Hospitali ni zaidi ya majengo

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
17,265
17,962
Wengi mtakuwa mmesikia jinsi serikali ya awamu ya tano inavyojinasibu kuhusu ujenzi wa hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati. Maeneo mengi kuna ujenzi unaendelea na Waziri Jafo yupo kila sehemu akikagua. Ni jambo jema lakini kuna maswali ya kujiuliza.

Ujenzi huo si sawa na barabara au daraja kwamba vikiwa tayari basi, matumizi yake yanaendelea bila kuhitaji rasimali nyingine.

Hospitali na vituo vya afya si majengo peke yake. Lazima kuwe na madaktari, manesi, watu wa maabara, wafamasia nk. Na kuna viwango na idadi yake. Lazima kuwe na vifaa tiba.
Hospitali zilizopo zina upungufu mkubwa wa vitu hivyo. Hakuna watalaam wala vifaa tiba. Hao wakufanya hizo sehemu mpya watatoka wapi?

Gharama ya hospital ya wilaya isiwe ya majengo pekee bali ijumuishe watalaam na vifaa stahili. Mitaani kuna madaktari hawana kazi lakini hospitali zote zina upungufu mkubwa wa watalaam. Kupanga ni kuchagua. Bombardier moja inaweza kutupa hospital nyingi zilizokakamilika – majengo, vifaa tiba, madaktari, wauguzi, wafamasia nk.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom