Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo: Kitengo cha Mapokezi wajirekebishe

askarikambi

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
246
263
Jumatano, Machi 6, 2019 nimefika katika hospitali yetu ya rufaa Mkoa wa Tanga, almaarufu kama "Bombo hospital" kumsindikiza mke wangu kupata matibabu.

Ni muda sasa tangu nimefika katika hospital hii, ambayo inasemekana kuwa, ndio mahali ambapo hospital ya kwanza ya serikali ilijengwa hapa.
Sina tatizo na mengine yanayoendelea hapa, nikiamini ni changamoto za kiutendaji katika hospitali nyingi za umma hapa nchini.

Ila leo, nataka kusema hili la mapokezi. Na kama wahusika ujumbe huu ukiwafikia, ni vizuri kuchukua hatua ili kusaidia jamii yetu.

Nimesikitishwa sana na kitendo cha mapokezi kuchelewa kumtoa kwenye gari la wagonjwa "ambulance" mgonjwa aliyeletwa kwa zaidi ya robo saa kama sio nusu saa kwa madai ya kuwa hakuna kiti cha magurudumu "wheelchair" au kitanda, huku hakuna jitihada za wazi kufanikisha hilo, hadi nesi aliyekuja na mgonjwa kulalamika huku akimuomba dereva wa ambulance arekodi muda waliofika hapo.

Nilichojiuliza, hawa mapokezi, wanajua ugonjwa au hali ya mgonjwa huyu aliyeletwa kwa ving'ora?
Kwanini hospital isiwe na utaratibu wa kuhakikisha hawakosi vifaa vya mapokezi ya wagonjwa?

Niwashauri Bombo, rekebisheni hili, wagonjwa wasifie mapokezi kwenu! Mnaweza kusema haijawahi kutokea, lakini kwa hili la leo, mnaweza sababisha kifo. Na jambo hili halikunigusa peke yangu, wengi tuliokuwa mapokezi lilitusikitisha, hasa vile tulivyokuwa tukimuona nesi aliyeleta mgonjwa akihangaika bila msaada kumshusha mgonjwa wake.

Jambo jingine nililoliona tofauti pale Bombo, ni eneo linaposimana gari la wagonjwa. Kwenye hospital nyingine, eneo hilo huwa limezibwa juu ili mvua au jua lisiwe tatizo katika zoezi la kumshusha mgonjwa. Hapa pako wazi, sijui wakati wa mvua wanawashusha na mwamvuli!!

Na mwisho ni mama mmoja kwenye meza ya mapokezi, sitasema sana juu yake, ila wamshauri tu kuwa, yupo pale kusaidia, hivyo awe na kauli nzuri. Kwa muda mchache niliokaa hapo, nimemuona hana PR nzuri kwa wateja, nilikuwa naangalia anavyojibu na kuona sintofahamu wanayoipata wateja wake.

Ashauriwe apunguze ukali, aelekeze badala ya kukosoa maelezo ya wateja wake. Ashautiwe tu.
Sisemi mengine kwa Bombo, rekebisheni mapokezi ya wagonja, najua changamoto zipo kila mahali.

Kazi njema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MGONJWA AKISUBIRI KUSHUSHWA BOMBO HOSPITAL.
IMG_20190306_103453.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio kamawaida yao hao hawajali wamezoea watu kufa,ukienda kufungua faili hapo mapokezi wapo too slow kwenye kujaza taarifa za mgonjwa utaona mtu wa mapokezi anatafuta herufi kwenye keyboard ya kompyuta,utadhani mtoto was chekechea anajifunza namna ya typing! Inachosha na kukera sana.
Mwingine nilimwona anasikiliza muziki badala ya kusikiliza wagonjwa huku akiwa hapo mapokezi.
Nikajiuliza ina maana hospitali hii haina uongozi au wameajitiana kindugu na kujuana na sio kitaaluma!!?
Wajirekebishe tumechoka!!
 
Hospitali nyingi tu za serikali ni wazembe nilishashuhudia mgonjwa aliyetakiwa awahishwe na ambulence hospital nyingine kubwa lakin wamejivuta vuta mpk mgonjwa kafia njiani
 
Tanzania kitu pekee tujuacho ni unafiq mambo muhimu kama haya watu tunayafumbia macho

hadi siku mtoto wa mkubwa yakimkuta ndo watajifanya kurekebisha na kuwawajibisha wahusika
 
Jumatano, Machi 6, 2019 nimefika katika hospitali yetu ya rufaa Mkoa wa Tanga, almaarufu kama "Bombo hospital" kumsindikiza mke wangu kupata matibabu.

Ni muda sasa tangu nimefika katika hospital hii, ambayo inasemekana kuwa, ndio mahali ambapo hospital ya kwanza ya serikali ilijengwa hapa.
Sina tatizo na mengine yanayoendelea hapa, nikiamini ni changamoto za kiutendaji katika hospitali nyingi za umma hapa nchini.

Ila leo, nataka kusema hili la mapokezi. Na kama wahusika ujumbe huu ukiwafikia, ni vizuri kuchukua hatua ili kusaidia jamii yetu.

Nimesikitishwa sana na kitendo cha mapokezi kuchelewa kumtoa kwenye gari la wagonjwa "ambulance" mgonjwa aliyeletwa kwa zaidi ya robo saa kama sio nusu saa kwa madai ya kuwa hakuna kiti cha magurudumu "wheelchair" au kitanda, huku hakuna jitihada za wazi kufanikisha hilo, hadi nesi aliyekuja na mgonjwa kulalamika huku akimuomba dereva wa ambulance arekodi muda waliofika hapo.

Nilichojiuliza, hawa mapokezi, wanajua ugonjwa au hali ya mgonjwa huyu aliyeletwa kwa ving'ora?
Kwanini hospital isiwe na utaratibu wa kuhakikisha hawakosi vifaa vya mapokezi ya wagonjwa?

Niwashauri Bombo, rekebisheni hili, wagonjwa wasifie mapokezi kwenu! Mnaweza kusema haijawahi kutokea, lakini kwa hili la leo, mnaweza sababisha kifo. Na jambo hili halikunigusa peke yangu, wengi tuliokuwa mapokezi lilitusikitisha, hasa vile tulivyokuwa tukimuona nesi aliyeleta mgonjwa akihangaika bila msaada kumshusha mgonjwa wake.

Jambo jingine nililoliona tofauti pale Bombo, ni eneo linaposimana gari la wagonjwa. Kwenye hospital nyingine, eneo hilo huwa limezibwa juu ili mvua au jua lisiwe tatizo katika zoezi la kumshusha mgonjwa. Hapa pako wazi, sijui wakati wa mvua wanawashusha na mwamvuli!!

Na mwisho ni mama mmoja kwenye meza ya mapokezi, sitasema sana juu yake, ila wamshauri tu kuwa, yupo pale kusaidia, hivyo awe na kauli nzuri. Kwa muda mchache niliokaa hapo, nimemuona hana PR nzuri kwa wateja, nilikuwa naangalia anavyojibu na kuona sintofahamu wanayoipata wateja wake.

Ashauriwe apunguze ukali, aelekeze badala ya kukosoa maelezo ya wateja wake. Ashautiwe tu.
Sisemi mengine kwa Bombo, rekebisheni mapokezi ya wagonja, najua changamoto zipo kila mahali.

Kazi njema.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu hapo Bombo hilo Tatizo la Lugha isiyo ya kuridhisha wanayotoa Wahudumu wa hapo Mapokezi ni la Muda mrefu,lakini hamna jitihada zozote zilizochukuliwa.

Isitoshe hilo la Lugha Chafu kwa Wagonjwa siyo hao tu bali hata Kiongozi wao ambaye ni Mganga Mfawidhi wa hiyo Hospital hana lugha nzuri hasa kwa Ndugu wa Wagonjwa.

Nilishawahi kuwa na Mgonjwa wangu kule Grade.Kuna siku alipokuja huyo Mganga Mfawidhi akataka kuniondoa tena kwa lugha isiyo sahihi(siwezi andika humu),baadae alipojua mimi ni nani ndiyo akaanza omba samahani.Kazi hazifanywi hivyo.

Wahusika fuatilieni haya Matatizo hapo Bombo ili Mchukue hatua stahiki.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
alipojua mimi ni nani ndiyo akaanza omba samahani
Sasa kama alipojua wewe ni nani akakuomba samahani, then if you are a high placed man, it is you who has a duty to take action! The Medical officer incharge, I know him personally, he is an approachable man, talk to him. But he has his immeadiate boss, the RAS, why not report him ?
 
Sijaona hoja yako ya Msingi.Kama unamfahamu ni vyema Mwambie ajirekebishe maana hata Mimi nilimueleza ukweli juu ya lugha yake chafu.

Pia hii ni sehemu ya kusemea maana hata huyo Boss wake anapitia hapa.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mgosi ungewapiga zongo tu.
Kwanini ulalamike zongo Tanga mwalijua?
 
Back
Top Bottom