Mbolabilika
JF-Expert Member
- Jul 30, 2019
- 2,126
- 2,860
Serikali ya Kenya inatengeneza muongozo wa uangalizi salama wa wagonjwa wa virusi vya corona wakiwa nyumbani.
Kulingana na waziri wa afya Mutahi Kagwe serikali inachukua hatua hiyo ili kupunguza msongamano katika hospitali za umma ili kuzuia kujaa kupitia kiasi
”Hospitali za Mbagathi na Kenyatta zinakaribia kujaa. Wagonjwa wengi waliothibitishwa ni wagonjwa wa pumu na wanaweza kutibiwa kutoka nyumbani”, alisema waziri huyo
Kagwe alitoa tangazo hilo huku wagonjwa wengine 124 wakithibitishwa kuwa na virusi hivyo hatua inayofanya idadi ya wagonjwa walioambukizwa virusi hivyo nchini Kenya kufikia 2,340
Maktba
Wakati huo huo Serikali imetishia kutoa picha za wagonjwa wa Covid -19 waliotoroka vituo vya karantini katika vyombo vya habari.
Waziri Kagwe amesema kwamba hatua hiyo itachukuwa wajibu muhimu ili kuwasaidia raia kuwatambua wale walio hatari kwao.
Kagwe amesema kwamba wale wanaotafutwa wamebadilisha mbinu na wameamua kuzima simu zao na kuendelea kutangamana na raia na hivyo basi kuhatarisha maisha ya wengine.
‘Unapozima simu yako, na kutoka Kawangware na kuelekea Thika na kurudi huku marafiki zako wakitupigia simu’, hiyo ina maana gani, alisema Kagwe.
Aliongezea, “Tunapofikia wakati ambapo tuna thibitisho kwamba unatoroka, hakuna chochote kinachoweza kuizuia wizara kuchapisha picha zako magazetini.
Alisema kwamba picha zitaandamana na maelezo yanayosema kwamba mgonjwa huyu ametoroka katika kituo cha karantini na hivyo basi ni mtu hatari kwa umma.
Waziri huyo amesema kwamba wagonjwa sita waliotoroka karantini Turkana walitafutwa na kurudishwa katika kituo hicho.