askarikambi
JF-Expert Member
- Dec 22, 2013
- 246
- 263
Jumatano, Machi 6, 2019 nimefika katika hospitali yetu ya rufaa Mkoa wa Tanga, almaarufu kama "Bombo hospital" kumsindikiza mke wangu kupata matibabu.
Ni muda sasa tangu nimefika katika hospital hii, ambayo inasemekana kuwa, ndio mahali ambapo hospital ya kwanza ya serikali ilijengwa hapa.
Sina tatizo na mengine yanayoendelea hapa, nikiamini ni changamoto za kiutendaji katika hospitali nyingi za umma hapa nchini.
Ila leo, nataka kusema hili la mapokezi. Na kama wahusika ujumbe huu ukiwafikia, ni vizuri kuchukua hatua ili kusaidia jamii yetu.
Nimesikitishwa sana na kitendo cha mapokezi kuchelewa kumtoa kwenye gari la wagonjwa "ambulance" mgonjwa aliyeletwa kwa zaidi ya robo saa kama sio nusu saa kwa madai ya kuwa hakuna kiti cha magurudumu "wheelchair" au kitanda, huku hakuna jitihada za wazi kufanikisha hilo, hadi nesi aliyekuja na mgonjwa kulalamika huku akimuomba dereva wa ambulance arekodi muda waliofika hapo.
Nilichojiuliza, hawa mapokezi, wanajua ugonjwa au hali ya mgonjwa huyu aliyeletwa kwa ving'ora?
Kwanini hospital isiwe na utaratibu wa kuhakikisha hawakosi vifaa vya mapokezi ya wagonjwa?
Niwashauri Bombo, rekebisheni hili, wagonjwa wasifie mapokezi kwenu! Mnaweza kusema haijawahi kutokea, lakini kwa hili la leo, mnaweza sababisha kifo. Na jambo hili halikunigusa peke yangu, wengi tuliokuwa mapokezi lilitusikitisha, hasa vile tulivyokuwa tukimuona nesi aliyeleta mgonjwa akihangaika bila msaada kumshusha mgonjwa wake.
Jambo jingine nililoliona tofauti pale Bombo, ni eneo linaposimana gari la wagonjwa. Kwenye hospital nyingine, eneo hilo huwa limezibwa juu ili mvua au jua lisiwe tatizo katika zoezi la kumshusha mgonjwa. Hapa pako wazi, sijui wakati wa mvua wanawashusha na mwamvuli!!
Na mwisho ni mama mmoja kwenye meza ya mapokezi, sitasema sana juu yake, ila wamshauri tu kuwa, yupo pale kusaidia, hivyo awe na kauli nzuri. Kwa muda mchache niliokaa hapo, nimemuona hana PR nzuri kwa wateja, nilikuwa naangalia anavyojibu na kuona sintofahamu wanayoipata wateja wake.
Ashauriwe apunguze ukali, aelekeze badala ya kukosoa maelezo ya wateja wake. Ashautiwe tu.
Sisemi mengine kwa Bombo, rekebisheni mapokezi ya wagonja, najua changamoto zipo kila mahali.
Kazi njema.
Sent using Jamii Forums mobile app