Hospital Yenye kipimo cha aleji

Hospital Yenye kipimo cha aleji

plock

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2016
Posts
501
Reaction score
567
Habari wakuu naomba mwenye kuweza kunisaidia hospital Bingwa nitakayoweza kufanyiwa vipimo na kutambua aleji ya vitu vinavyonitesa

Ninakuwa na mafua na pua kuziba na kusababisha koo kuwa na makohozi kwasababu ya mafua , au dawa itakayoweza kunisaidia kunitibu au kupata hali ya unafuu. Nitashukuru kwa msaada
 
Pole sana chief...
Kwa kuanzia epuka mazingira ya vumbi, spray zenye harufu kali, pia ikiwezekana nawa uso bila sabuni ili isiingie puani ....
Kingine ukipenge kamasi, usitumie vile vitambaa dizain kama taulo vyenye nyuzi nyuzi ....

Miaka hiyo mafua yamenisumbua sana, now namaliza hata miez6 bila kuumwa mafua

All the best ....
 
Ekenywa ipo magomeni wapo vizuri
 
Tumia mchanganyiko wa Tangawizi,limao,kitunguu saumu na Asali utapona
Kwa nilivyomuelewa ni tatizo lake la kudumu so anahitaji kufanya vipimo ili ajue source ya tatizo lake, ambalo labda akijua tatizo anaweza kupata solution ya kudumu
 
Asante sana najitahidi katika hili pia lakini nawasiwasi na vyakula au viungo vinavyotumika kwenye mboga au chakula kama chapati nikija haichukui nusu saa naona reaction lakini vingine bado sijajua kutokana na viungo vinavyotumika kujua ni kipi
 
Tumia mchanganyiko wa Tangawizi,limao,kitunguu saumu na Asali utapona
Asante sana nitafanyia kazi hili maana nimetumia nasal drops kwa miaka mingi pamoja na cetirizine kwa muda mrefu
 
Ekenywa ipo magomeni wapo vizuri
Asante ngoja nitafute mawasiliano yao kujua nianzie wapi kama naanza safari nipo mkoani Iringa ili niwe nahakika ninachokifata dar
 
Ekenywa ipo magomeni wapo vizuri
Asante ngoja nitafute mawasiliano yao kujua nianzie wapi kama naanza safari nipo mkoani Iringa ili niwe nahakika ninachokifata dar
 
Kwa nilivyomuelewa ni tatizo lake la kudumu so anahitaji kufanya vipimo ili ajue source ya tatizo lake, ambalo labda akijua tatizo anaweza kupata solution ya kudumu
Ni kweli ni la miaka mingi navumilia na kumeza cetirizine pamoja na nasal drop kwa ajili ya kunipa nafuu pua kuziba
 
Asante ngoja nitafute mawasiliano yao kujua nianzie wapi kama naanza safari nipo mkoani Iringa ili niwe nahakika ninachokifata dar
Jaribu hii 0717 574 546 japo pana foleni sana, ila natumai utasaidiwq
 
Wewe ni Mimi mi nimechoka sasa nayaacha kama yalivyo na baridi la mbeya ukichanganya na vumbi ni mateso kwa kweli, dawa Huwa natumia mentholdox at least Huwa inanisaidia
 
Pole sana aisee. Niliangaika sana na binti yangu alipokuwa mdogo kisa hayo mafua ya allergy.
Kila sehemu naambiwa vitu tofauti had nachoka. Ni mpaka pale nilipoamua kutafuta mwenyewe chanzo. Nikaanza kuandika kila alichotumia, alichokula nk kwa siku. Nikawa namuachisha kitu kimojakimoja kisha naangalia maendeleo yake. Ni zoezi la muda, ila lilinipa majibu, kuwa kitu chochote kikikaa kwenye frij, hata kama kitatolewa kwa muda, akila lazima ataumwa mafua. Ameacha na sasa zaid ya miaka 8 tatizo la mafua ya kudumu limeisha.
Unaweza usiende hospital, ila jichunguze mwenyewe, aina ya vyakula, mazingira yanayokuzunguka( matumizi ya feni, A/C, manukato unayotumia au wanaokuzunguka, vumbi, moshi/ sigara nk)
 
Pole sana Ngoja tuendelee kufata ushauri wa wadau ipo siku mtego utateguka wa hizi changamoto
 
Pole sana aisee. Niliangaika sana na binti yangu alipokuwa mdogo kisa hayo mafua ya allergy.
Kila sehemu naambiwa vitu tofauti had nachoka. Ni mpaka pale nilipoamua kutafuta mwenyewe chanzo. Nikaanza kuandika kila alichotumia, alichokula nk kwa siku. Nikawa namuachisha kitu kimojakimoja kisha naangalia maendeleo yake. Ni zoezi la muda, ila lilinipa majibu, kuwa kitu chochote kikikaa kwenye frij, hata kama kitatolewa kwa muda, akila lazima ataumwa mafua. Ameacha na sasa zaid ya miaka 8 tatizo la mafua ya kudumu limeisha.
Unaweza usiende hospital, ila jichunguze mwenyewe, aina ya vyakula, mazingira yanayokuzunguka( matumizi ya feni, A/C, manukato unayotumia au wanaokuzunguka, vumbi, moshi/ sigara nk)
Asante sana kunipa muongozo ngoja nianze na hii kwa kujitibia kufata muongozo wa kula kwa awali nilionekana nina changamoto ya maziwa na bidhaa zinazohusiana na hivyo pamoja na kitu chochote kinachotumia nyanya pamoja nimeacha lakini hakuna kitu
 
Back
Top Bottom