Hospitali ya Seliani (Arusha) acheni ubaguzi wa rangi

ambiliki

Member
Jun 26, 2013
80
46
Jana usiku nilimpeleka mgonjwa hosipitalini hapo. Kilichonisikitisha ni gharama kubwa alizo takiwa kulipa. Nilipouliza sababu za kumchaji hivyo wakasema si mzawa. Vipimo ambavyo ni vya kawaida walichaji 150,000. Kulazawa kwa siku moja 500,000 (laki tano).

Mbaya zaidi, wamechukua pesa ya kumuoda dakitari 50,000 na mgonjwa hakuona na dakitari na walikataa kurudish. Hii ni hospitali ya kanisa ila ina ubaguzi wa rangi tena uliopitiliza. Kweli kitanda kwa siku laki tano bei ya hoteli nyota tano hapo bado matibabu kisa si Mtanzania.

Huyu mgonjwa ni mtu ambaye ameishi Tanzania zaidi ya miaka mitano; ameoa Mtanzania anaishi hapa, ila Seliani Hospitali hakuna ubinadamu. Wanathamini pesa kuliko uhai wa binadamu.

Kuna siku nakumbuka walimrudisha mgonjwa mahututi kisa hana pesa. Ndugu waliomba wasaidiwe wakatafute pesa, walikataa katu. Hivi hapa ni vipimo walivyotaka walipwe laki na nusu na pia gharama walizochaji kumuona daktari na dakitari hatukumuona, ilibidi tuondoke na mgonjwa wetu.

IMG_20210209_022937_2.jpg
IMG-20210209-WA0003.jpg
IMG-20210209-WA0001.jpg
 
Samahani mwanajamvi sijaelewa unaposema mgonjwa amekaa Tanzania miaka 5 ni raia wa kujiandikisha au?
 
Ndiyo hiyo hiyo
Huyo mgonjwa ulompeleka ni mzungu nini?? kama ni mzungu watakuwa walijua ana hela ndiomama wakamcharge parefu au wakamcharge in dollars instead of Tsh....pia hiyo ni hospital ya private..ko wapo kibiashara zaidi, bila pesa hupati huduma..but huduma zao ni nzuri sana
 
Haya matakataka yenu mnaita dini ndo ubeberu wenyewe
Jina ni la dini Tatizo linakuja waajiriwa sio wa dini hivyo nni kuamua tu imradi hospitali ipate mapato makubwa apewe sifa kurinda kibarua
 
Kwani bei za kutalii tz mzawa na mgen ziko vip kama vitu sio special kwa Jil yenu mue mnaacha Kwan bongo hospital si Zipo nying
 
Back
Top Bottom