Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,583
- 6,633
SERIKALI hutoa ruzuku ya sh bilioni 36.7 kila mwaka kwa hospitali 97 za mashirika ya dini nchini.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, alitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage (CCM), aliyetaka kujua ni kwanini serikali isitumie hospitali za misheni kwa kuzipa ruzuku ya dawa na mishahara ya watumishi, ili ziweze kutoa huduma bora na kwa gharama nafuu kwa wananchi.
Aidha, mbunge huyo aliihoji serikali kama iko tayari kupandisha hadhi zahanati ya Bumbile, ili iweze kuhudumia visiwa vya Bumbile, Kalebe na Makibwa vilivyo mbali na hospitali za misheni za Ndolage, Rwantege na Kagondo.
Akijibu swali hilo, Dk. Rashidi alisema ruzuku hiyo ni mbali na ile iliyotolewa na halmashauri za mashirika ya dini kutoka katika mfuko wa maendeleo na mishahara ya watumishi walioshikizwa katika hospitali hizo.
Sambamba na hilo, alisema serikali inaendelea kuboresha mazingira yatakayoziwezesha hospitali hizo ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi kwa gharama nafuu.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inasimamia ubora na viwango katika kutekeleza hili. Wizara imeweka vigezo vya utoaji huduma kwa kila ngazi, alisema Dk. Rashidi.
Tanzania Daima | Mei 23, 2013