Hostel za udsm vs Ghorofa za Magomeni

Hostel za udsm vs Ghorofa za Magomeni

Block moja lenye floor 4 udsm limetumia milioni 500. Yaan wastani wa million 125 kwa floor nzima.
 
Pale Magomeni wameharibu eneo lile bure
Pale walitakiwa jenga hata kamji ka kipekee pale
 
Kwanza kabisa nitangulie kusema uzi huu si wa kupingana wala kui-challenge serikali yangu bali kuibua mjadala ambao utatusaidia kusimamia vema rasilimali za taifa. Sasa naomba kuanzia hapa;

Hostel za UDSM
Naambiwa yapo majengo 20 kila jengo lina ghorofa 4 na gharama yake ni 10bn

Ukichukua majengo 20 X kwa ghorofa 4 utapata ghorofa 80 (floors) ambazo zimetumia 10bn.

Maghorofa ya Magomeni;
Naambiwa yapo majengo 5 kila jengo lina ghorofa 8 hadi 9 na gharama yake ni 20bn. Tufanye wastani wa ghorofa 9 kwa zote.

Ukichukua majengo 5 X kwa ghorofa 9 utapata ghorofa 45 (floors) ambazo zimetumia 20bn

Sasa pale Magomeni kuna shida. Yafaa kuunda tume kuokoa pesa ya taifa maana Jografia ya Dar ni ile ile iweje wametumia pesa nyingi vile?

Naomba changia kwa weledi, usimtukane mtu, usimtukane Kiongozi yeyote maana ni kosa kisheria. Weka point tujifunze usiweke tusi!

My friend you have to go back to school

Zile ni hostel ujenzi wake ni tofauti na Nyumba za kuishi

I mean zinakuwa na partition tofauti na vyumba vyumba
 
Mleta mada unasikitisha kwa ulichokiona umetumia akili kuchambua...duh
 
Acheni kuhamisha magoli mimi nilipata kazi flan pale HOSTEL pale ...imetumika zaidi ya 10Bl na wanamadeni kwa Supplier wenyewe wanakili walifanya Siasa ili wapewe majengo mengi na wameahidi watakuwa wanaongeza ..Bajeti ili kufidia majanga ya Hostel
... Taratiiibuu kitaanza kueleweka, niliwahi kusema kuhusu hii issue kwamba kwa uzoefu wangu hapa JF tutapata wachangiaji ambao wamehusika kwenye huo ujenzi.
 
... It's unfortunate kwamba mpaka sasa ninachokiona kwenye hii post ni matusi na mapovu tuu, bado hamjampa jibu mleta mada kwa nini kuna hiyo tofauti ya bei kimahesabu?
Hili nalo kweli linahitaji degree kufahamu utofauti uliopo kati ya hostel na apartments? Hebu tuache masikhara bwana,, hosteli nyingi unaweza kukuta chumba kimoja tu kinakatiza upana wa ghorofa zima lakini kwenye apartments unakuta kuna vyumba vya kulala, sebule, dinning, vyoo, bafu, jiko na stoo; sasa yote haya unataka yalingane gharama na hostel? Kweli? Kikubwa angeuliza kwanza ukubwa wa hayo majengo na kama ramani zake zinafanana! Mimi nasema gharama ya Magomeni iko sawa!!
 
... Hostel wanaishi nani kama si watu? Au wanafunzi si watu?
Ndugu yangu unakoelekea utakuja kuuliza kwanini Ujenzi wa Kanisa ni gharama ndogo kuliko HOTEL ya Kulala wageni
 
Mkuu zile blocks zina vyumba vya kuishi.. Yaani Kuna nyumba ambazo wamedesign kuishi familia na Sio Yale blocks ambapo ni hostels..

Nikusaidie tu Kuna nyumba zinajengwa Ukonga Magereza kwa 10bn na znasimamiwa na hao TBA please zikikamilika angalau Njoo na mjadala ulinganishe na hizi hostels.. Japo si sahihi sana
 
Kwanza kabisa nitangulie kusema uzi huu si wa kupingana wala kui-challenge serikali yangu bali kuibua mjadala ambao utatusaidia kusimamia vema rasilimali za taifa. Sasa naomba kuanzia hapa;

Hostel za UDSM
Naambiwa yapo majengo 20 kila jengo lina ghorofa 4 na gharama yake ni 10bn

Ukichukua majengo 20 X kwa ghorofa 4 utapata ghorofa 80 (floors) ambazo zimetumia 10bn.

Maghorofa ya Magomeni;
Naambiwa yapo majengo 5 kila jengo lina ghorofa 8 hadi 9 na gharama yake ni 20bn. Tufanye wastani wa ghorofa 9 kwa zote.

Ukichukua majengo 5 X kwa ghorofa 9 utapata ghorofa 45 (floors) ambazo zimetumia 20bn

Sasa pale Magomeni kuna shida. Yafaa kuunda tume kuokoa pesa ya taifa maana Jografia ya Dar ni ile ile iweje wametumia pesa nyingi vile?

Naomba changia kwa weledi, usimtukane mtu, usimtukane Kiongozi yeyote maana ni kosa kisheria. Weka point tujifunze usiweke tusi!
Mzee kwa kutumia Idadi ya Ghorofa huwezi kulinganishe Bei
Tuambie hizo idadi ya Gorofa zote zina mita za mraba kiasi gani?
Au unataka kutuambia ramani ile ile iliyotumia Ubungo ndio iliyotumika Magomeni?
Unaweza kjenga nyumba hio hio moja mmoja akatumia Ceiling Fan mwengine akweka AC na bie zitkuwa tofauti sana
 
Kwanza kabisa nitangulie kusema uzi huu si wa kupingana wala kui-challenge serikali yangu bali kuibua mjadala ambao utatusaidia kusimamia vema rasilimali za taifa. Sasa naomba kuanzia hapa;

Hostel za UDSM
Naambiwa yapo majengo 20 kila jengo lina ghorofa 4 na gharama yake ni 10bn

Ukichukua majengo 20 X kwa ghorofa 4 utapata ghorofa 80 (floors) ambazo zimetumia 10bn.

Maghorofa ya Magomeni;
Naambiwa yapo majengo 5 kila jengo lina ghorofa 8 hadi 9 na gharama yake ni 20bn. Tufanye wastani wa ghorofa 9 kwa zote.

Ukichukua majengo 5 X kwa ghorofa 9 utapata ghorofa 45 (floors) ambazo zimetumia 20bn

Sasa pale Magomeni kuna shida. Yafaa kuunda tume kuokoa pesa ya taifa maana Jografia ya Dar ni ile ile iweje wametumia pesa nyingi vile?

Naomba changia kwa weledi, usimtukane mtu, usimtukane Kiongozi yeyote maana ni kosa kisheria. Weka point tujifunze usiweke tusi!

Cost za construction huwa hazipigwi hivyo kama unafanya biashara ya mayai. Site ya udsm ilikua new but ya magomeni kota inainvolve demolition of existing structures na kujenga mpya
 
Nyumba ya kuishi inamakolokoli mengi. Hostel ni nyumba tu. Afu pale chuo vitu vingine vimelipwa na Chuo..furnitures ni za chuo. Pale magomeni vyote vitalipwa naserikali. Nyumba ya kuishi inahitaji vitu vingi mno..hata vyumba vyake sio bwalo kama za histel
Natamani kujua serikali inahusisha institutions zipi
 
Hoja yako nzuri ila mie nadhani gharama inatofautiana kutokana na malengo na matumizi ya jengo husika, UDSM ni hostel kwa ajili ya kuwahifadhi watu kwa ajili ya malengo maalumu hivyo vitu vingi vinakuwa vimejengwa kwa ajili ya matumizi ya public tofauti na magomeni ambapo nyumba zile ni kwa ajili ya familia hivyo kila kinachowekwa pale ni kwa ajili ya familia hivyo kunakuwa na nyongeza za hapa na pale kwa kila idara yaani maji, sijui umeme na mambo mengine kila nyumba / apartment inajitegemea wakati UDSM wanaweza wakasema floor hii inatumia mita moja ya umeme..n.k

Ngoja wataalamu waje maana mie nimetoa maoni "in lay man perspective"
 
Mkuu hii umetoa wapi?....
acheni kusikiliza porojo za watawala gharama waliyopeleka Tba kwenye mradi wa Hostel ilikuwa ni Siasa mradi ule umewakula Pesa nyingi kuliko inayozungumzwa amini ninachokwambia
 
Back
Top Bottom