule mtwara,kasumulo,Namanga,mnanila,Rusumo na Tunduma?
 
Kidume Magufuli ameikimbia Corona Dar, amejificha kwenye mawe huko.
Ikulu Magogoni ingependeza zaidi wawekwe huko, maana ilijengwa na wageni wenyewe/ mabeberu.
 
Back
Top Bottom