Hospitali ya rufaa Mwananyamala ni uwanja wa kifo?

ipyax

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
4,040
6,291
Tarehe 4 mwezi huu mdogo wangu alipata ajali ya pikipiki eneo biafra akapelekwa mwananyamala hospitali ili apate matibabu. Niliyoyaona pale kwa kweli yanaumiza, sikitisha na kukatisha tamaa.

Mdogo wangu alifikishwa pale saa nne asubuhi na mimi nikafika saa tano na nusu, nimekuta mdogo wangu amewekwa kwenye machela chumba cha upasuaji mdogo hajapata huduma anavuja damu tu. Nikauliza manesi jamani mbona mgonjwa wangu hajahudumiwa..? Amefikishwa hapa zaidi ya saa 1 imepita na nyie mnapiga story tu. Wakawa wakali sana, usitufundishe kazi bwana we huoni wagonjwa ni wengi hapa?

Baada ya hapo nikaandikiwa list ya vifaa na dawa nikanunue ili waweze kufanya kutoa huduma, kwenda duka la dawa la hospitali hawana dawa kabisa, ikabidi niende nje kununua kwenye yale maduka yanayo tizamana na hospitali. How come hospitali ya rufaa ya mkoa wa kinondoni inakosa dawa? Bandage, drip, gauze nk? Huduma mbovu na ndiyo maana watu wanakufa sana pale.

Ndugu yako akiugua serious ukimpeleka pale basi uwezekano wa kufa ni mkubwa sana kuliko kupona. Serikali ifuatilie hili kwa sababu inasema imesambaza madawa hospitali zake lakini dawa hakuna.
 
Pole sana Mkuu..!
Kuna Vifo Vingine huwa vinatokea kwa uzembe wetu sisi!
Kuna watu wamefariki nyakati ambazo sio zao kabisa..!

vipi lakini, hujatuambia hali ya mgonjwa...!
 
Bodaboda ni janga,mpaka manesi nao wamechoka.bodaboda hawafuati sheria za barabarani, bodaboda utawakuta hawaheshimu traffic lights,hatima yake wamejaa mahospitalini mifupa imevunjika vunjika,sasa hospitali zimewachoka.
 
Poleni sana, natumaini mdogo wako anaendellea salama.

Hili la hospitali hiyo linawatokea wengi, inashangaza sana hadi leo wafanyakazi na menejimenti ya hospitali haijali.

Mkuu wa mkoa yupo busy na mengine kabisa ya duniani. Mkuu wa wilaya nae ana enjoy kuwa acting RC.

Majipu bado ni mengi sana tena kwa dharau juu, wapo wanaotaka kazi wapewe hao wavivu wapenda rushwa waondolewe.
 
Tarehe 4 mwezi huu mdogo wangu alipata ajali ya pikipiki eneo biafra akapelekwa mwananyamala hospitali ili apate matibabu. Niliyoyaona pale kwa kweli yanaumiza, sikitisha na kukatisha tamaa.

Mdogo wangu alifikishwa pale saa nne asubuhi na mimi nikafika saa tano na nusu, nimekuta mdogo wangu amewekwa kwenye machela chumba cha upasuaji mdogo hajapata huduma anavuja damu tu. Nikauliza manesi jamani mbona mgonjwa wangu hajahudumiwa..? Amefikishwa hapa zaidi ya saa 1 imepita na nyie mnapiga story tu. Wakawa wakali sana, usitufundishe kazi bwana we huoni wagonjwa ni wengi hapa?

Baada ya hapo nikaandikiwa list ya vifaa na dawa nikanunue ili waweze kufanya kutoa huduma, kwenda duka la dawa la hospitali hawana dawa kabisa, ikabidi niende nje kununua kwenye yale maduka yanayo tizamana na hospitali. How come hospitali ya rufaa ya mkoa wa kinondoni inakosa dawa? Bandage, drip, gauze nk? Huduma mbovu na ndiyo maana watu wanakufa sana pale.

Ndugu yako akiugua serious ukimpeleka pale basi uwezekano wa kufa ni mkubwa sana kuliko kupona. Serikali ifuatilie hili kwa sababu inasema imesambaza madawa hospitali zake lakini dawa hakuna.
mkeo akienda kujifungulia mwananyamala uweke asilimia 80 ya kuwapoteza mama na mtoto au mmoja kati yao
 
Serikali gani ifuatilie? hii ya ccm?
CCM ndo jeneza la watanzania.
 
Kamwe Huduma za afya hasa kwenye Hosp za Serikali hazitaweza kuwa bora kwa mwendo huu wa kutoa huduma bure na misamaha kibao.. Wengi wanoenda kutibiwa ni maskini na wengi wao hata kodi hawalipi.. Zinahudumia Wagonjwa wengi wasiowiana na vifaa tiba , madawa , rasilimali watu na kibaya zaidi miundombinu... Tutaendelea kulalamika milele..
 
Lakini hilo si sababu ya kuacha kumpa mtu huduma. Okoa maisha ya mtu unapoweza
Ajali za bodaboda nyingi ni za kizembe,hosoitali zina msongamano wa wagonjwa wa malaria ambayo unauwa kuliko bodaboda.
 
Pole sana Mkuu..!
Kuna Vifo Vingine huwa vinatokea kwa uzembe wetu sisi!
Kuna watu wamefariki nyakati ambazo sio zao kabisa..!

vipi lakini, hujatuambia hali ya mgonjwa...!
Mgonjwa wangu anaendelea vizuri mkuu, asante.
 
Bodaboda ni janga,mpaka manesi nao wamechoka.bodaboda hawafuati sheria za barabarani, bodaboda utawakuta hawaheshimu traffic lights,hatima yake wamejaa mahospitalini mifupa imevunjika vunjika,sasa hospitali zimewachoka.
Hata kukujibu nimeshindwa lakini ombea yasikukute wewe wala mtu wako wa karibu.
 
Pole Mkuu. Next time nenda hospital binafsi ufanye mlinganisho wa Huduma then utupe mrejesho.
 
Azimio la abuja limetekelezwa kwa kiwango gani hata tatizo liwe watoa Huduma za Afya badala ya serikali?
Tembelea ofisi za bima za Afya au NHIF wenyewe upate card ya uanachama ili next time ukiugua uchague hospital nzuri ya binafsi utibiwe. Vinginevyo utalalamika sana. Afya ni kipaumbele kwa maneno na makabrasha ila si kwa vitendo.
 
Mmmh pale unakufa huku unajiona,hasa wamama wajawazito duu wanakumbana na mengi,mi mke wangu alichomwa na sindano iliyopinda mkono ulivimba sana tena aliwaambia mbona hyo sindano imepinda wakamjibu hivohivo kuwa wewe unajua sana kuliko sisi,badae daktar mkuuu kauliza mbona umevimba hivi wife kamwelezea akasema naogopa kuchukua action kwa aliyekufanyia hivi kwa kua unaweza umizwa zaidi ya hivi,pana mengi pale sema basi tu,hasa wamama wajawzito kama mkeo ni mjamzito usithubutu kumpeleka hapo hospital utakuja juta maisha yako yote
 
Back
Top Bottom