Hospitali ya Seliani (Arusha) acheni ubaguzi wa rangi

Ipo wapi hiyo hospitali nimpigie Dkt Gwajima akawaadabishe.
Huyo Dr Gwajima hospital za Dodoma za serikali zimemshinda kusimamia.Sera ya afya inasema watoto chini ya umri miaka mitano matibabu ni bure,lakini leo tarehe9/2/2021 hospital ya General ya serikali nimelipia gharama ya cheti tuu kwa mtoto wa mwaka mmoja tsh15000/=.Serikali hii si ya kuiamini hata kidogo tena unalipa na wala hawana wasiwasi kwa maana ndiyo utaratibu wao kuchukua fedha kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.
 
Pole sana mkuu kwa maswaibu yaliyokukuta ,serikali ya ccm ilisema itatoa bima ya afya kwa waTZ wote ,ngoja tusubiri Gwajima na Roboti Mollei wamefikia wapi.?
 
Hiyo hospital mimi naiona Kama Mogadishu fulani siwezi kupita hapo wana gharama sio za nchi hiyo kuitwa hospital ya kanisa ni pazia tuu...
 
Jana usiku nilimpeleka mgonjwa hosipitalini hapo. Kilichonisikitisha ni gharama kubwa alizo takiwa kulipa. Nilipouliza sababu za kumchaji hivyo wakasema si mzawa. Vipimo ambavyo ni vya kawaida walichaji 150,000. Kulazawa kwa siku moja 500,000 (laki tano).

Mbaya zaidi, wamechukua pesa ya kumuoda dakitari 50,000 na mgonjwa hakuona na dakitari na walikataa kurudish. Hii ni hospitali ya kanisa ila ina ubaguzi wa rangi tena uliopitiliza. Kweli kitanda kwa siku laki tano bei ya hoteli nyota tano hapo bado matibabu kisa si Mtanzania.

Huyu mgonjwa ni mtu ambaye ameishi Tanzania zaidi ya miaka mitano; ameoa Mtanzania anaishi hapa, ila Seliani Hospitali hakuna ubinadamu. Wanathamini pesa kuliko uhai wa binadamu.

Kuna siku nakumbuka walimrudisha mgonjwa mahututi kisa hana pesa. Ndugu waliomba wasaidiwe wakatafute pesa, walikataa katu. Hivi hapa ni vipimo walivyotaka walipwe laki na nusu na pia gharama walizochaji kumuona daktari na dakitari hatukumuona, ilibidi tuondoke na mgonjwa wetu.

nenda katibiwe kwenu hamna cha bure hapa, hata huko kwenu mnatufanya hivi hivi, nilishabadilishiwa gharama za hotel baada ya kufahamu mimi siyo raia wa kenya.
 
Huduma za hiyo hospitali ni hovyo sn wanajali pesa tu yaani kufungua faili tu mtu anatozwa zaidi ya elfu 13 huko hlf huduma zao majibu ya vipimo unakuta siyo kbs sina hamu nao hao walitakaga kusabisha kifo kwa wife kwa majibu yao ya uongo

Watu wasizuzuke na jengo lao kwa kudhani liendana na huduma zao hovyo sn



Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Kwasasahv wapo vizuri sana, walikuwa na huo uzembe kipindi cha nyuma kidogo hata Mimi nilitaka kuwahama
 
Back
Top Bottom