ipyax
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 4,147
- 6,521
Tarehe 4 mwezi huu mdogo wangu alipata ajali ya pikipiki eneo biafra akapelekwa mwananyamala hospitali ili apate matibabu. Niliyoyaona pale kwa kweli yanaumiza, sikitisha na kukatisha tamaa.
Mdogo wangu alifikishwa pale saa nne asubuhi na mimi nikafika saa tano na nusu, nimekuta mdogo wangu amewekwa kwenye machela chumba cha upasuaji mdogo hajapata huduma anavuja damu tu. Nikauliza manesi jamani mbona mgonjwa wangu hajahudumiwa..? Amefikishwa hapa zaidi ya saa 1 imepita na nyie mnapiga story tu. Wakawa wakali sana, usitufundishe kazi bwana we huoni wagonjwa ni wengi hapa?
Baada ya hapo nikaandikiwa list ya vifaa na dawa nikanunue ili waweze kufanya kutoa huduma, kwenda duka la dawa la hospitali hawana dawa kabisa, ikabidi niende nje kununua kwenye yale maduka yanayo tizamana na hospitali. How come hospitali ya rufaa ya mkoa wa kinondoni inakosa dawa? Bandage, drip, gauze nk? Huduma mbovu na ndiyo maana watu wanakufa sana pale.
Ndugu yako akiugua serious ukimpeleka pale basi uwezekano wa kufa ni mkubwa sana kuliko kupona. Serikali ifuatilie hili kwa sababu inasema imesambaza madawa hospitali zake lakini dawa hakuna.