Majeneza getini mwa Hospitali ya Amana hayaleti taswira nzuri kwa Wagonjwa.

mkaskaz

JF-Expert Member
May 24, 2018
576
820
Habari wanaJamiiForums. Kwanza nimshukuru Mungu kwa uzima tulionao. Pili nishukuru kwa jukwaa hili ambalo linatupa fursa ya kutema nyongo zetu kwa usalama.

Kwa yeyote kati yetu ambaye ameshawahi kufika hospitali ya Mkoa wa Dar es Salaam (Hospitali ya Rufaa) atakubaliana na mimi kwamba kuna majeneza yanauzwa getini pale. Yaani kabla hujaingia hospitalini unakaribishwa na majeneza yakiuzwa kushoto na kulia mwa barabara. Jambo hili linaleta ukakasi kwelikweli kwa wagonjwa. Yaani linamnyong'onyesha mgonjwa anayeenda kupambania afya yake, kwamba asipotoboa jeneza linamhusu.

Mimi nadhani wauza majeneza wangetafuta sehemu nyingine angalau iliyojificha na siyo pale. Siamini kama ndio utaratibu wa hospitali kubwa za serikali. Kwa muono wangu mimi siyo sawa, na ninaomba mamlaka husika zichukue hatua haraka kurekebisha hili.

Jambo la pili tunaomba Serikali inunue jenereta kubackup umeme unapokatika kwenye hospitali kubwa. Amana kwa mfano, umeme ukikatika na huduma zote zinasimama mpaka urudi. Si sawa kwa hospitali ya Rufaa kukosa jenereta.

NB: Nimetumia Hospitali ya Amana kama kielelezo hai. Kama kuna Hospitali zingine zenye mazingira kama haya na zenyewe ziangaliwe.

Ahsante.
 
Umeongea jambo la maana
hapa inaonyesha hata kama mgonjwa alikua hana presha
anaweza kufa kwa ugonjwa mwingine tofauti na ule
uliompeleka pale
Nb:
Nasikia Janabi anampango wa kuomba wapewe figo kwa marehemu kama hawa?
Hivi kwa watu wanaopata ajali viungo vyao huwa hawavichui kweli?
 
Back
Top Bottom